Ijumaa, 31 Desemba 2021

DUH! KUMBE THAMANI YA JANA HAIPOTEI KWA SABABU YA LEO.

 


Ni jambo jema na zuri kuwepo kwa mabadiliko hasa chanya katika mambo mbalimbali yanayoendelea katika ulimwengu huu, kwasababu hayo mabadiliko ndiyo yanapelekea mafanikio/ maendeleo mengi katika dunia tuliyonayo ya kianza katika jamii husika na hatimaye kuenea ulimwenguni mathalani maendeleo ya sayansi na teknolojia yalivyo pelekea urahisi wa mawasiliano na hata kurahisisha kwa usafirishaji wa watu pamoja na bidhaa kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine na faida nyingine nyingi ambazo unapoziona unaona maajabu ya akili ya Mungu kwa mwanadamu.

Kwa Afrika kwa asilimia kubwa tunashukuru Mungu  kwa sababu tulivyokuwa jana sio tulivyo leo hasa kwa upande wa mavazi , mavazi ya enzi hizo sio tunayovaa sasa japo tunayafurahia na kumshukuru Mungu kwa hilo ingawa yameboreshwa hata kupitiliza maana siku hata siku mitindo inakuja ya hatari zaidi na hata material ( malighafi ) ya tofauti tofauti kulingana na wazo ( idea ) ya mtengenezaji ( designer ) wakati mwingine nguo za kulalia zinakuwa za kutokea hapo na wanyoshea mikono mafundi “ designer “  wetu! Hakika kweli wakati tunaenda nao vizuri

Ni kweli jana na leo zote ni siku ila zinatofautiana kwa majira yake kama sio kwa tarehe.

Natambua tunamtambua umuhimu wa mkunga baada ya kumsaidia mjamzito kujifungua salama.

Na mwanafunzi wanatambua umuhimu wa mwalimu baada ya kufaulu maana sio rahisi kwa mwanafunzi aliyefeli akamtafuta mwalimu na kumwambia asante kwa kunifundisha!

Japo ni vizuri kumkumbuka mwalimu hata kama ujafanikiwa kufanya vizuri maana kuna maarifa fulani umeyapata kutoka kwake.

Ni muhimu sana kutokusahau jana kwasababu imekuja leo, kwasababu sio vitu vyote ulivyojifunza jana kuwa leo havitatumika tena.

Kwani hata chakula kilichobaki jana kinaweza faa leo ( baadhi ya familia ) ni muhimu tu ukiandae vizuri kitumike leo tena na kwa asilimia kubwa chakula kilicho lala uitwa kiporo na wengine ukifurahia sana.

Ni muhimu utambue mambo yako ya jana ambayo upaswi kwenda nayo leo na vilevile yako ya leo haupaswi kuyakataa kwa kuwa yanaweza yasikifae ila yaka mfaa mwingine na mengine yanaweza yasiwafae wote ya kaja na kupita.

Naam hata utandawazi unaokuja leo tusisahau asili yetu ya jana! Kwa kuwa kupitia utandawazi unaweza kuona mambo mbalimbali hivyo usione kila kitu kinachoonyeshwa na kupitia mtandao basi kinafaa kuwa sehemu ya maisha yako.

Wako watu wanakosoa jamii yao kwakuona kutembea katika asili yake ni kupotoka au kutoheshimu hadhi yake lah! Katika mabaya unayo yaona yako mema usiyoyaona au uliyoyasahau.

Tambua ni hao watakao kukumbatia na kukusitiri na hata kukuzika pindi utakapo pumzishwa katika nyumba yako ya milele na sio wale unaowafuata utamaduni wao!

Haijalishi kama unawajua kiasi gani japo uko mbali ( utandawazi ) jua lako litabaki kuwa lako tu na hapo awatajali kuwa wewe ni shabiki wa utamaduni wao au la!

Sio kila kitu kinacholetwa mezani kwako ukachukua na ukala lazima uangalie kwa umakini je! Hicho chakula akitaathiri afya yangu ulimbukeni usikutese.

Ni vizuri unapofanya jambo lazima liwe jema machoni pa jamii yako hasa likiwa lililo chanya kwako.

Unapokuwa kijijini ishi kama mwanakijiji na unapokuwa mjini basi ishi kimjini basi hapo utakuwa bora kwa jamii yote zaidi sana mpende Mungu.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………………………..0764 018535

Ijumaa, 10 Desemba 2021

MUNGU ANATAKA KUJIONA YEYE!



Ni kawaida tu, kibinadamu kila mtu yeyote pindi anapojingalia kwenye kioo, upenda kujiona yeye na wala sio mtu anayefanana na yeye na wala sio yeye!

Katika mambo ambayo yanayomfurahisha Mungu kama sio kumpendeza ni pindi anapomuona mwanadam anapenda ajione yeye katika kila kitu kinachohusu maisha yake afya, uchumi na mambo yote ya kijamii.

Pindi anapojiona yeye katika maisha ya mwanadamu basi hapo udhihirisha kuwa huyo ni mali yake hata bila kusema kwa mtu husika kuwa yeye ni mali ya Mungu.

Lengo kubwa la Mungu kukufanya ni kutaka utambue na kumpa heshima kama Mungu na wala sio kitu kingine.

Ndomana anapoona utendaji wako mkubwa wa akili katika mambo yanayo kukabili upenda kukuacha ili utukufu wake usichanganyike na uwezo wa kibinadamu.

Namna nyepesi ya kumruhusu Mungu atawale/ahusike na shida hama jambo lako ni kutokuwa na nia ya kuwa komoa watu bali kuhakikisha Mungu anaonekana na kuwa unakuwa kwa faida yake.

Mtihani mkubwa unakuja pale namna gani Mungu anataka aonekane katika kile unacho/kinachokukabili inawezekana kazi pengine wewe ungependa kuendelea hapo ili wale wanaokuchukia wakuone, hivyo ukawa unafunga na kuomba katika hali hiyo lakini Mungu pengine anataka uondoke hapo ili utukufu wake uonekana huko unakokwenda! AU kuna mabaya yatakuja kwenye ofisi hiyo ambayo yanaweza kuweka maisha yako rehani.

Mathalani,Daudi alikuwa anaomba ili mwanae apone na aliacha hata kula ili amshawishi Mungu afanye kitu kwa ajili ya kunusuru uhai wa mwanae lakini Mungu akutaka kuonekana kwa namna hiyo ambayo sawa na matakwa yake.

Watu wengi wanakata tama kwa kutojua namna gani Mungu anataka aonekane katika yale yanayo kukabili, mathalani wengine walitegemea afanye leo lakini Mungu alipendezwa kufanya kesho kutwa hivyo akili ya Mungu na mtu zikatofautiana, naye akashindwa kukubaliana na tofauti hiyo.

Pindi unapotambua namna gani Mungu anataka ajionyeshe kwa watu kutokana  na yale yanayo kukabili ushindi unakuwa ni haki yako mathalani wanaisraeli walipokuwa wakipigana vita Mungu aliwapa ushindi kwa namna mbalimbali sawa na namna yake au alivyokuwa anataka wakati mwingine waliimba na ushindi ukapatikana na mara nyingine Musa kwa kunyoosha mkono Israel walishinda n.k

Ukitaka kushindana na Mungu au kuchelewa katika hatua yako basi tafuta namna yako tofauti na mpango wake au alivyokusudia.

Moja ya kitu ambacho Mungu anataka akione yeye kwako pindi unavuka salama au kushinda vita ni watu wamuone yeye katika huo ushindi na sio wewe kutaka wakuone wewe! Mungu anaweza kubatili huo ushindi au usijirudie tena katika hatua inyofuata.

Unahitaji kujua Mungu anataka kujiona yeye katika maisha yako na sio mtu mwingine ili aweze kuwa Mungu kwako kwelikweli na kuchukua shida yako pamoja na kuwa furaha yako katika siku zote za maisha yako.

Unahitaji kujua Mungu anataka aonekane katika jambo lolote linalo kukabili hivyo kumruhusu aonekane kama anavyotaka ni kumshawishi atende .

Muhimu katika yote, ni vizuri utambue pindi Mungu atakavyojionyesha bila shaka nawe UTAONEKANA TU! Usiwe na haraka.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………….0764 018535