1 petro 1: 11……..Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na
Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso
yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.
Uwa
tunaifurahi leo kwasababu tumeipita jana na tunaitumaini kesho kwakuwa tunaishi
leo,
Mathayo 17: ( 24-27 )…… 24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya,
atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba
ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na
mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba
ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.
Tuna tambua katika machafuko hapo uimara wa mtu uonekana, na ni
katika msingi ulioshikiliwa na neno lazima uwe salama katika dhoruba yoyote.
Moja
ya kitu kinachopiganiwa sana na watu ni kuwa na heshima “ kuheshimika” maana
itazidi kumjengea nafasi katika jamii aliyekuwepo.
Japo
ni mtego mkubwa kwakuwa watu wengi wako tayari kupata heshima lakini awako
tayari kudhihakiwa pasipo kujua wakati mwingine dhihaka uweza kukupeleka kwenye
heshima. Ndomana wengine uweza kusema baada ya taabu/dhiki faraja!
Inakuwa
sawa na mtu anataka kuvuna pasipo kujigharimu katika kupanda!
Imekuwa
ni rahisi mtu kuikabili dhiki/changamoto baada ya kuona kuna neema mbele yake
lakini sio kitu rahisi kuikabili dhiki/changamoto kama hataona neema
itakayozaliwa baada ya hapo.
Unapoamua
kuishi na Mungu hayo majira uwezi kuyakwepa kwakuwa yapo ili kuhakikisha
heshima yako inadumu na sio kushuka ni sawa mjenzi wa ghorofa lazima haende
chini sana ili apate uwezo wa kwenda juu sana.
Kila
mtu upenda heshima lakini ni muhimu kutambua heshima inatengenezwa unaweza jua
au kutojua lakini ukitembea kwenye kanuni basi matunda yake yatadhihirika tu.
Unapotambua
baada ya dhiki kuna heshima haupaswi kuishi maisha ya unyonge au ya ukiwa bali
ni kipindi cha kuimarisha roho+akili+mwili wako tayari kuingia katika hatua
nyingine ya maisha yako iliyobeba heshima yako.
Kipindi
cha dhihaka kinakuwa kigumu sana kwa mtu asiyejua namna gani ya kuishi katika
kipindi hicho, unaweza kukuta mtu katika kipindi hiki amejawa na lawama, huzuni
na teso lisilokoma, na hali hii inaweza pelekea kushindwa kuifikia heshima yake.
Unapaswa
kujua heshima inakuja, katika kujibu maswali yaliyo jikita katika fahamu zako
na hata kuondoa pumziko la roho yako na sio kuwa kikwazo kwa wenzako.
Na
heshima ya kudumu haiji tu kwasababu imetokea tu bali kwasababu unastahili,
hivyo ni lazima ustahili kwanza ili heshima iweze kuja kwakuwa kila jambo
linatokea katika mazingira yake na kama si mazingira yake ni vigumu kutokea.
Ni
muhimu kuzingatia katika dhiki uko na nani ili heshima ije!
“ Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako
vyanifariji. ” zaburi 23:4
Usije
ukaishi maisha ya kufuata mwili ukategemea heshima ya Mungu
ikuambate/kukufunika kwa kuwa heshima yake haichanganywi .
Unapopita
katika dhiki pamoja na Mungu basi hapo tegemea heshima ya Mungu kukuinua.
INAITWA
SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa
na:
Cothey Nelson……………………….0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni