Ijumaa, 22 Aprili 2022

TULIA! LIPO JIBU

 



Kama binadamu unayeishi katika ulimwengu huu uwa unakuwa na mahitaji kulingana na wakati au hali husika.

Mbali na mahitaji ya msingi kwa binadamu ili aweze kuendelea kuishi ( mavazi, malazi na chakula )!

Katika mahitaji ya binadamu haya ni baadhi tu kutokana hali na hatua:

v  Mathalani, pindi unapohitaji maji unakuwa na kiu basi hapo utapenda upate maji na sio kitu kingine.

v  Vilevile unapokuwa na njaa basi hapo utahitaji chakula ili utimize uhitaji wa nafsi yako,

v  Naam unapofikia katika rika la kuoa au kuolewa basi hapo basi hapo utafurahi kupata mwenza wa maisha yako na sio mtoto aliyekosa mapenzi ya baba au mama.

Na kuna wakati moyo wako unaweza kosa utulivu unatamani ufanye hili au lile unaona bado alikosawa.

Wakati mwingine unatamani uchukue maamuzi ambayo yatabadilisha maisha yako lakini bado unaona sio wakati sahihi.

Na mbaya zaidi wakati mwingine unatamani hata ugombane au ulianzishe lakini bado upati amani katika moyo wako.

Nipende kusema kuwa hali hiyo uliyonayo wewe sio wa kwanza hata yesu mwenyewe ilishawai kumpata!

Marko 14:36 Akasema, Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe

Kama binadamu kuna wakati unafika unaweza fika na kujiuliza hivi niendelee na safari au nirudi nilikotoka,

Ikumbukwe hayo ni majira ambayo nilazima utayapitia na sio kwa wakati mmoja tu bali kila ngazi  mpya Mungu atakapo kukupeleka lazima hali hiyo isababishe kukosa utulivu.

Bila shaka katika hali hiyo unahitaji kujua  mahitaji ya msingi ili uweze kuwa salama katika kipindi hicho naam utahitaji utulivu wa akili na wa nafsi tayari kusikia sauti ya amani inayoweza kukutoa hapo ulipo!

Ikumbukwe farao alipoota ndoto ile ndoto iliyosababisha moyo wake kutangatanga na kutafuta jibu litakalosababisha amani ya kweli katika akili na moyo wake.

Na baada kutafuta kwa muda mrefu kutafuta jibu la ndoto yake kwa watu aliowaamini na hata waganga aliowategemea bado awakuweza kusababisha amani katika moyo wake,

Ndipo kijana yusufu akaitwa ili kutatua swali la mfalme lililoleta giza katika nchi nzima!

Mwanzo 41:16 Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani.

Ni lazima Mungu akupe jibu litakalosababisha amani ndani yako, linaweza kupitia mtu au Mungu mwenyewe.

Unapoamua maamuzi ya kutulia katika hali hiyo sio kwamba umeshindwa bali ni hali ya kuruhusu nguvu ifanye kazi kwa namna yake au kupitia wewe.

Muhimu kujua kuwa unapombeba Mungu anakuwa yeye anafanya kupitia wewe hivyo  kuruhusu wewe kushindwa na yeye kusema ameshindwa na anaitwa ni MUNGU ASIYEISHINDWA! Ni kitu kisichowezekana.

Hauhitaji kujiona umeshindwa pindi mbingu inakuwa upande wako maana ni yeye pekee anayeweza kuifanya kesho kutwa ikawa leo na leo ikawa jana yaani ni Mungu anashangaza na anafanya ili ushangae.

Anaitwa mwanzo maana ndiye jina lake na mwisho maana ndio ukamilifu wake anapoanza jambo ni lazima alikamilishe asili ya vyote viko mikononi mwake.

Anaitwa NIKO  AMBAYE  NIKO!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………..0764 018535

Ijumaa, 8 Aprili 2022

SIRI YANGU

 



Mahali ambapo mtu akijiangalia anajiona yeye! Naam na hii ni zaidi ya kioo,  kwani kioo kinaweza kisikuonyeshe hali halisi yako ikakuacha katika kasoro na pengine hata kupelekea kujisahau fulani lakini sio mahali penye SIRI YAKO maana hapo pengine umeweka staha yako.

Naam mtu anaweza akacheka au kulia sana na wote mkasikitika naye kama sio kulia bali au ila yeye mwenyewe anajua uhalisia wake kama kweli analia au anacheka na kwasababu gani hiyo inaitwa SIRI YAKE.

Mahali penye siri kunaweza kuwa ni chanzo cha unyonge  au ujasiri wa mtu husika.

Na endapo ukajua siri ya mtu unakuwa ni sawa na mtu aliye uchi mbele zako! ( japo inategemea uzito wa siri )!

Ndo mana kwa baadhi ya watu pindi wanapogundua siri yake imeshajulikana kuchukua maamuzi ya kuhatarisha maisha yake ni kitu kinawezakana hama kujiua kabisa.

Unapotaka kumshinda mtu kirahisi haijalishi dunia ina mwogopa kiasi gani basi tambua chanzo cha uimara!

Mathalani, ndomana Daudi ilikuwa rahisi kumshinda Goliath japo alikuwa tishio katika dunia ila Daudi alitambua siri na udhaifu wa Miungu yake anayoitegemea hivyo jiwe moja tu likatosha kuwaondelea aibu Israel yote.

Ø  Samson na siri ya nguvu zake!

Waamuzi 16:16 Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa.

 17 Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu.

 18 Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.

 19 Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka.

 

Japo ili kusudiwa Samson kukamatwa na kuteswa na hatimaye kufanyika mkombozi  kwa watu wa Mungu.

 

Pia ziko siri zinazo mtafuna mtu kimya kimya hata kupelekea kifo chake, mathalani mtu anakataa kuwatoa  sadaka ndugu zake na wengine  ( imani za kishirikina ) hivyo anajitoa sadaka mwenyewe na anakubali kufa pasipo kusema siri hiyo na anakubali kufa na siri yake moyoni.

Japo kuna siri ambazo mtu anakufa nazo pasipo kusema inawezekana  labda ni aibu au heshima yake itashuka hivyo anakubali kupotea nayo lakini pengine angesema inawezekana angepata muafaka wa jambo lake.

Pia, wako watu wanagombana na kushindwa kukaa pamoja kutokana mtu mmoja ametoa siri zake kwa watu asiopenda wajue/ wafahamu jambo lake.

Nakubaliana kabisa kuwa siri ni heshima au staha ya mtu, na inapotokea mtu kuvujisha au kutoa siri zako bila shaka unamuona ameamua kukuabisha lakini inawezekana sio kweli!

Tambua mtu kuvujisha siri zako haizuii hatma ya Mungu kutimia katika maisha yako, Ni kweli anaweza mtu kuvujisha siri zako anataka akuone umeshuka chini mavumbini lakini Mungu anaweza kukutoa hapo mavumbini na kukuweka juu.

 

Ø  Mtazame tena Samson:

 

Waamuzi16:21 Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.

 22 Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake.

 23 Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu.

 24 Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu.

 25 Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili.

 26 Samsoni akamwambia yule kijana aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate kuzitegemea.

 27 Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza.

 28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.

 29 Kisha Samsoni akazishika nguzo mbili za katikati ambazo nyumba ile ilikaa juu yake, akazitegemea, moja kwa mkono wake wa kuume na moja kwa mkono wake wa kushoto.

 30 Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. Basi wale watu aliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko wale aliowaua wakati wa uhai wake.

 31 Ndipo ndugu zake, na watu wote wa nyumba ya baba yake wakatelemka, wakamtwaa wakamchukua, wakamzika kati ya Sora na Eshtaoli, katika kiwanja cha kuzikia cha Manoa baba yake. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka ishirini.

 

Ni kweli siri inapotambulika unakuwa kama kuku aliyeloa lakini hatma ya Mungu haloi wala haipukutiki imeshikwa na asili yake na kuambatanishwa na maisha yako.

Unapokuwa umeinama kuutazama hile aibu au mateso unayoyapitia kwa kujulikana siri yako lakini ujue mpango wake haujawai kufeli wala kushindwa!

Unahitaji kujua siri itabaki kuwa siri na maisha yako na yataendelea kuwa ni maisha yako usikubali kuutoa uhai wako kwa sababu siri imejulikana na watu wengi.

Ni muhimu utambue watu wanaweza kujua siri zako na baadae waka pumzika kwa amani ( kufariki ) lakini sio hazina ya kimungu iliyo ndani na hiyo ndio iliyoshikilia hatma ya maisha yako.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………………………..0764 018535