“ Namna yake” ni hali inayoonyesha vile alivyo au namna anavyoendesha mambo yake!
Na imekuwa ni msemo wa kawaida katika ulimwengu wa sasa katika mambo mengi;
i) Ili upate kile kitu basi wewe enenda kwa namna hii alafu muda si mrefu itakuwa ya kwako.
ii) Ukitaka “ kuwin ili game” ni lazima uende kwa namna hii nje ya hapo “ utafail- utashindwa”
iii) Ukitaka kumpata huyu binti au kijana wewe fanya hivi tu alafu atakuwa wa kwako.
iv) Ukitaka kuipata ile “tenda” wewe fanya hivi au andika “ proposal” iliyo ya namna hii basi utaipa.
Mwisho wa siku tunatambua kila jambo lina namna yake ili uweze kulipata/kufanikiwa sio kwenda vyovyote tu ukutegemea kupata kila kitu.
Ni kweli unaweza kukosa vingi kwasababu ujui jinsi/namna yake ili uvipate hama unaweza kujikuta unakosea kila siku kwasababu ujui jinsi/namna ya kukifanya kiufasaha.
Hii hali ya namna ya kufanya kitu imeleta shida sana katika jamii tuliyonayo; mathalani unaweza kukuta kila mtu ana namna yake ambayo yeye binafsi anataka asalimiwe au atendewe, utoshangaa kusikia watu wakisema huyu mtu ili aitike salamu yako amekutathmini kwanza kwa muda wa kutosha mbali na hilo, pia katika salamu wako watu wanapenda uwakumbatie pindi unapowasalimia hapo ndipo wataona umewasalimia na kuna wengine ukiwapungia mkono kama ishara ya kuwasalimia wanaona sawa tu hawana shida bali wengine wanaweza ona kuwa umewadharau…….mbali hayo pia yako mambo mengine namna tofauti tofauti ya kuongea na watu kutokana na hadhi ( status ) yao, rika lao pia kwa namna mbalimbali hata katika upande wa mapishi inaweza kuwa wote mnapika mchele lakini namna ya kupika mkatofautiana kutokana na sababu mbalimbali inaweza kuwa kutokana na ushauri wa daktari kuna vitu vitaongezwa au kupunguzwa kwa mgonjwa, hama kutokana na mapenzi ya mtu husika anapenda apike kwa namna ipi?
Kuna namna ya vitu/mtu kuvifanya vilivyo asili kwakuwa ni lazima vipitie katika hali hiyo ili viweze kuwa katika hali yake ( vitu vilivyo asili vinaenenda kwa asili ) lakini kwa jambo ambalo si sawa katika mwenendo au baadhi ya watu unaweza kukuta mtu amejiwekea namna yake katika kuendesha mambo yake utafikiri hiyo namna walikaa na Mungu wakakubaliana, ila hiyo ni namna ya ubinafsi iliyo tawaliwa na matakwa ya mtu husika lakini watu wa namna hii upenda kutembea kwa namna hiyo akiitafsiri kuwa hiyo ndio namna yake.
Bila shaka unaweza kukuta namna hiyo inabadilika ghafla pindi moyo utakapo pata mwelekeo mwingine pia kuishi kwa namna yako ni kitu kizuri lakini kuwa mwangalifu isije ikawa kero kwa watu wengine.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni