Mahali ambapo mtu akijiangalia anajiona yeye! Naam na hii ni zaidi ya kioo, kwani kioo kinaweza kisikuonyeshe hali halisi yako ikakuacha katika kasoro na pengine hata kupelekea kujisahau fulani lakini sio mahali penye SIRI YAKO maana hapo pengine umeweka staha yako.
Naam mtu anaweza akacheka au kulia sana na wote mkasikitika naye kama sio kulia bali au ila yeye mwenyewe anajua uhalisia wake kama kweli analia au anacheka na kwasababu gani hiyo inaitwa SIRI YAKE.
Mahali penye siri kunaweza kuwa ni chanzo cha unyonge au ujasiri wa mtu husika.
Na endapo ukajua siri ya mtu unakuwa ni sawa na mtu aliye uchi mbele zako! ( japo inategemea uzito wa siri )!
Ndo mana kwa baadhi ya watu pindi wanapogundua siri yake imeshajulikana kuchukua maamuzi ya kuhatarisha maisha yake ni kitu kinawezakana hama kujiua kabisa.
Unapotaka kumshinda mtu kirahisi haijalishi dunia ina mwogopa kiasi gani basi tambua chanzo cha uimara!
Mathalani, ndomana Daudi ilikuwa rahisi kumshinda Goliath japo alikuwa tishio katika dunia ila Daudi alitambua siri na udhaifu wa Miungu yake anayoitegemea hivyo jiwe moja tu likatosha kuwaondelea aibu Israel yote.
Ø Samson na siri ya nguvu zake!
Waamuzi 16:16 Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa.
17 Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu.
18 Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.
19 Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka.
Japo ili kusudiwa Samson kukamatwa na kuteswa na hatimaye kufanyika mkombozi kwa watu wa Mungu.
Pia ziko siri zinazo mtafuna mtu kimya kimya hata kupelekea kifo chake, mathalani mtu anakataa kuwatoa sadaka ndugu zake na wengine ( imani za kishirikina ) hivyo anajitoa sadaka mwenyewe na anakubali kufa pasipo kusema siri hiyo na anakubali kufa na siri yake moyoni.
Japo kuna siri ambazo mtu anakufa nazo pasipo kusema inawezekana labda ni aibu au heshima yake itashuka hivyo anakubali kupotea nayo lakini pengine angesema inawezekana angepata muafaka wa jambo lake.
Pia, wako watu wanagombana na kushindwa kukaa pamoja kutokana mtu mmoja ametoa siri zake kwa watu asiopenda wajue/ wafahamu jambo lake.
Nakubaliana kabisa kuwa siri ni heshima au staha ya mtu, na inapotokea mtu kuvujisha au kutoa siri zako bila shaka unamuona ameamua kukuabisha lakini inawezekana sio kweli!
Tambua mtu kuvujisha siri zako haizuii hatma ya Mungu kutimia katika maisha yako, Ni kweli anaweza mtu kuvujisha siri zako anataka akuone umeshuka chini mavumbini lakini Mungu anaweza kukutoa hapo mavumbini na kukuweka juu.
Ø Mtazame tena Samson:
Waamuzi16:21 Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.
22 Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake.
23 Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu.
24 Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu.
25 Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili.
26 Samsoni akamwambia yule kijana aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate kuzitegemea.
27 Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza.
28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.
29 Kisha Samsoni akazishika nguzo mbili za katikati ambazo nyumba ile ilikaa juu yake, akazitegemea, moja kwa mkono wake wa kuume na moja kwa mkono wake wa kushoto.
30 Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. Basi wale watu aliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko wale aliowaua wakati wa uhai wake.
31 Ndipo ndugu zake, na watu wote wa nyumba ya baba yake wakatelemka, wakamtwaa wakamchukua, wakamzika kati ya Sora na Eshtaoli, katika kiwanja cha kuzikia cha Manoa baba yake. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka ishirini.
Ni kweli siri inapotambulika unakuwa kama kuku aliyeloa lakini hatma ya Mungu haloi wala haipukutiki imeshikwa na asili yake na kuambatanishwa na maisha yako.
Unapokuwa umeinama kuutazama hile aibu au mateso unayoyapitia kwa kujulikana siri yako lakini ujue mpango wake haujawai kufeli wala kushindwa!
Unahitaji kujua siri itabaki kuwa siri na maisha yako na yataendelea kuwa ni maisha yako usikubali kuutoa uhai wako kwa sababu siri imejulikana na watu wengi.
Ni muhimu utambue watu wanaweza kujua siri zako na baadae waka pumzika kwa amani ( kufariki ) lakini sio hazina ya kimungu iliyo ndani na hiyo ndio iliyoshikilia hatma ya maisha yako.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni