Ni kauli au msemo ulio na hali ya ugumu au kutowezekana pindi
utakapo amua kuutafakari kwa kina “maisha
yake ndani yangu” !!!
Ni ngumu tu kuishi ndani ya maisha ya mwingine! Kwakuwa yeye
anayo ya kwake (anayoyapenda/ matakwa yake) na wewe unayo ya kwako (ubinafsi)
na kila mtu ujisikia vizuri kuishi maisha anayoyataka, maisha ya uhuru binafsi
ndiyo yanayopelekea furaha ya kweli…!
Japo inawezekana kwakuwa endapo utaishi katika hali hii itafanya
wepesi kuyapata mambo ya mwingine pindi utakapoishi huku ukiufurahisha moyo
wake, hapo utayajua kwa mapana zaidi yanayoendelea moyoni mwake na kufaidika
matunda yake.
Kuna kutamani kuishi maisha ndani ya mtu na kuna kuthubutu na
kudumu katika maisha ya mwingine!
Ni furaha ya mzazi kuona mtoto wake anafanana naye katika
muonekano lakini inakuwa na maana zaidi kwake kama mwenendo wake utafanya
wengine wabarikiwe/wapendezwe nao.
Unapokuwa ujui njia ni vigumu tu kuwa kiongozi wa hiyo
safari, maana hamtofika mnapotakiwa kwenda na hata ikatokea bahati umefika
unaweza usijue kama umefika maana huna mwelekeo sahihi wa wapi unatakiwa kwenda
au kuwa.
Kuyaishi maisha ya mwingine lazima uweze kuyasahau maisha
yako, kiwango cha kuyasahau maisha yako ndicho kiwango cha kuyaishi maisha ya
mwingine.
Moja ya kitu kinachoweza kuleta mshikamano zaidi/kuongezeka
kwa upendo ni namna ya kila mtu mmoja kujisahau na kuanza kuishi kwa ajili ya
mwenzake tu.
1 petro 4:8…zaidi ya yote iweni
na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa
dhambi.
“ Maisha yake ndani
yangu” hama! Ni
kauli iliyojaa lugha ya kufikirika sana kama sio ya picha na hali ya
kutowezekana kwa mtu kuishi ndani ya maisha ya mwingine kwa kuwa kila mtu
anaishi maisha yake na zaidi sana matakwa hayafanani na hata ya kifanana sio kwa
asilimia zote.
Kuna mambo mengi utayapata endapo utakubali kuishi ndani ya
mtu na kuna mambo utayakosa endapo utaishi nje ya mfumo huo hata kama
utaonyesha utayari kiasi gani kwa huyo mtu?
Ni kusudi la Mungu kuona tunaishi katika maisha yake ili
kuyafikia yale yaliyo mipango yake.
Ufike hatua ya kuonyesha ni kweli unaishi lakini sio maisha
yako bali wewe unaifuata njia ambayo wengine awaioni au awaielewi.
Yohana 8:29……Naye aliyenipeleka
yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale
yampendezayo.
Raha ya kitu ni pale utakapoamua kukipendeza kwa asilimia mia
nacho kitafanya au kudhihirika na kupata faida.
Bidii yako ya kuishi nje yako ndio neema ya yule unayeishi
kwa ajili yake inaongezeka katika maisha yako.
“ Nje yake hakuna vitu vyake bali ndani yake
kuna mambo yake”
Usitegemee kupata vya kwake kama ukiamua kuishi nje yake
maana nje yake hakuna neema yake.
Usipoteze muda kufikiria maisha yake ndio maisha yako wakati
namna sahihi ya kufanya ili yeye aishi kupitia wewe hipo.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni