Ijumaa, 27 Mei 2022

USIKAE CHINI, INGAWA NI KWELI UMECHOKA!

 



Mwanzo 40: 14 Ila unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii.

Ø  Yusufu anaonyesha namna alivyochoka katika maisha ya gereza, akihitaji msaada wa kutoka katika maisha ya utumwa wa gereza!

Mwanzo 43: 14 Mungu Mwenyezi na awape rehema usoni pa mtu yule ili awafungulie ndugu yenu huyo mwingine, na Benyamini. Nami nikifiwa na watoto wangu, nimefiwa.

Ø  Ni kauli ya yakobo ikionyesha namna alivyochoka na kukata tamaa kwa kupotea kwa mtoto wake yusufu!

Karibu!

Sifa moja ya kukaa chini ni ishara ya kuchoka, japo sio kila anayekaa chini anaashiria kuwa amechoka !

Wapo watu wasio tamani kukaa chini ila inapowalazimu wanakuwa hawana namna! Maana imebidi na wala sio hiari tena.

Na pindi unapomuona mtu anakaa chini huna haja ya kumcheka kwa sababu hujui amekutana na nini kikamlazimu kukaa chini ila hapo iwe funzo kwako na kuzidi kuomba Mungu kuwa hali hiyo isikukute, na ikitokea umeenda chini basi nguvu ya kuinuka ikuvike.

Ni kweli dunia na mambo yaliyoko ndani yake yanakukusudia kukuweka chini kama sio kukupoteza kabisa, lakini usiruhusu kukaa chini.

Mathalani, unaweza kuwa mwanandoa uliyepoteza watoto tisa (9) pindi kila anafikia hatua kujifungua basi anafariki na sasa unaujauzito na siku za kujifungua zimekaribia na picha iliyo kichwani mwako ni kupoteza tena pamoja na hali hiyo kukuzongazonga hakikisha usiiruhusu hali hiyo ikamate moyo wako.

Pia unaweza kuwa ni mwanafunzi wa kidato cha nne/sita umekuwa ukirudia mitihani ili upate credit ili uende hatua nyingine na sasa umerudia hii ni mara ya tano ( 5 ) katika hali hiyo usiruhusu kukaa chini maana bado unayo nafasi.

Unaweza kuwa ni kijana ulipata kuwa na mahusiano na watu 14 hata mlifikia hatua ya karibu ya kufunga ndoa lakini ikashindikana na inawezekana baadhi yao umeshiriki nao ngono hivyo aibu na ukiwa pamoja na hatia kama nuksi inatawala hisia zako na sasa uko wa kumi na tano (15 ) bado akili yako ijapata matumaini kabisa katika hali hiyo usiruhusu kukaa chini.

Mbali na kusoma pia unaweza kuwa umejaribu biashara nyingi lakini zote zimekufa na hata hii uliyonayo unaona inaenda kufa pamoja na uhalisia huo ukisukumwa na mawazo yako pamoja na moyo wako kuinama katika hali hiyo usiruhusu kukaa chini

Ni muhimu utambue kuwa sio mara zote unapokaa chini unaweza kuinuka wakati mwingine neema na nguvu inaweza isiwepo.

Na msingi katika yote ni lazima ujue katika hali hiyohiyo inayokukabili kuna watu wanategemea ushindi wako ili waishi.

Pia ni vizuri ujue hata kama watu wote wamekaa chini ulio wategemea na uliowaamini lakini bado hali hiyo isikukamate tambua kila mtu ana neema yake pamoja na kila jambo lina majira yake.

“ MAUMIVU YA MWISHO NDIO MNG’AO WA KESHO”

Katika yote usikubali kuyasikiliza maumivu bali angalia mng’ao wa kesho.

Ni sawa na mjamzito anavumilia maumivu ( uchungu ) kwa ajili ya heshima yake ya kupakata!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………………..0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni