Ijumaa, 27 Machi 2020

LA MSINGI!




Tunasema ni siku nyingine kwakuwa kulikuwa na siku kabla ya leo………………….!

Karibu…………….!

Unaweza kukaa na mtu kwa muda mwingi ukicheka naye na hata kutaniana naye na hata ikiwezekana kula pamoja naye, ukawa mvumilivu kwa huyo mtu na hata ukaacha baadhi ya shughuli zako kwa ajili ya kutoa umakini wako wote ukitaka kujua ujio wa huyo mtu ulikuwa na lengo gani hasa?

Kwa kiasi kikubwa ujio wa mtu kwako unaweza kuubashiri katika muonekano wa sura pamoja na tone ya sauti yake ( huzuni au furaha ) uweza kubashiri kitu na kuanza kuandaa moyo wako kupokea kitu kitakachosemwa na mtu husika.

Na inakuwa mchanganyo kidogo kama sio sana pindi utakapo bashiri kitu ambacho mtu atasema na wewe lakini ikiwa tofauti kabisa na kile anachosema, mathalani unaweza ukawa na changamoto ya kifedha ghafla mgeni akakutembelea na kwa muonekano wa kawaida ukajua kuwa huyu mtu yuko vema nawe ukafikiri hapa ndipo mahali pa kuponea ili siku hiyo isipite bure lakini ukashangaa mtu huyo anakwambia “ biashara zangu zimekwama kidogo ningepata kiasi fulani cha fedha kingenisaidia katika kipindi hiki “

Bila shaka ukiwa na moyo mdogo unaweza kujikuta kimoyomoyo unaomba aondoke tu maana hana faida kwako kwa wakati huo na ikitokea anaendelea na mazungumzo mengine unaweza kujibambikizia shughuli ya kufanya hapohapo tu ili mradi tu aondoke au ukaunda safari ya ghafla ili mradi uepukane naye.

Ni jambo la kawaida tu unapomuhitaji mtu kuongea naye ukweli vinywaji na chakula vinaweza visiwe vya msingi kwake bali kile kiini/lengo kuu la kikao hicho ndicho kitakuwa cha maana kwake.
Hutakosa kusikia mtu katika hali ya kujuta baada ya kutopendezewa na jambo la msingi lililoendelea katika mazungumzo hayo……………..hizi ni baadhi ya kauli zake:

“ mi nilifikiri ameniitia jambo la maaaaana sana kumbe hakuna kitu “

“ tangia siku hile ya kile kikao na alichoniambia thamani yake nimeishusha kabisa kwangu mimi nilifikiri ataniambia jambo la msingi kumbe ujinga mtupu “

NOTE: Ni jambo la msingi wakati mwingine mkanganyo mkubwa utokea katika jambo husika lakini linaweza lisiwe la msingi kwa sasa lakini likawa la msingi katika hatua inayofuata katika maisha yako.

Karibu katika somo……………………………………………!!!

Katika jambo lolote linalo muhusisha Mungu jua katika utendaji mzima wa hilo jambo linamuhitaji Mungu kuliko kitu chochote, na ni muhimu zaidi kuliko oxgen katika maisha ya mwanadamu maana ukikosa oxgen unaweza kufa kimwili ila ukimkosa Mungu utaangamia roho na mwili pia.

Na hata katika mambo ya kushirikiana katika shughuli za kibiashara la muhimu nguvu ya uchumi na wazo lililobora ulilokuwa nalo.

Ni kweli kabisa katika kufanikisha mambo mengi, watu na mtaji ni muhimu lakini sio muhimu kuliko Mungu, kwakuwa vyote vya tokana na Mungu.

Na ni muhimu kujua ili ufanikishe mambo ya kimungu katika hali yoyote ni muhimu sauti ya Mungu iwe nguvu katika moyo wako kuliko jambo lolote, sauti zisizo ambatana kweli ya Mungu zisiwe na nguvu kwako kwakuwa watu uliwakuta na utawaacha lakini Mungu ulikuwa naye kabla ujatokea katika ulimwengu wa nyama na hata hitimisho lako limebebwa na yeye.

Sizungumzii kuwa watu sio wa muhimu la hasha! Bali hekima inahitajika katika utendaji maana hakuna aliyezaidi ya mwingine wala aliye chini ya mwingine! Ila katika yote Mungu anabaki kuwa Mungu.

Ukimfanya Mungu kama kiongozi wako na ikiwa jambo LA MSINGI katika maisha yako hauwezi kupoteza na kufika kwenye hatima yako ni jambo lisilopingika.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………..................…………0764 018535

Ijumaa, 6 Machi 2020

JICHO LA MUNGU




Moja ya kitu kinachoweza kufanya uyafurahie mazingira kwa kusema ni mazuri ni baada ya kuona “ kazi ya jicho “ 

Natukumbuke kuwa kuna kuona kwa aina mbili, kuna kuona kwa macho pia kuna kuona kwa akili mathalani unaweza pewa hesabu iliyofungwa fungwa sana na ukiangalia kwa haraka unaweza ukakosa jibu lakini pindi akili yako ikapata utatuzi wake basi hapo wewe utakuwa unaangalie jibu tu maana ugumu umeshapotea.

Utofauti mkubwa wa jicho la Mungu na la mwanadamu, jicho la mwanadamu uangalia kilichopo na uweza kubashiri kile kinachoweza kutokea lakini sio jicho la Mungu lenyewe uona mwisho wa jambo ulio na uhakika na sio kubashiri au kubahatisha.

Kwa mtu unayetaka kutembea na Mungu hama kuona mkono wa Mungu, basi unahaja ya kuhakikisha jicho lako linaona kama la Mungu, nje ya hapo itakuwa ni vigumu tu kwasababu mtakuwa hamja ambatana.
Unapotaka kuifurahia dunia kama wanadamu  wanavyoifurahia basi tembea katika jicho la kibinadam lakini pindi utakapotaka kuifurahia dunia kama vile ulivyokusudiwa basi hakikisha jicho la Mungu lina nafasi ndani yako.

Hata unapokuwa katika hali ngumu kiasi gani katika uchumi, ugonjwa au mahusiano lakini utakapotembea katika jicho la Mungu ni lazima uone kesho yenye faida iliyo jaa utatuzi wa shida ya leo.

Kuna baadhi ya mambo yanayoweza kukuta ghafla ukajiona thamani yako haipo lakini pindi utakapo jiona katika mtazamo au jicho la Mungu thamani yako itarejea kwa kasi ya ajabu.

Unahitaji kujiona katika jicho la Mungu ili uweze kulitumikia kusudi la Mungu vizuri lililoko ndani yako, maana katika utumishi kuna misukosuko mingi nje ya jicho la Mungu unaweza kupoteza mwelekeo sahihi.

Maisha ya Mungu yanazaliwa ndani yako pale utakapoishi katika mwelekeo wa jicho la Mungu.
Unapoyatazama mambo kwa jicho la Mungu ni vigumu sana upate kushikwa  mikono na watu hasa wanaona kwa jicho la wanadamu.

Unapoyatazama mambo kwa jicho la Mungu hata waliokaribu nawe na kutegemea watakuunga mkono watakuona umepotea.

( Nuhu-safina )!
Mwanzo 6: 13 Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.
                    14 Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami.
                22 Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.

Hatua ya awali ya kuanza kuona kama Mungu ni kuanza kujifunza kuisikia sauti ya Mungu na kukubaliana nayo kwa umakini wote kuliko chochote.

Uwa hatuoni kama Mungu anavyoona kwa kuzaliwa bali kuna hatua mpaka kufika hapo ndomana mtu azaliwi tu akawa chuo kikuu lazima kuna hatu za awali ambazo ni muhimu sana katika kukupeleka uko juu!

INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey  Nelson………………………………………………. 0764 018535