Kama tunavyojua milima kama miinuko iliyojitokeza katika ardhi iliyo chipuko kwa asili ( tangu dunia kuumbwa) na mingine iliyojitokeza kutokana na tabia nchi mathalani volcano na sababu nyingine! Tunaishi na kuifurahia.
Moja ya kitu kinachoweza kufanya uendelee kupanda mlima/kuendelea na safari yako ni uwezo wa jicho lako katika kuona kilele cha mlima!
“ maana pale utakapo paona ndipo utakapo pamiliki”
Kile unachokiona ndicho utakachokimiliki nje ya kuona uwezi kumiliki ( uwezi kumiliki gizani ).
Nguvu inazaliwa au kupungua kutokana na nguvu ya kuona inayozaliwa ndani yako.
“ ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo”
NI KWELI MLIMA NI MREFU LAKINI UNAPANDIKA!
Karibu!
Mwendo wako katika kupanda mlima uamliwa na ukubwa ( upana au urefu ) wa mlima hivyo masaa, siku au mwezi utakao tumia katika kufika kilele cha mlima na sio kwamba au pandiki huo mlima .
Mathalani mlima mrefu katika afrika ni KILIMANJARO na hapo haimaanishi kuwa hakuna mlima afrika zaidi Kilimanjaro la asha! Ipo milima mingi tu na iliyo na muonekano mzuri na wa kuvutia vilevile pia inapandika vizuri tu ila moja ya utofauti ya utofauti ya mlima huu ni mingine ni siku au muda utakazo tumia ili kufika kileleni.
Ukweli wakati mwingi jicho linapoona mlima vile ulivyo mkubwa unaweza kukuta miguu ikakosa nguvu na kupelekea hata moyo kughairi.
Ni muhimu ujifunze kuona jambo kwa jicho la tatu, uone tu maadam pana nafasi ya kuweka hatua kuelekea juu basi hapo uanze kuona fursa ya kwenda juu na hatimaye kufika kileleni.
Pindi akili yako inapoanza kuona kama kuna kufika basi ustahimilivu na kuvumilia mitelezi, kujikwaa na hata kuchomwa miiba na mengine mengi na hatimaye unafika.
Kuna siri kubwa sana ya ushindi inayozaliwa katika kuona kwa kuwa bila ya kuona hakuna ushindi.
“ kikubwa uwezi kwenda pasipo kuona”
Mathalani unapoona huyu mtu si mwema kwako hakuna jambo jema litakalopata kibali/kukubaliki katika moyo wako hata akicheka utaona anakusanifu.
Mungu anakuwa sawa na imani yako ukiona anaweza utaweza!, utaona uweza wake, maana ukiona kuwa ni baba yako naye atakuwa baba yako ( imani- jicho lililojichifa ). Jambo ukishaliona kuwa ni gumu ni vigumu tu yeye kukupa akili yake. ( kuyafunua macho )! Labda upate neema tu.
Macho yako yanaweza kuzuia utendaji wa kimbingu au kuruhusu utendaji wa kimbingu.
Ishara ya kukubali na kuamini Mungu ni mkubwa na hakuna linalo mshinda ni pale tu akili yako na macho yako hayataweza kuona huu mlima mkubwa na haupandiki,
“ nitayainua macho yangu ni tazame mlimani msaada wangu utatoka wapi?”
Tambua dunia na vyote vimetoka kwake yeye ndiye anajua alifanya nini milima ikatokea na mbingu ikawa juu na nchi ikawa chini na bahari/maji yakawa ni mipaka yake.
“ aliyekitengeneza anaweza kukibomoa”
Kama vyote asili yake ni yeye basi mshike yeye na wala si maneno ya watu!
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………..………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni