Katika dunia tuliyonayo kuna vitu ukicheka navyo, navyo vitakuchekea naam na kuna vitu ukivipoteza/ kuvipotezea unaweza usione deni la kupotea kwake pia vilevile kuna vitu ukiviimbia navyo vitacheza kama unavyotaka nawe utafurahi.
Napia katika maisha kuna wakati unaweza kuona haya ni majira ya kushinda kabisa lakini inaweza kutokea umeshindwa………ni kama wakati unataka kuweka tonge mdomoni basi hapo linachukuliwa! Vilevile kuna wakati unaweza kuona sasa umeshashindwa inabidi ukubali yaishe tu ili maisha yaendelee ghafla kwa namna usio dhani unajikuta una ona ushindi huo na hatimaye unatangazwa mshindi.
Naam kama kuna vitu vya kuogopa na kuvipa nafasi ya kutosha ili viweze kuchukua nafasi yake kwa maana havizuiliki ni MAJIRA ni kama upepo unapokuja kwako kwa nguvu hauwezi kutumia mikono ili usikukuguse/kukufikia ndivyo majira yalivyo, kwani hauwezi kujidanganya kukaa macho ili kuzuia usiku usiingia wala mchana usipite ni sawa na kuiamisha bahari kwa ndoo ukitegemea utafikia siku bahari itaamia upande unako mwaga maji kupitia ndoo yako nzuri.
“ maadam dunia idumupo MAJIRA ya kupanda na kuvuna havitakoma” iko hivyo tu jua liwake hama mvua inyeshe kila kitu kitakuwa kwenye majira yake.
Uwa majira yanakuwa na nguvu nyuma yake isiyoweza kuzuiliwa na kitu chochote ni zaidi ya maji useme utaweka ukingo naam ni zaidi ya upepo useme utapita tu pasipo kusikia kishindo chake nawe uendelee na mambo yako.
Majira yana nguvu za asili na pindi inapodhihirika kwa mtu au mahali hama wakati wake haijalishi uko wapi ni lazima kusudi lake litimie na kukuchukua kwenda hatua nyingine basi hapo lazima nafasi ikutafute ndipo hapo “kapuku” anakuwa “hitaji au jibu” la watu na hatimaye anafamyika baraka kwa wengi.
Na unaweza kuwa na rafiki yako mmeshibana sana lakini majira yanaweza kukutofautisha huyu akawa rais na wewe ukaendelea kwa raia mwema na wakati mwingine usishangae muuza maji ya kandoro akawa mmiliki wa kiwanda cha kuzalisha maji.
Pia unaweza ukawa na ndoto nyingi kubwa na nzuri sana lakini nje ya majira utalaumu watu na kuona upendo umeshuka au haupo kabisa.
Ni afadhali ucheze na umeme ukakamilisha historia au biashara ikaishia hapo lakini sio majira unaweza ukaishi katika ,maumivu makali pasipo kujua ni lini maumivu yatakoma.
Ni sawa na kiongozi anashiriki katika mazishi ya mtu aliyekuwa anamtegemea kila kitu “ mfadhili wake “ machozi yake yanakuwa ni sawa na kisima kisichokauka na pengine moyoni mwake anasema laiti ningetangulia mimi ili anizike kuliko kuipata aibu hii baada ya yeye kufariki.
Haupaswi kuogopa majira bali ishi ukijua kuna majira na yanapita sawa yalivyowekwa unapokuwa umeshiba jua kuna majira ya njaa yanakuja! Na unapokuwa na nguvu jua kuna majira yanakuja ambazo hauta kuwa na nguvu ulizo kuwa awali.
Ni kama unapokuwa mtoto basi fanya mambo ya kitoto na unapokuwa kijana basi fanya yatakayo dhihirisha kuwa wewe ni kijana na pia unapokuwa mzee basi ufanye mambo yanayohusiana au yanayolingana na rika hilo na sio unapokuwa mzee ukatamani kufanya mambo ya kitoto au bibi akajitahidi kuwa kijana wa kisasa.
“ utajitahidi tu ila utakuwa kero kwa wengine”
Lazima utambue jana ikishapita imepita na mambo yake usilazimishe jana ifanane na leo hayo ni majira mengine yana mambo yake.
Ndomana mtu akiondoka uondoka na utambulisho wake pamoja na mambo yake hata mkijitahidi kumfananisha lakini huyo atakuwa kama yule, utajifariji lakini ukweli na uhalisia wake utabaki kuwa wake.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni