Moja ya kazi ya macho ni kuona na akili kutafsiri kile
ulichokiona,hivyo ni muhimu uone ili uweze kujua kuwa haya mema au si mema!
Utakapo amua kuishi katika macho ya nyama utaona mema mengi
yanayokuvutia na hata kukushawishi kuyapata hivyo hivyo ukiishi katika Mungu
utaona mema ya Mungu japo wakati mwingine yanaweza yasivutie.
Ni jambo la kawaida binadamu kupenda mema au kutendewa mema
na pindi anapokosa kuyapata hayo mema uweza kujikuta kuishi maisha ya ukiwa.
Ni kweli sio kila mema unayoyaona yanaweza kukupeleka pema
hasa yanayotokana na macho ya nyama, kwakuwa chochote ili kikupate ni lazima kiwe
katika hali ya kukuvutia ( muonekano wa nje kama kuna mema ). Na ndomana ata
Eva ili ale tunda kwanza alivutiwa nalo na pia alishawishika na hali ya kujua
mema na mabaya.
Usitegemee kuona mema nje ya kile kilichoko ndani yako, dunia
ikiwa na nguvu ndani yako basi hapo tegemea macho ya nyama kuwa na nguvu basi
hapo inakuwa ngumu kuona kwa jicho la Mungu.
Japo wakati mwingine unaweza kuwa na Mungu lakini usiyaone
mema ya Mungu kwasababu akili imekataa kukubaliana na macho ya Mungu.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mema ya macho na mema ya
Mungu!
Ni tarajio la Mungu tuone mema kupitia yeye ( Ruth &
Ibrahim ) maana katika yeye mema yanapatikana lakini sio mema yanayozaliwa na
macho nyama, uharibifu unaweza kuzaliwa au kupatikana.
Mema ya macho yana mwisho, haijalishi hayo mema unayatazama
vipi au yana mng’ao upi jua kuna mahala itafika mwisho haijalishi uliutegemea
au haukutegemea…kwa kuwa chochote kinachoonekana kwa macho, mara nyingi
kinakuwa kimetengenezwa au kimejitengeneza na uwa vitu vilivyo na sifa hizi uwa
vinakuwa na mwisho kwakuwa vimetoka kwenye mikono ya wanadamu lakini mema
yanayoonwa kwa macho ya Mungu, kwakuwa yanatengenezwa na Mungu na kwakuwa Mungu
hana mwanzo wala mwisho naam ndivyo yatakavyokuwa mambo yake ( kwakuwa vile
alivyo ndivyo mambo yake yatakavyokuwa).
Ni dhana isiyo sahihi kuwa tunaweza pata mambo ya Mungu
kwakuwa watulivu/ wakimya, bali mpaka tumpate Mungu ili tuweze kuona kama
anavyoona, lazima uyaone ili uyapate maana hauwezi kukipata kitu usichokiona.
Wakati mwingine kuna gharama kubwa katika kuyapata mema ya
Mungu kwakuwa wakati mwingine tunayapata mema yake baada ya kukosea sana hivyo
neema ya Mungu inaturudisha katika njia yake au jambo lake.
Ni muhimu kujua kuwa ustawi wako uko mikononi mwake Mungu na
ili uupate ni vyema uone kama yeye anavyoona nje ya hapo mbwembe zote
zitakupeleka shimoni tu.
Hauhitaji mambo mengi, bali unahitaji mema ya Mungu ili uwe
salama na ndipo utaanza kufurahia wokovu wako na maisha yako.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………..0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni