“ ukombozi wa nafsi ndio uhuru wa roho “
Nafsi ya mwanadamu inaweza kuwa katika hali mbili tofauti
inaweza kuwa huru au utumwani na hali hizi utokana na kile kilichobebwa ndani
ya nafsi.
Nafsi inapobeba mambo mengi yenye huzuni na mateso basi
machozi ndio fungu lake.
Bora mtu afungwe jela miaka mia kuliko kuishi ndani ya
kifungo cha nafsi.
Japo wako watu waliofungwa nafsi na hata kukosa dira nzuri ya
maisha yake lakini akakuta ameyazoelea hayo maisha pasipo kujua yuko shimoni na
anatakiwa kutoka na mbaya akili yake iliyotiwa giza akaona hayo ndio maisha
aliyokusudiwa kuishi hii ni zaidi ya hatari.
Na pia nafsi inapokuwa kifungoni uwa magonjwa yanaweza kuwa
fungu lako!
Nafsi ni nini?
-Ni hali kamili iliyondani ya mwili wa binadamu inayo
mwezesha mtu kujitambua!
Hivyo huwezi kuigusa kama unavyogusa mwili wa binadamu japo
hiyo nafsi ina umuhimu mkubwa kuliko mwili wa mtu husika.
Nafsi ni rahisi kugandamana na jambo linaloendelea katika
maisha ya mtu husika linaweza kubeba kisirani/mauzi na mateso katika utendaji
wa mtu husika.
Nafsi ni kama mtu asiyevaa nguo na pindi anapovaa nguo kama
ni safi na size ikaendana na umbo lake basi bila shaka itatoa muoneka unaovutia
kama si kupendeza sana na hapo huo muonekana ukaathiri katika maisha yake na
hata kupelekea kuyafurahia maisha yake.
Lakini pindi nafsi ikiwa imevaa nguo chafu basi hapo
uwezekano wa kujichukia ni mkubwa na kila tendo atakalofanyiwa liwe zuri au
baya linaweza kuondoa thamani yako katika jamii, hali hiyo uwa fungu lake.
Na ni ukweli usiopingika uwezi kuwa na muonekano tofauti na
nafsi yako ilivyo mathalani mtu aliyejeruhiwa katika nafsi yake ni wazi sura
yake itaonyesha basi kama nafsi yako ilivyo ndivyo utakavyoonekana katika jamii
husika.
Nafsi yako ikivaa ukatiri na ukaanza kutoa udhihirisho wake
katika matendo basi hapo jamii itapata sura au namna ilivyo nafsi kupitia
matendo ya ukatiri yanayotoka ndani yako.
Na ili nje uweze kupata badiliko la kweli hilo badiliko ni muhimu ni lazima lianzie ndani
ya nafsi yako ndo maana kuna uwezekano usio na mashaka ndani yake kama nafsi
yako ikipona basi hapo kuyafurahia maisha ni swala lisilopingika.
Ukatiri wa simba haupo kwenye muonekano wan je bali upo ndani
yake uliambata na asili yake na uwezi kuubadilisha kwa kukata manyoya yake.
Ni muhimu ujue unahitaji kuwa na nafsi iliyo na utoshelevu wa
Mungu yaani kama vile kama anavyotaka au alivyoikusudia na sio kitu kingine
mathalani kama jamii ilivyokutengeneza katika uharibifu wake au wewe mwenyewe
ulivyoitengeneza tofauti na mpango wa Mungu.
Ni hatari sana kukutana mtu aliyejeruhiwa nafsi alafu hiyo
nafsi ikashindwa kutawaliwa na akili yake kwa kuwa tendo atakalolifanya
linaweza tikisa jamii nzima na kutoamini binadamu gani huyu aliyefanya tukio
hili utoshangaa mtu huyo akila nyama ya mtu mchana kweupe bila uwoga!
Kufurahia maisha yako inategemea hali njema ya nafsi yako!
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………..0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni