Katika dunia tuliyonayo kuna mambo yanafanyika ambayo unaweza kukosa majibu kwa nini yanafanyika hivi au yanakuwa hivi au mtu huyu anafanya hivi! Wakati mwingine unaweza kujipa majibu mwenyewe na pengine ukasema hayanihusu.
Kuna mambo ambayo mtu ujikuta unaguswa kufanya binafsi hata bila kushurutishwa na mtu na pengine kuamua kumshauri mtu unayemuona anafanya visivyofaa kumwambia aache au afanye kwa namna nyingine ambayo itampa matunda kama sio kumsaidia.
Mathalani unaweza kukuta mtu anasumbuliwa na figo na limefikia kiwango cha kutofanya kazi likahitaji mbadala na watu hata ndugu wakagoma kutoa figo zao ili kukuokoa maisha ya mtu walisema wanampenda na hawata mwacha kamwe katika shida yoyote lakini ghafla kwa namna isiyofikiriwa akatokea mtu mmoja ambaye inawezekana mnamfahamu au msiomfahamu akawa yuko radhi kutoa figo yake na hatimaye akaitoa figo yake! Mkabaki na butwaa……..!
Pasipo kujua inawezekana aliwahi kuweka patano na mgonjwa wakati wa uzima wake “ sitaweza kukubali kuona unapotea wakati uwezo wa kukusaidia ninao “ !alisema aliyetoa figo, na hapo alikuwa anatekeleza alichokisema kwa matendo tu.
Unaweza kukuta mtu anatenga muda wake na kwenda majalalani na kukaa na mtu mnayemuona chizi na pengine hata kula naye pasipo kujali mazingira yaliyo mzunguka au watu watanielewaje bali ujali hile raha ya nafsi yake anayoisikia pindi akifanya hicho kitendo-kuheshimu patano!.
Pia unaweza kukuta mmoja ambaye sio ndugu hiyo familia lakini yeye binafsi amejitolea kumpeleka hospitali mgonjwa wa hiyo familia kwa kutumia usafiri wake ( gari ) kumpeleka na kumrudisha nyumbani pasipo kuchangiwa hata hela ya mafuta bali siku zote ufanya hivyo uku moyo wake umejawa na furaha pasipo kuchoka, unaweza usijue kwanini anafanya hivyo unaweza kuta alishaingia mapatano kuwa “usafiri wangu utatumika kwa faida yako na hasa wakati unashida” na hapo anasimamia kile alichokisema.
Nakubaliana kabisa kuliweka patano sio kazi bali kulisimamia patano hiyo ni habari nyingine.
Mathalani kuna mapato yanawekwa nchi na nchi kutotengeneza mabomu “nuclear” ili kutoiweka dunia katika hari ya hatari lakini bado wanakwenda kinyume na hayo makubaliano, wanabaki kulaumiana wenyewe kwa wenyewe.
Pia katika hali utekelezaji kuna uwezekano kuwa unayaheshimu maagano yenu hama kuna kuna siri iliyojificha iko ndani yake.
Kuna aina mbalimbali ya mapatano lakini mimi ningependa kuongelea makundi haya ya mapatano:
i. Mapatano kati ya nafsi na nafsi
ii. Mapatano kati ya nafsi na Mungu.
Mapatano ya nafsi naam hayo mapatano nimeyaongelea kidogo hapo juu lakini pia ningependelea kuongelea mapatano kati ya nafsi na Mungu haya ni mapatano ya ajabu sana maana unaweza kukuta unafanya mambo ambayo wewe mwenyewe uyaelewi, watu awaelewi ( unaowaamini na usio waamini ) ila cha ajabu moyo wako unajawa na furaha na amani ya kutosha.
Mathalani unaweza kuwa na patano na Mungu kufuta viatu vya mtumishi pindi anapoingia kanisani kuongoza ibada aijalishi amepiga kiwi au ajapiga/ vina vumbi au havina vumbi wapo watu watainuka kinyume nawe pengine atamchungaji mwenyewe akawahaelewi na watu wakainuka na kukuvunja moyo hiyo hali isikuweke chini!
Unapoishi katika patano lako na Mungu hapo kunawiri katika utu wa ndani kuna kuwa dhahiri, nguvu ya ndani inaongezeka na macho yako yanatiwa nuru ya kiungu.
Nipatano la ajabu sana maana kuna wakati mwingine litakupeleka kujitoa mwanga mathalani hilo patano linaweza kukuweka kuwa karibu na mashoga na kuwa na mzigo nao, jamii na hata familia yako inaweza kuwa kinyume nawe hata isikuelewe unapotoa muda wako kuongea na mashoga maana watu uamini ” ukitembea na mwizi nawe utakuwa mwizi ” inabidi uwe na nguvu ya kusimamia patano lasivyo unaweza kulivunja patano lako na Mungu.
Wakati mwingine unapolitumikia patano lako na Mungu kubali kuvunja heshima ya cheo na nafasi yako katika jamii unayoishi.
Katika patano na Mungu tunaliona kwa Samson alivyoenda kinyume na utaratibu wa jamii yake ya kuoa nje ya kabila lake, lile patano lilikuwa na nguvu ndani yake naye aliamua kuliishi patano kwa gharama yoyote.
Waamuzi 14:1 Samsoni akatelemkia Timna, akaona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti.
2 Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemwona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi mnipatie, nimwoe.
3 Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu zote, hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana ananipendeza sana.
4 Lakini baba yake na mama yake hawakujua ya kuwa jambo hili ni la Bwana; maana alitaka kisa juu ya Wafilisti. Basi wakati ule Wafilisti walikuwa wakiwatawala Israeli.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………….……………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni