Ijumaa, 2 Julai 2021

ILI AWE MTOAJI NI LAZIMA MSIKILIZE

 



Ni kanuni ya maisha ya kila siku……ili usikilizwe ni lazima ujifunze kusiliza wengine!

Na moja ya ushawishi wa mtu kuendelea kutoa kwako pasipo kuchoka na kila siku ajisikie mdeni ni pale atakapogundua kuwa unamsikiliza!

Na hali ya kusikilizwa sio kivutio cha watu wengine tu bali hata kwa Mungu ni kichochezi kikubwa cha kufanya achilie hazina yake kwako!

Kutoka 19:5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,

Kusikilizwa ni shauku ya Mungu kwa watu wake!

Hivyo tunakubaliana kuwa ni muhimu kutambua ili uweze kusikilizwa ni lazima usikilize, wakati mwingine hali hile unayoitoa katika kusikia ndiyo utakayo sikilizwa.

Kama ilivyo kwa wazazi ili uweze kupata vitu vingi kutoka kwao mbali ya kuwa ni wazazi wako ni lazima uhakikishe mioyo yao imefunguka kwako na sio kitu kingine ni hali ya umakini ulionao kwao katika kutekeleza kile wanachosema.

Ni muhimu sana uwe mwangalifu wa kile unachokisikia kwakuwa kile unachokisikia ndicho kitakachokutunza au kukuharibu, usije ukawa unaisikiliza dunia uku ukitegemea mbingu ( Mungu ) ikutunze au itoe kwa ajili yako ni kitu kisichowezekana.

Uwezi ukamtumikia bwana john alafu ukategemea mshahara kwa bwana abdalah!

Kile unachokisikiliza kinaonyesha nafasi kilichonacho katika moyo wako ( maisha yako ) kwa hali hiyo ndiyo kinavyoweza kuwajibika kwa ajili yako na wala sio zaidi au chini bali ni kile kiwango utakachokisikiliza ndivyo kitawajibika kwako.

Mathalani mtu anapojua anasikilizwa ( kupendwa ) ni wazi atajiachia kwake anajua yuko salama! kwa kifupi kile kiwango anachojua anapendwa ndicho kiwango atakacho jiachia sio zaidi au chini.

Ukitaka Mungu awe mtoaji bila kumsikiliza bila shaka utakuwa unajidanganya ni sawa na kula upepo ukategemea utashiba.

Ni wazi ukitaka kuuteka moyo wa mzazi hauhitaji kupeleka sana maombi yako kwake au kwao bali wewe jikite katika umakini wa kumsikiliza bila shaka mahitaji yako yatatulika hata bila ya kuomba maana hata ukiomba kitu utakuwa umeongeza uharaka na kusababisha waache shughuli walizokuwa wanazozifanya ili kukamilisha hitaji lako.

Ndivyo ilivyo kwa Mungu hauhitaji kuomba sana ili akusikilize bali hakikisha unajigharimu katika kutekeleza sauti yake naye atausika nawe kwa maana ni yeye aliye ruhusu uje duniani hawezi kukuacha endapo tu utaendelea kumsikia.

Maana yeye anaijua kesho yako!

Mathayo 6:33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Anajua kwanini alikuleta duniani na anajua akupe nini uzidi kuyafurahia maisha yako hapa duniani maana ni sehemu aliyoiweka kwa ajili yako.

Tunapozungumzia kumsikiliza Mungu sio kama kusikiliza muziki au taarifa kwenye vyombo vya habari la asha! Bali tunazungumzia hali ya kujiweka ndani ya sauti yake na ukubali gharama zake.

Anapokwambia  “ TOA” ikibidi uwe tayari wewe na familia ulale njaa ili mtu mwingine ashibe.

Uwezi sema nimeisikia sauti ya Mungu nikafurahi na jasho likakutoka basi imeisha na ngoja kesho nisikie tena sauti yake au maelekezo yake.

Lazima ujue sauti ya Mungu inalengo la kukutoa katika hatua moja na kukupeleka katika kiwango kingine na sio kuchangamsha mwili tu.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………0764 018535

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni