Ijumaa, 6 Mei 2022

UPEKEE WA KIJANA WA KIUME!



 

Kijana kama nguzo tegemeo katika jamii yake!

Uwa familia inakuwa na furaha sana pindi inapoona ina vijana wa kubwa wanaojitambua na kuwa mwelekeo katika jamii husika.

Vijana ni rika lililopo kati ya miaka 18-35, pia inaweza kwenda hadi miaka 45 na bado akaitwa ni kijana na jamii ikamtambua hivyo!

Hii ni hatua sio ya msingi tu bali pia ina upekee wake kuliko hatua zingine, mambo yanayochipua katika hatua hii ni ngumu sana kuchipua katika hatua nyingine ya mwanadamu katika ukuaji wake,

Biblia inasema fahari ya kijana ni nguvu zake! Uwa ina maanisha hivyo kuwa nguvu alizonazo kijana uwezi kulinganisha na mtoto au mtu mzima mwenye umri zaidi ya 45,

Naam kijana kama kijana utofauti wake katika rika lingine uanzia kwenye jina KIJANA, likiwa limebeba sifa na tabia za ujana lililobebwa na uweza ulio ndani ya hatua hiyo.

Kijana ni neno lililobeba jinsia zote mbili lakini tutajikita zaidi katika jinsia ya kiume.

Kijana wa kiume “ mtoto wa kiume “  ana namna anayo chukuliwa na kuandaliwa kama mtoto wa kiume tofauti kijana wa kike “ binti “

Kutoka 1:16 akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.

Upekee unaanza hapo, japo wote ni vijana lakini ipo jinsia mmoja inawindwa kuliko nyingine.

Dunia ina hofia jinsia hii!

Kuna upekee unaodhihirika katika:

(a)    Katika muonekano

i.                    Wa ndani

ii.                  Wa nje

(b)   Katika kubeba kusudi

A.MUONEKANO

Ni vile anavyotakiwa kuwa na picha pindi unaposikia neno kijana wa kiume, namna ya fikra zako inavyokupa picha na kusema huyu ndiye kijana wa kiume:

Katika muonekano wa ndani:

Kuna vitu vinatakiwa viwe ndani yake ambavyo vitamtofautisha na rika lingine,

(i)                 Fikra

Fikra ni uwanja muhimu sana katika kumtambulisha kijana huyu na kumtofautisha na rika lingine maana fikra za kijana zinategemewa kuwa ni fikra chanya zinazo endana na wakati uliopo, zilizo jaa faida zaida kuliko hasara.

(ii)               Mtazamo wake.

Ni hali ya kutafsiri mambo katika kuleta ufumbuzi sahihi katika jamii yake hata ikibidi kuhatarisha maisha ili jamii yake iwe salama, haijalishi jamii inamuelewaje?

Bali yeye ujali usalama wa kesho katika jamii yake.

(iii)             Hulka zake

Asiwe na hulka za kizamani( kizee zee) bali hizo hulka zimtambulishe sasa huyu ni kijana katika uwanda wake.

(iv)             Tabia ya ujasiri na kuthubutu

Hii kitu ndicho kinachotegemewa kwa sehemu kubwa kionekane katika maisha ya kijana maana yeye ndio tumaini la jamii yake katika changamoto mbalimbali zinazo ikabili jamii yake, wakati mwingine anaweza kuweka maisha rehani ili kuleta ufumbuzi wa jambo katika jamii husika.

(v)               Hali ya kutochoka

Pia ni sifa inayomtambulisha kijana kuchokachoka katika kusimamia kwa kile anachokiamini, katika mambo mengi anaweza kusimama na kuwa salama pasipo kuchoka labda tu mwili wake ushambuliwe na maradhi,

Endapo utakuwa unachoka bila shaka utazuwa maswali katika kichwani kwa watu kuwa huyu ni kijana kweli au mzee anayeutaka ujana.

Pia katika rika hili kufanya makosa kwake ni sehemu ya kujifunza ili baade aweze kufanya kitu bora zaidi, hivyo apaswi kuchoka haraka.

Katika muonekano wa nje:

Kwa kiasi kikubwa utambulisho wake ubwebe na jinsia katika maumbile yake ya kiume;

-          Kifua chake ( kutokuwa na maziwa )

-          Koromeo

-          Kuota ndevu

Endapo na jinsia nyingine ikiwa na vitu hivyo tofauti na jinsia ya kiume kutakuwa na shida katika maumbile ya ndani kama sio homoni ya jinsia nyingine kuzidi katika mwili wake kuliko homoni ya jinsia yake kuu, ( homoni imbalance ).

 

B.KUBEBA KUSUDI

Hapa ndio kiini cha somo langu, mbali na muonekano kusababisha utofauti pia kusudi linaenda mbali zaidi ikiwa wote ni vijana wa kiume lakini kusudi linaweza kutofautisha mmoja na mwingine unaweza kupenda au kutopenda hama kujua au kutojua.

Wote ni vijana lakini kusudi tofauti miongoni mwao litaanza kuwatofautisha wanaweza wasijue lakini lile kusudi litawaendesha na kuwapeleka kule linakuwa taka waende.

Ni muhimu ujue kijana aliyebeba kusudi na kulielewa hilo kusudi anakuwa ni zaidi ya mtu aliyebeba bomu tayari kwa kujitoa mwanga.

Anakuwa ni mtu aliye tayari kulifia kusudi lake kwa gharama yoyote inakuwa ni sawa aliyepewa ndege ili aende agonge jingo na ndipo hapo panakuwa mwisho wa maisha yake.

Ni muhimu kujua mtu anapopewa/ kubeba kusudi la Mungu unakuwa umepewa dhamana na mbingu hivyo usaidizi wote wa mbingu uko nyuma kwa ajili ya kukupa usaidizi wowote utakao uhitaji ili mradi litimize lile ulilokusudiwa.

Na ujue plan ya Mungu haijawai kufail!

Kama vile mvua ishukavyo juu ya ardhi kwa ajili ya kuchipua ndivyo litakavyo kuwa neno langu litokalo kinywani mwangu litakwenda kutimiza makusudi yote niliyo lituma. ( isaya 55:11 )!

Hivyo kijana anapobeba kusudi la Mungu kwa ajili kulitimiza hapa duniani anakuwa ni hatari kwa kuwa alichobeba kimebeba uzima wa maisha ya wengi.

Hivyo unakuwa mtu ni hatari kwa sababu amebeba hatari ( mtu aliyebeba bomu la nuclear )

Kijana aliyebeba kusudi anakuwa anaweza kupitia katika changamoto/mitihani mingi kutokana na kile alichokibeba, maana alichokibeba anakielewa mwenyewe na hakuna anayekielewa wala usaidizi wowote.

Mifano ya watu waliotofautishwa na kusudi!

a)      Yusufu

b)      Samson

c)      Yesu

Maadam unajua unalokusudi jua nguvu imekuatamia haitakuacha hadi ulichokibeba kudhihirika kwa watu waone nuru.

Unapojua unalokusudi lazima ujifunge mkanda ( kulikubali kusudi ) ili nguvu inaposhuka ikukute na moyo uliotayari.

Yesu alisema” kikombe hiki kiniepuke lakini sio kama nipendavyo bali mapenzi yatimizwe”.

Ni Mungu amekuamini akakupa hilo jukumu/kusudi liheshimu mfanye Mungu haone ajakosea kukupa wewe hilo kusudi.

Ni muhimu ujue kwa hilo kusudi umepewa dhamana na mbingu kuwepo duniani ni sawa unaitwa na rais ikulu hiyo ni fursa ambayo haitajirudia.

Ni vizuri usaidizi wa Mungu ulionao juu ya hilo kusudi lililoko ndani yako huo ndio usaidizi tosha huna haja kuangaza macho yako uku na uku ukihitaji msaidizi kwa watu.

Ahuhitaji mambo mengi bali maisha ya kusoma neno la Mungu na maombi yakiwa ni fungu lako ili uzidi kuhatamia kile ulichokibeba ndani yako.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………….……………….0764 018535

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni