Ijumaa, 1 Mei 2020

MAJIBU YALIYO NDANI YA UTULIVU




Moja ya kitu kinachosababisha majuto katika maisha ya mtu ni kufanya maamuzi akiwa katika hali ya kukosa utulivu, wakati mwingine hali hii ya kukosa utulivu inaweza sababishwa na hasira pamoja na jazba. Mathalani mtu mmoja pindi atakapoamua kumchoma kisu mwenzi wake kwasababu ya jambo baya alilolifanya au kwakuhisi tu……….baadae, hicho kitendo alichokifanya kinaweza kumgharimu maisha yake hata kujuta kwanini amefanya hilo jambo hata kujikuta yuko jela au uraiani katika maisha ya mateso.

Niseme wazi katika hali yoyote iliyo ndani ya moyo wa mwanadamu uwa inatoa majibu inawezekana katika hali ya utulivu au kukosa utulivu bado kutakuwa na majibu, japo sio kila kila jibu unalolitoa linaweza kuwa sahihi katika swali ambalo unalopaswa kulijibu ndomana ata katika mitaala ya elimu unapopewa mtihani na kuamua kujibu unaweza kupata au kukosa!

Inaaminika majibu sahihi au mazuri yanategemea sana ulimwengu wa utulivu, maana hapo panakutafakari maisha yatakayoendelea mara baada ya kutoa maamuzi au majibu katika jambo husika.

Kwani moja ya sifa ya majibu yatokanayo na hali ya utulivu ni majibu yaliyojaa usalama ndani yake na wala sio kisasi wala kukomoa.

Ni muhimu kutokukubali kusema kwakuwa watu wanakujaza upepo  wa kusema hama kuona nisiposema heshima yangu itashuka hama wazfa wangu utakosa nguvu.

Ni muhimu huo utulivu ubebwe na Mungu mwenyewe na wala sio akili zako, maana akili zako zinaangalia maslahi yako lakini Mungu anaangalia maslahi ya ufalme wake, kwakuwa kwa kiasi kikubwa maslahi yako yanawezaleta uharibifu katika ufalme wa Mungu lakini ufalme wa Mungu utaimarisha maisha yako.

Utulivu katika Mungu ni jambo jema sana na wala sio kitu cha kuzoelea bali ni kitu cha kuwa makini nacho ili kikurahisishie kufikia hatma yako, ni afadhali ukose vyote lakini uwe na utulivu wa kutosha na Mungu maana kupitia hali hiyo inakuwa rahisi kutembea katika mwelekeo na Mungu utakaokupa mwanga katika maisha yako.

Ni muhimu uhakikishe jibu lako linajenga ufalme wa Mungu na wala sio kustawisha nafasi/heshima  yako maana nafasi yako inakipindi tu cha muda fulani na wala sio cha milele ndomana wanasema “ cheo ni dhamana “.

Unahitaji kujua thamani uliyonayo mbele za Mungu ndio hiyohiyo aliyonayo mtu mwingine, hivyo tambua hakuna mwenye nafasi zaidi ya mwingine hivyo jibu lako lijengwe katika upendo wa kristo. ( mpende jirani yako kama nafsi yako ).

Unahitaji kuona kama Mungu anavyoona ili uweze jibu kama Mungu angelikuwepo angelijibu.

“ majibu yako ya leo ndio mstakabali wako wa kesho”
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey  Nelson…………………………………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni