Ijumaa, 17 Septemba 2021

MAJIRA

 


Katika dunia tuliyonayo kuna vitu ukicheka navyo, navyo vitakuchekea naam na kuna vitu ukivipoteza/ kuvipotezea unaweza usione deni la kupotea kwake pia vilevile kuna vitu ukiviimbia navyo vitacheza kama unavyotaka nawe utafurahi.

Napia katika maisha kuna wakati unaweza kuona haya ni majira ya kushinda kabisa lakini inaweza kutokea umeshindwa………ni kama wakati unataka kuweka tonge mdomoni basi hapo linachukuliwa! Vilevile kuna wakati unaweza kuona sasa umeshashindwa inabidi ukubali yaishe tu ili maisha yaendelee ghafla kwa namna usio dhani unajikuta una ona ushindi huo na hatimaye unatangazwa mshindi.

Naam kama kuna vitu vya kuogopa na kuvipa nafasi ya kutosha ili viweze kuchukua nafasi yake kwa maana havizuiliki ni MAJIRA  ni kama upepo unapokuja kwako kwa nguvu hauwezi kutumia mikono ili usikukuguse/kukufikia ndivyo  majira yalivyo, kwani hauwezi kujidanganya kukaa macho ili kuzuia usiku usiingia wala mchana usipite ni sawa na kuiamisha bahari kwa ndoo ukitegemea utafikia siku bahari itaamia upande unako mwaga maji kupitia ndoo yako nzuri.

“ maadam dunia idumupo MAJIRA ya kupanda na kuvuna havitakoma” iko hivyo tu jua liwake hama mvua inyeshe kila kitu kitakuwa kwenye majira yake.

Uwa majira yanakuwa na nguvu nyuma yake isiyoweza kuzuiliwa na kitu chochote ni zaidi ya maji useme utaweka ukingo naam ni zaidi ya upepo useme utapita tu pasipo kusikia kishindo chake nawe uendelee na mambo yako.

Majira yana nguvu za asili na pindi inapodhihirika kwa mtu au mahali hama wakati wake haijalishi uko wapi ni lazima kusudi lake litimie na kukuchukua kwenda hatua nyingine basi hapo lazima nafasi ikutafute ndipo hapo “kapuku” anakuwa “hitaji au jibu” la watu na hatimaye anafamyika baraka kwa wengi.

Na unaweza kuwa na rafiki yako mmeshibana sana lakini majira yanaweza kukutofautisha huyu akawa rais na wewe ukaendelea kwa raia mwema na wakati mwingine usishangae muuza maji ya kandoro akawa mmiliki wa kiwanda cha kuzalisha maji.

Pia unaweza ukawa na ndoto nyingi kubwa na nzuri sana lakini nje ya majira utalaumu watu na kuona upendo umeshuka au haupo kabisa.

Ni afadhali ucheze na umeme ukakamilisha historia au biashara ikaishia hapo lakini sio majira unaweza ukaishi katika ,maumivu makali pasipo kujua ni lini maumivu yatakoma.

Ni sawa na kiongozi anashiriki katika mazishi ya mtu aliyekuwa anamtegemea kila kitu “ mfadhili wake “ machozi yake yanakuwa ni sawa na kisima kisichokauka na pengine moyoni mwake anasema laiti ningetangulia mimi ili anizike kuliko kuipata aibu hii baada ya yeye kufariki.

Haupaswi kuogopa majira bali ishi ukijua kuna majira na yanapita sawa yalivyowekwa unapokuwa umeshiba jua kuna majira ya njaa yanakuja! Na unapokuwa na nguvu jua kuna majira yanakuja ambazo hauta kuwa na nguvu ulizo kuwa  awali.

Ni kama unapokuwa mtoto basi fanya mambo ya kitoto na unapokuwa kijana basi fanya yatakayo dhihirisha kuwa wewe ni kijana na pia unapokuwa mzee basi ufanye mambo yanayohusiana au yanayolingana na rika hilo na sio unapokuwa mzee ukatamani kufanya mambo ya kitoto au bibi akajitahidi kuwa kijana wa kisasa.

“ utajitahidi tu ila utakuwa kero kwa wengine”

Lazima utambue jana ikishapita imepita na mambo yake usilazimishe jana ifanane na leo hayo ni majira mengine yana mambo yake.

Ndomana mtu akiondoka uondoka na utambulisho wake pamoja na mambo yake hata mkijitahidi kumfananisha lakini huyo atakuwa kama yule, utajifariji lakini ukweli  na uhalisia wake utabaki kuwa wake.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………..0764 018535

 

Ijumaa, 3 Septemba 2021

MAJI YA MACHO


Unapozungumzia maji ya macho hapo nazungumzia maji yanayotirirka kutoka machoni yanayozungumza kwa lugha ambayo, kwa yule yanayomtoka uwa anaielewa!

Na maji haya yanaweza kutoka kwa mtu baada ya kufurahishwa au kuumizwa na kitu au hali fulani katika maisha yake.

Ni kama machozi ya samaki yasivyoweza kuonekana maana yanaishia majini, na uwa samaki maji ya macho yake yanatoka pale  aliyoyategemea na kutarajia kuwa tofauti na matarajio yake japo wewe unaweza usielewe ila yeye na walio katika ulimwengu wake wanaelewa vizuri.

Ni sawasawa na ndege au wanyama mathalani kuku au mamba na hata kondoo pamoja na mbuzi uwa wana lugha zao kuelezea hali zao kufurahishwa na kuhuzunishwa kwao, wako wanaotoa lugha ya machozi na wengine mingurumo na miemko katika muonekano wao.

Naam ni kama mtu aliyetegemea nguzo katika kujistili kama egemeo lake katika siku za maisha yake lakini pindi anapoona wageni mchwa wakiweka makazi ndani ya nguzo yake ya mbao aliyoipenda na kuitegemea basi hapo moyo wake uweza kuinama na kuruhusu maji adimu yatoke machoni.

Watu wengi ulia pindi wanapoona mchana unaondoka na usiku unakuja maana huo ni wakati ambao hataweza fanya yale anayoyataka maana ni giza tu litakuwa linatawala mboni ya jicho lake alitaweza kuimiri.

Kilio kikubwa katika familia ni pale anapoona anaumwa/wameondokewa na tegemeo au nguzo katika familia japo wote  ni sawa lakini kila mtu ana nafasi yake katika familia na hapo ndipo panapoonyesha umuhimu wake.

Mathalani mwanamke aliyefiwa na mume (mjane ) mbali na kumpenda sana lakini kama alikuwa tegemezi pekee katika familia hapo uweza kulia katika kiwango cha juu sana sawa na utamaduni wa kabira lake uku akijua kuwa ni kama ndege imepoteza mwelekeo angani na rubani ajui afanyi nini ili aokoe maisha ya watu ( abiria ).

Ndo maana hata nyumba ikipata itilafu yoyote kabla ya kukarabati wataalamu uwa wanaangalia namna ya nguzo zilivyoathirika je! Zinaweza kuimiri au zibadilishwe ili kufanya jengo kuwa imara.

NINAPO IANGALIA KESHO UWA MAJI YA MACHO YANATOKA!

Karibu!

Kuna vitu katika mwili wa mwanadamu vinafanyika kwa hiari yako au nje ya hiari yako,

Kuna vitu vingine mwilini unafanya kutegemea nguvu ya vionjo vyake, mathalani kuna baadhi ya maneno ukiambiwa tu unaweza jikuta umekaa chini hata bila kujua umekaaje hapo chini na inaweza kuwa ni habari ya kuuzunisha au kukufurahisha.

Tumekuwa tukijua kuwa nguvu inapotikisika hapo jengo kuanguka ni jambo linategemewa kutokea tu.

Moja ya kitu kinachoweza kumfanya mtu asitishe kufanya jambo ni pale anapoona kesho haiwezi kuwa ni sawa na picha iliyomo katika kichwa chake hama sawa na ndoto yake.

Na kuna mtu anafanya kitu uku akijua baada ya miaka kadhaa hata weza fanya tena na hana njia nyingine na hata kuwa njia nyingine hawezi  kuandaa kesho itakayo mpa kicheko uwa anafanya tu na jioni ikifika maji adimu machoni pake ndo yana kuwa usingizi wake.

Unaweza kukuta mtu anachukua maamuzi ya kujinyonga au akazidi kuwa chini pindi pale anapogundua kesho yake imejaa giza.

Ni muhimu utambue maadam kwakuwa ulikuwa na mwanzo basi una mwisho, hivyo unavyo ona giza katika jambo fulani jua hivyo ni ishara ya asili yako kwakuwa kutakuwa na mambo tu utakosa majibu hata kama unakitu gani maadam unaishi hapa duniani?

Maadam kuna mahali akili zako zilipata uelewa fulani jua mwisho wa uelewa hapo ndipo mpaka uweza wa akili yako kuona majibu katika maswali/ kuona dhahabu katika mawe mengi.

Unamuhitaji Mungu mwenyewe kuijua kesho kwakuwa kesho yeye anaijua anaimudu, ishi maisha uku ukijua unahita neema yake.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………….………0764 018535