Kijana kama nguzo
tegemeo katika jamii yake!
Uwa familia inakuwa na
furaha sana pindi inapoona ina vijana wa kubwa wanaojitambua na kuwa mwelekeo
katika jamii husika.
Vijana ni rika lililopo
kati ya miaka 18-35, pia inaweza kwenda hadi miaka 45 na bado akaitwa ni kijana
na jamii ikamtambua hivyo!
Hii ni hatua sio ya
msingi tu bali pia ina upekee wake kuliko hatua zingine, mambo yanayochipua
katika hatua hii ni ngumu sana kuchipua katika hatua nyingine ya mwanadamu
katika ukuaji wake,
Biblia inasema fahari
ya kijana ni nguvu zake! Uwa ina maanisha hivyo kuwa nguvu alizonazo kijana
uwezi kulinganisha na mtoto au mtu mzima mwenye umri zaidi ya 45,
Naam kijana kama kijana
utofauti wake katika rika lingine uanzia kwenye jina KIJANA, likiwa limebeba
sifa na tabia za ujana lililobebwa na uweza ulio ndani ya hatua hiyo.
Kijana ni neno
lililobeba jinsia zote mbili lakini tutajikita zaidi katika jinsia ya kiume.
Kijana wa kiume “ mtoto
wa kiume “ ana namna anayo chukuliwa na
kuandaliwa kama mtoto wa kiume tofauti kijana wa kike “ binti “
Kutoka
1:16
akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na
kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni
mtoto mwanamke, na aishi.
Upekee
unaanza hapo, japo wote ni vijana lakini ipo jinsia mmoja inawindwa kuliko
nyingine.
Dunia ina
hofia jinsia hii!
Kuna upekee
unaodhihirika katika:
(a)
Katika muonekano
i.
Wa ndani
ii.
Wa nje
(b)
Katika kubeba kusudi
A.MUONEKANO
Ni vile anavyotakiwa
kuwa na picha pindi unaposikia neno kijana wa kiume, namna ya fikra zako
inavyokupa picha na kusema huyu ndiye kijana wa kiume:
Katika
muonekano wa ndani:
Kuna vitu vinatakiwa viwe
ndani yake ambavyo vitamtofautisha na rika lingine,
(i)
Fikra
Fikra ni uwanja muhimu
sana katika kumtambulisha kijana huyu na kumtofautisha na rika lingine maana
fikra za kijana zinategemewa kuwa ni fikra chanya zinazo endana na wakati
uliopo, zilizo jaa faida zaida kuliko hasara.
(ii)
Mtazamo wake.
Ni hali ya kutafsiri
mambo katika kuleta ufumbuzi sahihi katika jamii yake hata ikibidi kuhatarisha
maisha ili jamii yake iwe salama, haijalishi jamii inamuelewaje?
Bali yeye ujali usalama
wa kesho katika jamii yake.
(iii)
Hulka zake
Asiwe na hulka za
kizamani( kizee zee) bali hizo hulka zimtambulishe sasa huyu ni kijana katika
uwanda wake.
(iv)
Tabia ya ujasiri na kuthubutu
Hii kitu ndicho
kinachotegemewa kwa sehemu kubwa kionekane katika maisha ya kijana maana yeye
ndio tumaini la jamii yake katika changamoto mbalimbali zinazo ikabili jamii
yake, wakati mwingine anaweza kuweka maisha rehani ili kuleta ufumbuzi wa jambo
katika jamii husika.
(v)
Hali ya kutochoka
Pia ni sifa
inayomtambulisha kijana kuchokachoka katika kusimamia kwa kile anachokiamini,
katika mambo mengi anaweza kusimama na kuwa salama pasipo kuchoka labda tu
mwili wake ushambuliwe na maradhi,
Endapo utakuwa unachoka
bila shaka utazuwa maswali katika kichwani kwa watu kuwa huyu ni kijana kweli
au mzee anayeutaka ujana.
Pia katika rika hili
kufanya makosa kwake ni sehemu ya kujifunza ili baade aweze kufanya kitu bora
zaidi, hivyo apaswi kuchoka haraka.
Katika
muonekano wa nje:
Kwa kiasi kikubwa
utambulisho wake ubwebe na jinsia katika maumbile yake ya kiume;
-
Kifua chake ( kutokuwa na maziwa )
-
Koromeo
-
Kuota ndevu
Endapo na jinsia
nyingine ikiwa na vitu hivyo tofauti na jinsia ya kiume kutakuwa na shida
katika maumbile ya ndani kama sio homoni ya jinsia nyingine kuzidi katika mwili
wake kuliko homoni ya jinsia yake kuu, ( homoni imbalance ).
B.KUBEBA KUSUDI
Hapa ndio kiini cha
somo langu, mbali na muonekano kusababisha utofauti pia kusudi linaenda mbali
zaidi ikiwa wote ni vijana wa kiume lakini kusudi linaweza kutofautisha mmoja
na mwingine unaweza kupenda au kutopenda hama kujua au kutojua.
Wote ni vijana lakini
kusudi tofauti miongoni mwao litaanza kuwatofautisha wanaweza wasijue lakini
lile kusudi litawaendesha na kuwapeleka kule linakuwa taka waende.
Ni muhimu ujue kijana
aliyebeba kusudi na kulielewa hilo kusudi anakuwa ni zaidi ya mtu aliyebeba
bomu tayari kwa kujitoa mwanga.
Anakuwa ni mtu aliye
tayari kulifia kusudi lake kwa gharama yoyote inakuwa ni sawa aliyepewa ndege
ili aende agonge jingo na ndipo hapo panakuwa mwisho wa maisha yake.
Ni muhimu kujua mtu
anapopewa/ kubeba kusudi la Mungu unakuwa umepewa dhamana na mbingu hivyo
usaidizi wote wa mbingu uko nyuma kwa ajili ya kukupa usaidizi wowote utakao
uhitaji ili mradi litimize lile ulilokusudiwa.
Na ujue plan ya Mungu
haijawai kufail!
Kama vile mvua
ishukavyo juu ya ardhi kwa ajili ya kuchipua ndivyo litakavyo kuwa neno langu litokalo
kinywani mwangu litakwenda kutimiza makusudi yote niliyo lituma. ( isaya 55:11
)!
Hivyo kijana anapobeba
kusudi la Mungu kwa ajili kulitimiza hapa duniani anakuwa ni hatari kwa kuwa
alichobeba kimebeba uzima wa maisha ya wengi.
Hivyo unakuwa mtu ni
hatari kwa sababu amebeba hatari ( mtu aliyebeba bomu la nuclear )
Kijana aliyebeba kusudi
anakuwa anaweza kupitia katika changamoto/mitihani mingi kutokana na kile
alichokibeba, maana alichokibeba anakielewa mwenyewe na hakuna anayekielewa
wala usaidizi wowote.
Mifano ya watu
waliotofautishwa na kusudi!
a)
Yusufu
b)
Samson
c)
Yesu
Maadam unajua unalokusudi
jua nguvu imekuatamia haitakuacha hadi ulichokibeba kudhihirika kwa watu waone
nuru.
Unapojua unalokusudi
lazima ujifunge mkanda ( kulikubali kusudi ) ili nguvu inaposhuka ikukute na
moyo uliotayari.
Yesu alisema” kikombe
hiki kiniepuke lakini sio kama nipendavyo bali mapenzi yatimizwe”.
Ni Mungu amekuamini
akakupa hilo jukumu/kusudi liheshimu mfanye Mungu haone ajakosea kukupa wewe
hilo kusudi.
Ni muhimu ujue kwa hilo
kusudi umepewa dhamana na mbingu kuwepo duniani ni sawa unaitwa na rais ikulu
hiyo ni fursa ambayo haitajirudia.
Ni vizuri usaidizi wa
Mungu ulionao juu ya hilo kusudi lililoko ndani yako huo ndio usaidizi tosha
huna haja kuangaza macho yako uku na uku ukihitaji msaidizi kwa watu.
Ahuhitaji mambo mengi
bali maisha ya kusoma neno la Mungu na maombi yakiwa ni fungu lako ili uzidi
kuhatamia kile ulichokibeba ndani yako.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………….……………….0764 018535