Ijumaa, 23 Julai 2021

INASHAWISHI


Ni kawaida tu, kuwa kitu kinachoshawishi lazima kiwavute wengi kwake! kwa kuwa kinasifa ya kuvutia, “ PESA “ wengine wanasema ni jibu la maisha au heshima ya mtaa!

Tukiachana na PESA kwanza!

Neno USHAWISHI limekuwa ni msingi mkubwa katika dunia ya leo.

Kila bidhaa ni lazima iwe na ushawishi ili iweze kumvutia mhitaji ( mteja ).

Mtu anaweza kuwa na bidhaa nzuri sana lakini bado akafanya vitu vingi ili watu washawishike! Na watu wanafanya hivyo, ili kujaribu kuleta mvuto unaombatana na uelewa kwa watu pengine watampendezwa na kutokea kukipenda hatimaye kukinunua/kukichukia.

Na ni wazi ushawishi wowote usio na matokeo mazuri basi hali hiyo ya ushawishi uweza kukoma kabisa kama sio kupungua.

Ni kweli mahali popote penye ushawishi watu wengi ukimbilia hapo, japo hapo ukweli wakati mwingine ubora unaweza usiwepo.

Kwa kiasi kikubwa dunia ya sasa vitu vingi vinabebwa na ushawishi mathalani ili mtu akupende ni lazima umshawishi au aone sababu ya kukupenda hama atakapo kupenda nini atafaidika au kitaongezeka.

Na hii dhana imeingia hata upande wa ajira imepelekea ili mtu akupe kazi yake au akuajiri lazima umshawishi kuwa unaweza hiyo kazi na uko tayari kufanya hiyo kazi.

Na hata katika uwanja wa kukopa imekuwa ngumu ili mtu akukopeshe tu, ili mtu akukopeshe ni lazima umshawishi ili aone sababu ya kutoa pesa yake yaani umuhimu wa hitaji ulionalo, pia uhakika wa kurudi fedha yake pamoja riba yake.

Ushawishi umekuwa ni msingi wa mambo mengi kwenda pasipo kujali huko yanapokupeleka kuna usalama au la!

Wako watu walio hatarisha afya zao na hata maisha yao ili kutaka kumshawishi mtu akubali kufanya jambo fulani lenye maslahi kwake mathalani wako watu walikubali kufanya ngono na mabosi wao ili kupata ajira hama kupata nafasi za juu.

Ni kweli usiopingika ushawishi unaweza kuzaliwa katika muonekano wa nje au nguvu inayozaliwa ndani yako.

Ni muhimu utambue ushawishi ulioambatana na muonekano uwa unakuwa na mwisho lakini ushawishi unaotoka ndani yako uwa hauna kikomo ni kama bahari isivyo kuwa na mwanzo wala mwisho.

Kila ushawishi unaambatana/unaendana na matokeo pamoja na majira, pia ukijiona umefika ujue wapo waliofika kabla yako.

Kuwa na muonekano unaovutia ni kitu kizuri sana lakini kitu pekee kitachoweza wavutia watu na Mungu pia ni pale utakapo jali UTU WA MTU.

Muonekano wako usikupumbaze kuona watu vile watu wanakusifia ukafikiri mbinguni wanakupigia makofi namna ulivyovaa au namna unavyotabasamu.

Tambua Mungu ndiye ametia hiyo akili katika kichwa ( ubunifu ) ila akumaanisha ukishajiona umetokeleza duniani basi ujione umetokelezea hadi mbinguni.

Katika yote lazima utambue wewe ni asili ya Mungu na Mungu kwa thamani mtu aliutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

“ unapokunywa chai ya maziwa usione wajinga wanaokunywa chai ya rangi”

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………….0764 018535

 

Ijumaa, 2 Julai 2021

ILI AWE MTOAJI NI LAZIMA MSIKILIZE

 



Ni kanuni ya maisha ya kila siku……ili usikilizwe ni lazima ujifunze kusiliza wengine!

Na moja ya ushawishi wa mtu kuendelea kutoa kwako pasipo kuchoka na kila siku ajisikie mdeni ni pale atakapogundua kuwa unamsikiliza!

Na hali ya kusikilizwa sio kivutio cha watu wengine tu bali hata kwa Mungu ni kichochezi kikubwa cha kufanya achilie hazina yake kwako!

Kutoka 19:5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,

Kusikilizwa ni shauku ya Mungu kwa watu wake!

Hivyo tunakubaliana kuwa ni muhimu kutambua ili uweze kusikilizwa ni lazima usikilize, wakati mwingine hali hile unayoitoa katika kusikia ndiyo utakayo sikilizwa.

Kama ilivyo kwa wazazi ili uweze kupata vitu vingi kutoka kwao mbali ya kuwa ni wazazi wako ni lazima uhakikishe mioyo yao imefunguka kwako na sio kitu kingine ni hali ya umakini ulionao kwao katika kutekeleza kile wanachosema.

Ni muhimu sana uwe mwangalifu wa kile unachokisikia kwakuwa kile unachokisikia ndicho kitakachokutunza au kukuharibu, usije ukawa unaisikiliza dunia uku ukitegemea mbingu ( Mungu ) ikutunze au itoe kwa ajili yako ni kitu kisichowezekana.

Uwezi ukamtumikia bwana john alafu ukategemea mshahara kwa bwana abdalah!

Kile unachokisikiliza kinaonyesha nafasi kilichonacho katika moyo wako ( maisha yako ) kwa hali hiyo ndiyo kinavyoweza kuwajibika kwa ajili yako na wala sio zaidi au chini bali ni kile kiwango utakachokisikiliza ndivyo kitawajibika kwako.

Mathalani mtu anapojua anasikilizwa ( kupendwa ) ni wazi atajiachia kwake anajua yuko salama! kwa kifupi kile kiwango anachojua anapendwa ndicho kiwango atakacho jiachia sio zaidi au chini.

Ukitaka Mungu awe mtoaji bila kumsikiliza bila shaka utakuwa unajidanganya ni sawa na kula upepo ukategemea utashiba.

Ni wazi ukitaka kuuteka moyo wa mzazi hauhitaji kupeleka sana maombi yako kwake au kwao bali wewe jikite katika umakini wa kumsikiliza bila shaka mahitaji yako yatatulika hata bila ya kuomba maana hata ukiomba kitu utakuwa umeongeza uharaka na kusababisha waache shughuli walizokuwa wanazozifanya ili kukamilisha hitaji lako.

Ndivyo ilivyo kwa Mungu hauhitaji kuomba sana ili akusikilize bali hakikisha unajigharimu katika kutekeleza sauti yake naye atausika nawe kwa maana ni yeye aliye ruhusu uje duniani hawezi kukuacha endapo tu utaendelea kumsikia.

Maana yeye anaijua kesho yako!

Mathayo 6:33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Anajua kwanini alikuleta duniani na anajua akupe nini uzidi kuyafurahia maisha yako hapa duniani maana ni sehemu aliyoiweka kwa ajili yako.

Tunapozungumzia kumsikiliza Mungu sio kama kusikiliza muziki au taarifa kwenye vyombo vya habari la asha! Bali tunazungumzia hali ya kujiweka ndani ya sauti yake na ukubali gharama zake.

Anapokwambia  “ TOA” ikibidi uwe tayari wewe na familia ulale njaa ili mtu mwingine ashibe.

Uwezi sema nimeisikia sauti ya Mungu nikafurahi na jasho likakutoka basi imeisha na ngoja kesho nisikie tena sauti yake au maelekezo yake.

Lazima ujue sauti ya Mungu inalengo la kukutoa katika hatua moja na kukupeleka katika kiwango kingine na sio kuchangamsha mwili tu.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………0764 018535