Kama binadamu unayeishi katika ulimwengu huu uwa unakuwa na mahitaji kulingana na wakati au hali husika.
Mbali na mahitaji ya msingi kwa binadamu ili aweze kuendelea kuishi ( mavazi, malazi na chakula )!
Katika mahitaji ya binadamu haya ni baadhi tu kutokana hali na hatua:
v Mathalani, pindi unapohitaji maji unakuwa na kiu basi hapo utapenda upate maji na sio kitu kingine.
v Vilevile unapokuwa na njaa basi hapo utahitaji chakula ili utimize uhitaji wa nafsi yako,
v Naam unapofikia katika rika la kuoa au kuolewa basi hapo basi hapo utafurahi kupata mwenza wa maisha yako na sio mtoto aliyekosa mapenzi ya baba au mama.
Na kuna wakati moyo wako unaweza kosa utulivu unatamani ufanye hili au lile unaona bado alikosawa.
Wakati mwingine unatamani uchukue maamuzi ambayo yatabadilisha maisha yako lakini bado unaona sio wakati sahihi.
Na mbaya zaidi wakati mwingine unatamani hata ugombane au ulianzishe lakini bado upati amani katika moyo wako.
Nipende kusema kuwa hali hiyo uliyonayo wewe sio wa kwanza hata yesu mwenyewe ilishawai kumpata!
Marko 14:36 Akasema, Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe
Kama binadamu kuna wakati unafika unaweza fika na kujiuliza hivi niendelee na safari au nirudi nilikotoka,
Ikumbukwe hayo ni majira ambayo nilazima utayapitia na sio kwa wakati mmoja tu bali kila ngazi mpya Mungu atakapo kukupeleka lazima hali hiyo isababishe kukosa utulivu.
Bila shaka katika hali hiyo unahitaji kujua mahitaji ya msingi ili uweze kuwa salama katika kipindi hicho naam utahitaji utulivu wa akili na wa nafsi tayari kusikia sauti ya amani inayoweza kukutoa hapo ulipo!
Ikumbukwe farao alipoota ndoto ile ndoto iliyosababisha moyo wake kutangatanga na kutafuta jibu litakalosababisha amani ya kweli katika akili na moyo wake.
Na baada kutafuta kwa muda mrefu kutafuta jibu la ndoto yake kwa watu aliowaamini na hata waganga aliowategemea bado awakuweza kusababisha amani katika moyo wake,
Ndipo kijana yusufu akaitwa ili kutatua swali la mfalme lililoleta giza katika nchi nzima!
Mwanzo 41:16 Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani.
Ni lazima Mungu akupe jibu litakalosababisha amani ndani yako, linaweza kupitia mtu au Mungu mwenyewe.
Unapoamua maamuzi ya kutulia katika hali hiyo sio kwamba umeshindwa bali ni hali ya kuruhusu nguvu ifanye kazi kwa namna yake au kupitia wewe.
Muhimu kujua kuwa unapombeba Mungu anakuwa yeye anafanya kupitia wewe hivyo kuruhusu wewe kushindwa na yeye kusema ameshindwa na anaitwa ni MUNGU ASIYEISHINDWA! Ni kitu kisichowezekana.
Hauhitaji kujiona umeshindwa pindi mbingu inakuwa upande wako maana ni yeye pekee anayeweza kuifanya kesho kutwa ikawa leo na leo ikawa jana yaani ni Mungu anashangaza na anafanya ili ushangae.
Anaitwa mwanzo maana ndiye jina lake na mwisho maana ndio ukamilifu wake anapoanza jambo ni lazima alikamilishe asili ya vyote viko mikononi mwake.
Anaitwa NIKO AMBAYE NIKO!
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni