Ijumaa, 24 Juni 2022

USIOGOPE KUSIMAMA MAANA HUO NDIO MWANZO WA KUTEMBEA:

 



Katika ukuaji wa mtoto kuna hatua anazotakiwa kupitia ili kuweza kutembea na hatimaye kukimbia na kila hatua ina umuhimu wake……. Naam ili aweze kutembea ni muhimu aweze kusimama kwanza!

Ni hali ya kawaida kibinadamu, kuvutiwa na jambo jema au kitu kinachooneka katika muonekano wa kupendeza macho ( kuvutia ) mathalani unapoona nyumba nzuri ya kisasa ukadhani imeshushwa tu ikawa hapo, pasipo kujua walianza na msingi kabla ya kufikia hapo au katika ukamilifu wake.

Mathalani  pindi unapokuwa na ndoto ya kuwa mfanya biashara mkubwa, lakini  mawazo na uwoga wa kupata hasara unaweza kukupa hofu ya kuanza hiyo biashara hivyo ukabaki kufikiri tu.

Kuna watu awapendi misukosuko katika hatua ya awali pasipo kujua misukosuko ndio inajenga uimara wao wa kesho, na msingi bora wa kesho unategemea misukosuko ya leo.

Kwa mwanamke mwenye akili na mwenye mapenzi ya kweli kwa mwanae uwa anakaa uku anamategemeo kuwa miezi  kadhaa ikifika utegemea kumuona mtoto wake akitembea mwenyewe na pindi anapoona anachelewa kutembea inaanza kumsumbua moyoni mwake hivyo uweza kumfanyisha mazoezi na hata kumnunulia vitu au kumpa visaidizi ili aweze kumsaidia kutembea ( mapenzi ya mama kwa mtoto wake ).

Karibu katika somo!

Usiogope kusimama maana huo ndio mwanzo wa kutembea:

Inawezekana kabisa ni kweli ujawahi kusimama mwenyewe katika jambo lolote, hata unalolifikiria unahisi utaanguka au watu watakuonaje maana walizoea kuona katika hali fulani tu! Usiogope ni kama mtoto anapotoka katika hatua ya kutambaa na kuanza kusimama japo anaweza kuanguka mara nyingi lakini mwisho atasimama na hatimaye akaanza kutembea naam mwisho kabisa akakimbia na hapo furaha mzazi uongezeka.

Ni majira tu yakifika tu ni viungo vyenyewe vinampa msuko wa kufanya jambo sawa na hatua aliyonayo hata kama yeye ayuko tayari viungo vitamsukuma.

Ujue mtoto anapoanza kutembea uwa hana reference/ pa kufuata bali yeye ufanya kile anachokiona na uwa hana wazo nitadondoka na kuumia japo hali hizo zinaweza kujitokeza/kumpata bali yeye ujisikia raha anapotembea na hata akianguka bado haimkatishi tamaa ya kusimama tena na kukimbia.

Naam unapotaka kuisimamia ndoto yako lazima ujiangalia ndani yako na sio nje yako bali ujue wewe ndio mwenye dhamana ya maisha yako na wala sio mtu mwingine.

Ni muhimu kutambua hali uliyonayo sasa ( nguvu ) sio hali hiyo utakayo kuwa nayo kesho ( uzee ) lazima uandae kesho yako kuwa na kicheko kuliko leo usije ukasema” Ningelijua Ningelifanya”

Kumbuka wanaosema umechelewa au hautaweza ndio watu hao hao watakaokusifia  utakapofikia kwenye kilele chako, ukiishi katika maneno yao hauwezi kuiona nuru yako ya kesho.

Unapoufurahia mchana lazima ujiandae kwa usiku ili uendelee kufurahia maana huo ndio ukamilifu wa siku.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cotrhey  Nelson………………………………………………………….0764 018535

Ijumaa, 10 Juni 2022

USILIE! ANAJIVUNIA WEWE

 



 

Ni kawaida ya binadamu kuwa kila jambo analolifanya uwa nyuma yake linakuwa na sababu yake, pindi unapomuona mtu anacheka uwa anakuwa na sababu ya kucheka vilevile pindi unapomuona mtu analia uwa anakuwa na sababu ya kulia japo sio lazima uelewe kama anavyoelewa yeye maana ni kama maumivu ayapatayo mtu anayetumbuliwa jipu na sio anayetumbua jipu.

Unaweza kukuta mtu analia na ikatokea ukajua sababu yake ya kulia, pindi unapojua \unaweza kushindwa kujua uzito wa kumpeleka mtu kuwa katika hali hiyo lakini ukweli moyo ni kificho, maumivu ya mtu anayajua mtu mwenyewe na zaidi sana kile unachokiona ni sehemu ndogo katika kile kinachomfanya alie.

Japo linapotokea unaweza usijue kwanini limetokea, muda mwingi tunaona kama uonevu na wala sio majigambo ya Mungu katika uwanda wake!

Muda mwingine inakuwa ni maamuzi yaliyofanyika katika ulimwengu wa roho ila matokeo yanaonekana katika ulimwengu wa mwili.

Ni muhimu unapopita katika kipindi kigumu ni sawa na mwanafunzi akiwa katika chumba cha mtihani jicho la msimamizi likiwa juu yake………ni zaidi pindi unapopita katika kipindi kigumu uwa mbingu inatulia kukuangalia kuona misuli yako ya rohoni kiwango chako! Ni sawa bondia aliye ulingoni wakati anaendelea na pambano anaweza sema sasa naweza/ninasababu  ya kuinua mikono lakini zinaweza kuja nguvu akiwa katika maumivu ya mwili na akipata fursa na hatimaye akatangazwa kuwa ni bingwa.

Wakati Mungu anajivunia wewe ni wazi maumivu yanaweza kuandamana na wewe!

“ Tazama mwanakondoo azichukue dhambi za ulimwengu”

Ni maneno mazuri lakini yaliyobeba dimbwi la mateso ili liweze kutimia ni lazima jasho la damu liwe limeshatoka.

Ili Mungu aendelee kujivunia ni muhimu tu, uweze kuruhusu afanye apendavyo na sio utakavyo yaani na uwe wewe kwa uhalisia wako, na sio mtu anaishi katika maisha ya wengine bali ishi katika wewe ( ishi maisha yako).

Watu wengi wanapopita katika kipindi kigumu uwa awapendi kuonyesha wanapitia kipindi hicho hivyo kuishi sio maisha yao(japo sio muhimu watu wajue kuliko Mungu anavyopaswa kujua), kucheka wakati ndani analia, kwani kipindi hiki watu wengi awapendi wajue yale wanayo yapitia watu wasije wakawadharau katika hali hiyo utazidisha kipindi kigumu kiwe zaidi kuliko kinavyotakiwa ni sawa na mwanafunzi anapofanya mtihani na kushindwa/kupata matokeo sio mazuri itamlazimu arudie  huo mtihani mpaka atakapo faulu au amue kuacha shule.

Ni muhimu kukubali watu wakuone vile ulivyo ili neema inapokujilia wajue sasa Mungu amekuinua na wala sio jitihada zako.

Hivyo unapokuwa chini wacha ieleweke hivyo labda Mungu mwenyewe aamue kukufunika tu lakini sio wewe ujifunike.

Na pia ni muhimu utambue kila kipindi ambacho unapitia kina maana kubwa katika ustawi wako pia lipo kusudi jema ambalo Mungu analo katika hilo, hivyo ondoa mashaka.

Na utambue kuwa ni Mungu pekee mwenye uchungu wa kweli kuliko mtu/kitu chochote katika maisha yako hivyo anavyoruhusu haya yaje kwako hana lengo la kukuweka katika hatari ambayo haina utatuzi wa kukutoa hapo salama kama aliweza kukutunza tumboni mwa mama yako japo kipindi hicho mimba nyingi ziliharibika lakini wewe ulikuwa salama maana hakuna mtu mwingine awezaye kukutunza unapokuwa tumboni hivyo awezi kushindwa kukutunza sasa.

Uwa wazo jema la Mungu kwa mtu wake aliwezi badilika ila mtu husika anaweza badilika lakini sio ahadi ya Mungu. AKISEMA ANAISIMAMIA MWENYEWE!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………..……0764 018535