Tunasema ni siku nyingine kwakuwa kulikuwa na siku kabla ya
leo………………….!
Karibu…………….!
Unaweza kukaa na mtu kwa muda mwingi ukicheka naye na hata kutaniana
naye na hata ikiwezekana kula pamoja naye, ukawa mvumilivu kwa huyo mtu na hata
ukaacha baadhi ya shughuli zako kwa ajili ya kutoa umakini wako wote ukitaka
kujua ujio wa huyo mtu ulikuwa na lengo gani hasa?
Kwa kiasi kikubwa ujio wa mtu kwako unaweza kuubashiri katika
muonekano wa sura pamoja na tone ya sauti yake ( huzuni au furaha ) uweza
kubashiri kitu na kuanza kuandaa moyo wako kupokea kitu kitakachosemwa na mtu
husika.
Na inakuwa mchanganyo kidogo kama sio sana pindi utakapo
bashiri kitu ambacho mtu atasema na wewe lakini ikiwa tofauti kabisa na kile
anachosema, mathalani unaweza ukawa na changamoto ya kifedha ghafla mgeni
akakutembelea na kwa muonekano wa kawaida ukajua kuwa huyu mtu yuko vema nawe
ukafikiri hapa ndipo mahali pa kuponea ili siku hiyo isipite bure lakini
ukashangaa mtu huyo anakwambia “ biashara zangu zimekwama kidogo ningepata
kiasi fulani cha fedha kingenisaidia katika kipindi hiki “
Bila shaka ukiwa na moyo mdogo unaweza kujikuta kimoyomoyo
unaomba aondoke tu maana hana faida kwako kwa wakati huo na ikitokea anaendelea
na mazungumzo mengine unaweza kujibambikizia shughuli ya kufanya hapohapo tu
ili mradi tu aondoke au ukaunda safari ya ghafla ili mradi uepukane naye.
Ni jambo la kawaida tu unapomuhitaji mtu kuongea naye ukweli
vinywaji na chakula vinaweza visiwe vya msingi kwake bali kile kiini/lengo kuu
la kikao hicho ndicho kitakuwa cha maana kwake.
Hutakosa kusikia mtu katika hali ya kujuta baada ya
kutopendezewa na jambo la msingi lililoendelea katika mazungumzo hayo……………..hizi
ni baadhi ya kauli zake:
“ mi nilifikiri ameniitia jambo la maaaaana sana kumbe hakuna
kitu “
“ tangia siku hile ya kile kikao na alichoniambia thamani
yake nimeishusha kabisa kwangu mimi nilifikiri ataniambia jambo la msingi kumbe
ujinga mtupu “
NOTE: Ni jambo la msingi wakati mwingine mkanganyo mkubwa
utokea katika jambo husika lakini linaweza lisiwe la msingi kwa sasa lakini
likawa la msingi katika hatua inayofuata katika maisha yako.
Karibu katika somo……………………………………………!!!
Katika jambo lolote linalo muhusisha Mungu jua katika
utendaji mzima wa hilo jambo linamuhitaji Mungu kuliko kitu chochote, na ni
muhimu zaidi kuliko oxgen katika maisha ya mwanadamu maana ukikosa oxgen
unaweza kufa kimwili ila ukimkosa Mungu utaangamia roho na mwili pia.
Na hata katika mambo ya kushirikiana katika shughuli za
kibiashara la muhimu nguvu ya uchumi na wazo lililobora ulilokuwa nalo.
Ni kweli kabisa katika kufanikisha mambo mengi, watu na mtaji
ni muhimu lakini sio muhimu kuliko Mungu, kwakuwa vyote vya tokana na Mungu.
Na ni muhimu kujua ili ufanikishe mambo ya kimungu katika
hali yoyote ni muhimu sauti ya Mungu iwe nguvu katika moyo wako kuliko jambo
lolote, sauti zisizo ambatana kweli ya Mungu zisiwe na nguvu kwako kwakuwa watu
uliwakuta na utawaacha lakini Mungu ulikuwa naye kabla ujatokea katika
ulimwengu wa nyama na hata hitimisho lako limebebwa na yeye.
Sizungumzii kuwa watu sio wa muhimu la hasha! Bali hekima
inahitajika katika utendaji maana hakuna aliyezaidi ya mwingine wala aliye
chini ya mwingine! Ila katika yote Mungu anabaki kuwa Mungu.
Ukimfanya Mungu kama kiongozi wako na ikiwa jambo LA MSINGI
katika maisha yako hauwezi kupoteza na kufika kwenye hatima yako ni jambo
lisilopingika.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………..................…………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni