Ijumaa, 29 Mei 2020

MUNGU HAKOSEI




Kitu ambacho MAJAMBAZI, MAFISADI, MAJANGIRI NA HATA WANASIASA…… hawawezi sahau kusema “KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA” hasa wanapokuwa wamepewa nafasi kuongea katika hali ngumu iliyo wakuta watu fulani au jamii kwa ujumla wake.

Naam unaweza kuwa binadamu wa kwanza pindi utakapoinuka na kusema Mungu anamakosa au anakosea! Kwasababu katika hali ya kawaida watu wengi wanamuogopa Mungu kuliko kumuheshimu.

Na utakuwa binadamu wa kawaida kama sio mwenye busara utakaposema MUNGU HAKOSEI! Japo hili neno sio wakati wote linakuwa na maana sana kwa mtu anayelisikia au kulitamka kutokana na mateso au maumivu yaliyo ndani ya moyo wa mtu husika.

Japo wakati mwingine mazingira na uhalisia wa mambo yanayoonekana na kile anachokisema Mungu ina onekana kuwa haiwezekani tena hata kama yeye anasema! Kwa kuwa dhoruba inapokua kali na moyo uweza kupoteza matumaini yake.

Ahadi ya kuingia nchi ya kanani!
Yoshua 1:6 Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.
Imani uweza kufifia pindi unapowaona watu kama majitu!

Hesabu 13:33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
Pindi unapotambua/ kusikia ahadi ya Mungu juu ya maisha yako, usifikiri tu kwasababu amesema basi itakuwa tu hata kama niki lala au kuisubiria tu itakuwa au itakuja tu sio kitu chepesi kama utakavyo fikiria.

Uwa ahadi ya Mungu inapoachiliwa ndivyo vita vinainuka kuizima hiyo ahadi isi dhihirike katika mwili au isitimie.

Hata yesu alipotaka kuzaliwa na hata alipozaliwa vita dhidi yake ikaibuka………..hata malaika akamtokea yusufu na kumwambia aondoke!

Luka 2:9 Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.
          10 Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;
          11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.
Kwa hivyo ni muhimu kutambua kuwa kitu kipya kinapotaka kuzaliwa hapa anga linatambua na hata kuweka kizuizi dhidi ya hicho kitu.

Mathayo 2:13 Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.

Hali ya kutambua kuwa Mungu hana kawaida ya kukosea, hali hiyo lazima idumu katika maisha yako mpaka ahadi hiyo itimie, uwa Mungu anaposema anakuwa ameshamaliza ahitaji nyongeza tena zaidi ya kuona imetimia.

Ni muhimu kutambua ni kweli Mungu hakosei ( maana ajawai kukosea ) ila wewe unaweza ukakosea ukasababisha ukose ahadi ambayo Mungu aliiandaa kwa ajili yako.

Ahadi ya Mungu hipo na inapotoka uwa imetoka inategemea mazingira yake ili kutendeka zaidi ya asili ya neno lenyewe lisiloshindwa, lenyewe liko zaidi ya mazingira yote na linajitosheleza alihitaji usaidizi wowote, maana neno la Mungu ndio asili ya vyote hata vile unavyo viogopa vinaweza kumezwa hama kusimamishwa na neno.

Na ni muhimu akili yako ijue kwamba kabla ya wewe ujazaliwa naam hata dunia kabla haijaumbwa mpaka leo Mungu ajawai kukosea japo wakati mwingine kutokana na akili zetu zilizo na mipaka unaweza kuhisi hama kuwaza kwamba Mungu anakosea kutokana na muono wako lakini sio sahihi, kwakuwa hiyo ni akili yetu sio akili yake.

Na ukumbukwe hakuna mtu/kitu kinachoweza kumrekebisha Mungu maana vyote vilifanywa naye zaidi sana Mungu kuachilia siri yake katika akili zetu mathalani ukuaji wa vitu: mimea, wanyama na viumbe vingine lakini sio kuviboresha zaidi ya kujifunza kwanini iko hivyo/ inakuwa hivi.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………….0764 018535


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni