Ijumaa, 12 Juni 2020

MUNGU KATIKA ULIMWENGU WANGU;




Japo duniani tuko watu wengi tunaoishi lakini kila mtu ana himaya yake ( ulimwengu ),
Ulimwengu wa mtu ni mahala ambapo:

(a)   Ni hali ya mtu kujiona mwenyewe kwa uhalisia wake.

(b)   Ni mahali ambapo mtu ujielewa na kujisikia fahari

(c)    Ni mahali palipo ubeba usiri wake.

(d)   Ni hali iliyojificha ndani ya mtu inayomfanya/iliyomfanya kuwa vile.
-          Umasikini
-          Utajiri
-          Ugonjwa
-          Afya njema

Ni ulimwengu ambao ni mtu binafsi ndio mwenye dhamana/maamuzi wa kuifunua watu wengine waijue au waione.

Ni hatari sana kuwa na mtu unayeishi naye na asiruhusu uingie katika ulimwengu wake hapo kuambatana itakuwa ngumu, unaweza kukuta mtu anacheka lakini amaanishi kucheka!

Maisha ya wakristo yanaweza kuwa ni magumu sana endapo utakubali kuishi na Mungu uku ukificha mambo yako katika ulimwengu wako, Na kutoruhusu Mungu aingilie na kufanya marekebisho ili ulimwengu wako uwe na faida kwake.

Ni muhimu utambue ulimwengu wako ( mahala pa siri ) panaweza kukupa ushindi hama kukupa kushindwa.

Pindi utakapo ruhusu utawala wa Mungu mkamilifu katika ulimwengu wako hauwezi kuwa na sura tofauti tofauti ( uku uonekane mwema na kule uonekane mbaya ) lugha rahisi unafiki utakuwa ni historia.

Usipo ruhusu ukarabati wa Mungu katika ulimwengu wako ni rahisi kuanza kuwaona watu ni wachawi au hawapendi maendeleo yako lakini utakapo ruhusu ukarabati wake hapo ndipo utaanza kuwaona watu kama Mungu anavyowaona.

Ni jambo lisilo pingika pindi utakapoamua kuwa na ulimwengu uliosalama basi na wewe utakuwa salama sio rahisi kuwa tofauti na ulimwengu wako ulivyo, 

Mambo mengi yanaweza kukutokea yanaweza kuwa mabaya au mazuri hautaji kuipa shida akili yako bali tambua ulimwengu wako ndio matokeo yake.

Wewe unakuwa chimbuko la ulimwengu wako, vile ulivyo unategemea ubora au uimara wa ulimwengu wako. ( maana huo ndio msingi wa wewe kuwa vile ulivyo ).

Hauhitaji kupambana sana ili ushinde bali unahitaji kuwa na ulimwengu uliosalama, imara na wenye nguvu basi hapo ushindi utapatika tu.

Usijivunie mambo yanayoendelea nje ya ulimwengu wake yanayoonekana kuwa ni mazuri bali kama ulimwengu wako hauko vizuri jua huo uzuri utaharibika tu muda si mrefu.

Kama mti unavyotegemea mizizi katika maisha yake ndivyo binadamu utegemea namna ulimwengu wake ulivyo katika ustawi wake!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………..0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni