Alhamisi, 20 Mei 2021

UTUMWA WA AKILI.

 


 Neno “ utumwa “ ni neno lisilovutia kulisikia masikioni mwa mtu, kutokana na uhalisia ulivyo wa mtu anayeishi maisha ya utumwa, kwa asilimia kubwa unaishi maisha usiyoyapenda kwahiyo furaha ya kweli inakuwa adimu katika maisha hayo! Kwa kifupi unalazimika kuishi hivyo sawa na matakwa ya mtu mwingine.

Hivyo tunakubaliana kabisa moja ya teso la utumwa ni kutoishi maisha yake au kuishi vile upendeleavyo bali unaishi kwa matakwa ya mwingine tena bila ridhaa yako.

Ni maisha yaliyobeba hali ya ukatiri na kutojaliwa! Unaishi kwa sababu unapumua na wala si kwa sababu unafurahia maisha.

Pindi unapokuta mtu anaishi maisha haya ( utumwa ) kuwaza kujiua ni kitu kinawezekana tu na utoshangaa kumkuta mtu kajiua, kwa maana utumwa wa akili unaweza kufanana na mtu aliye zezeta kwa maana kwa kiasi kikubwa mtu uishi nje ya utashi wake.

Hapa duniani kuna utumwa wa aina nyingi mathalani kuna utumwa wa pesa,ngono,kazi,akili na mengine mengi.

Lakini ningependa kuangalia UTUMWA WA AKILI,

Hii ni hali ya mtu kushindwa kuitawala akili yake na kujikuta kufanya mambo ambayo kwa uhalisia ayapendi.

Ni maisha ambayo mtu anaishi baada akili yake kukosa jibu liletalo amani litakalo ondoa shida hiyo inayomkabili, utakuta mtu anakubali kufanya jambo moyo,akili na hisia azitaki lakini imemlazimu maana hana namna nyingine.

Akili yako inaweza kushikiliwa na mtu mwengine kutokana na ridhaa yako au nje ya ridhaa yako ikakupelekea kufanya mambo kwasababu tu imekulazimu mbali na hapo maisha yako yatakuwa vinginevyo.

Utumwa wa akili ni mambo yote ambayo akili yako yanakusukuma kutenda nje na utashi wako ili mradi tu maisha yako yawe salama au yaendelee.

Ni vile akili yako imeshikiliwa na vitu vingi vinavyofanya akili yako isiwe na maamuzi yake.

Mbali na hapo kuna utumwa wa akili unaoupenda ( hata pasipo kujua kuwa huu ni utumwa ) ambao unaweza ona uko sawa tu kwa namna ulivyo kwakuwa hauna madhara ya moja kwa moja katika maisha yako ya sasa mathalani akili yako inakupa msukumo wa kupenda kula vitu vyenye mafuta na sukari nyingi pasipo kuwa na tabia ya kunywa maji ya kutosha wala kufanya mazoezi  madhara yake utayaona baadae! Hata utumiaji wa madawa ya kulevya unaweza mdogo mdogo lakini baadae ukishakolea hautasita kuuza hata nyumba ili uendelee kutumia madawa ya kulevya.

Na kwa utumwa usioupenda unaweza kujikuta wewe unagombanisha watu kila inapoitwa leo la huyu unalipeleka kwa yule na yule unalipeleka kwa wale ili mradi tu wasielewane.

Kiujumla utumwa wa akili hauna matokeo mazuri katika maisha yako haijalishi unaupenda au haupendi mambo yote unayo yafanya ayatatoa mwelekeo sahihi /bora katika maisha yako.

Njia za kukuwezesha kuondokana na utumwa wa akili;

i)                    Ongeza maarifa juu ya kitu kinachokutatiza katika akili yako ( hali ya kutafuta ufumbuzi ) na kushindwa kupata mwelekeo na unaweza kuongeza maarifa kutokana na kujisomea vitabu au matumizi sahihi ya mitandao na hata katika watu unaowaamini wanaoweza kukushauri na hatimaye kutoka katika hilo tatizo au hiyo hali.

ii)                  Anza kufanya tofauti na akili yako ilivyo kamatwa, kama unajua akili yako imejaa uchonganishi basi anza kujenga tabia ya kusema vizuri kwa waliokuuzi na wasiokuuzi.

iii)                Mshirikishe Mungu katika hali inayokusumbua akili yako! Yeye aweza kubadilisha na kufanya tena yale yote yaliyoshindikana kwa wanadamu,

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………..0764 018535

 

Ijumaa, 7 Mei 2021

UTULIVU WENYE KISHINDO



 

Katika hali ya kawaida uwa mtu atulii tu! pasipo sababu inayomfanya atulie, inawezekana kuwa ni sababu iliyoanzia ndani yake iliyojaa na ubinafsi wake au yaliyosabishwa na mambo yaliyo nje yake.

Utulivu unaendana sana na subira au moyo wa kungojea kitu kwa matumaini makubwa!

“ kimya kina kishindo”

Na kuna utulivu kwa maana ya kupata pumziko la akili, ili ikusaidie kurudi katika ubora wa utendaji wako! Pia kuna utulivu wa lengo la kujiandaa na jambo na hatima kuushangaza ulimwengu yaani unafanya jambo au tukio ambalo masikio yakisikia yatawashwa na hata macho hayata amini kile kinachoonekana.

Mathalani, shambulio la magaidi dhidi ya marekani ( September eleven ) ni shambulio lililoweza kubomoa balozi za marekani zilizopo Kenya na Tanzania kwa wakati mmoja, hii mikakati ya shambulio hili lilikuwa la siri sana na kuchukua muda mrefu katika maandalizi yake hata kama mchunguzi wa mambo haya ungeweza kusema shambulio alipo au wameaghirisha.

Uwa ardhi inapoachwa kwa muda baada ya kupoteza rutuba yake au kuachwa kwa muda kwa sababu zingine lakini pindi muda utakapofika shughuli zinaweza kuanza tena au kuendelea kwa kishindo kisichokuwa cha kawaida au kupatikana kwa mavuno yakutosha japo wakati mwingine unapoona ardhi imeachwa unaweza kuhisi kuwa imetelekezwa lakini sivyo!

Unaweza kukuta mtu yuko kimya kama hayupo vile katika shughuli fulani isifanye ukafikiri kuwa ameshindwa, kumbe anatunza fedha au anarejesha nguvu zake ili aweze kufanya jambo kwa kishindo kingine cha ajabu.

Kwahiyo unapokaa na mtu usitishwe au usipotezee utulivu wake, endapo kama hautajua yapi yanaendelea katika utulivu wake maana kwa kujua hapo panaweza kufanya ujiamini au ukimbie.

“ ukiona kobe kainama ujue anatunga sheria “

Hivyo utulivu au ukimya wa mtu sio ukupe matumaini kwamba ameshindwa, kwani unaweza kujikuta uko katika mazingira magumu kwa kutokujua kinachoendelea katika utulivu wake.

Utulivu wenye kishindo haya ni maisha mazuri sana yanayokupa nafasi ambayo wengine awawezi kudhani kuwa utatokea hapo au kuwa mshindi.

“ yesu alipokuwa anaelekea kwenye kifo, kambi ya adui ilishangilia sana na kuamini imeshinda ule ukimya na upole wake pamoja na unyenyekevu wake alishajua ameshamaliza kila kitu, lakini awakutambua maana ya neno la yesu alilolisema “ imekwisha “ ila walielewa baada ya yesu kuingia katika himaya yake ya utawala wa giza hapo alishindwa kuamini kilichomtokea.

Ingawa mambo mengi yanapokuzonga hapo unaweza kuwaza mengi na maamuzi mengi yanaweza kuja katika akili zako lakini ukiingia katika ulimwengu wa utulivu na Roho mtakatifu hapo unakuwa hatari zaidi ya hatari yenyewe.

Usipende watu wakuelewe mapema subiri matokeo yatawaelewesha vizuri kuwa wewe ni nani?

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………………………………………….0764 018535