Ijumaa, 26 Agosti 2022

ILIKUWA NI LAZIMA YAKATWE ILI UWEZE KUSTAWI

 



Ayubu 14:7 Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake hayatakoma.

Naam ni kawaida ili kutengeneza muonekano mzuri wa bustani wakati mwingine uweza kupitia hatua ya kukatwa au kupunguzwa kwa majani sawa na ramani mtengenezaji bustani na hata kupelekea sio kuvutia  tu bali na kupendeza pia.

Naam karibu sana!

Kuna baadhi ya mambo inabidi yaondolewe haijalishi unayapenda/kuyatazamia au vinginevyo itakuwa kikwazo kwako katika kuona mkono wa Mungu ukikustawisha.

Gideoni, mtihani katika kupunguza wanajeshi wa kwenda nao vitani.

Waamuzi 7:2 Bwana akamwambia Gideoni, Watu hawa walio pamoja nawe ni wengi mno hata nikawatie Wamidiani katika mikono yao, wasije Israeli wakajivuna juu yangu wakisema, Mkono wangu mwenyewe ndio ulioniokoa.

 3 Basi sasa enda, tangaza habari masikioni mwa watu hawa, na kusema, Mtu awaye yote anayeogopa na kutetemeka, na arudi aondoke katika mlima wa Gileadi. Ndipo watu ishirini na mbili elfu wakarudi katika watu hao, wakabaki watu elfu kumi.

 4 Bwana akamwambia Gideoni; Hata sasa watu hawa ni wengi mno; uwalete chini majini, nami nitawajaribu huko kwa ajili yako; kisha itakuwa ya kwamba yule nitakayekuambia, Huyu atakwenda pamoja nawe, ndiye atakayekwenda pamoja nawe; na mtu yule nitakayekuambia, Huyu hatakwenda pamoja nawe, basi mtu huyo hatakwenda.

 5 Basi akawaleta watu chini majini. Bwana akamwambia Gideoni, Kila mtu atakayeyaramba maji kwa ulimi wake, kama vile arambavyo mbwa, huyo utamweka kando; kadhalika kila mtu apigaye magoti kunywa.

 6 Na hesabu ya hao waliokunywa kwa kuramba-ramba, wakipeleka mkono kinywani, ilikuwa watu mia tatu; bali watu wengine wote walipiga magoti kunywa maji.

 7 Bwana akamwambia Gideoni, Kwa watu hawa mia tatu walioyaramba maji nitawaokoa, nami nitawatia Wamidiani katika mikono yako; lakini watu hawa wote wengine na waende zao, kila mtu mahali pake.

 

Gideoni alishajiamini kuwa yeye mwenyewe akienda na wanajeshi hao wote atapata ushindi lakini Mungu akuona hivyo bali Mungu aliona ni wengi sana ila wakibaki wachache wangetosha kupata ushindi na kumpa utukufu.

Kuna mambo yasipokatwa yakiendelea kuwepo wakati mwingine baada ya kukusaidia yanaweza kukuzidi sana na hatimaye kukuangamiza au kukufunika au kukuzamisha.

Naam wakati mwingine matawi yasipoweza kukatwa ungeyategemea/kuyatazamia hayo kuliko Mungu; na wakati mwingine ungeweza bweteka au kulizika.

Naam tukija katika uhalisia wa neno lenyewe “ KUKATWA”  ni neno lisilovutia macho yako, mathalani mtu anapoamua kugombea nafasi mbalimbali katika chama au kampuni ila pindi anaposikia jina lake limekatwa uwa anajisikia vibaya sana na pengine ataanza kulaumu mtu au kuhisi watu waliosababisha, kwasababu wanamuonea kijicho!

Bila shaka hata mti ungeweza kupewa fursa kusema kitu pindi unapokatwa matawi yake bila shaka ni maumivu makali ndani yake na pengine hata kupelekea kufa kwake kama usipokuwa mwangalifu katika ukataji.

Naam katika upande mwingine, katika maisha ya kawaida ya kibinadamu upenda kuwa na vyanzo vingi vya mapato yake ili viweze kurahisisha maisha yake ya kila siku hivyo tunahitaji kuwa na mikono mingi au matawi.

Naam hapo mikono yake inapoanza kukatwa au kufa bila shaka moyo wa mtu upatwa na maswali yenye majibu na mengine yasiyo na majibu.

Uwa mawazo yake yanaweza mpelekea wakati mgumu wa kumudu majukumu yake huku akiangalia vyanzo vya vipato vyake vinazidi kupungua.

Bila shaka mtu mwenye akili anapoona vyanzo vyake vya kipato vinapungua uweza kutumia nguvu zake na uweza wake kupambana ili kuhakikisha ashuki pale alipokua hata ikibidi kwenda kwenye vyombo vya sheria ili kuhakikisha anavitunza vyanzo vya vipato vyake.

Kwa uhakika watu upenda kuwa na vyanzo vya kipato imara ili atapoingia hatua ya uzee asije akawa mtu wa majuta na kujilaumu namna ujana wake alivyoutumia hama kuwa kero kwa jamii inayomzunguka.

Ni wazi kuna hatua nyingine ili uweze kuingia kuna vitu vinabidi vikatwe au viweze kupungua ili viweze kukupa nafasi au uweze kuwa na sifa ya kuingia katika hatua nyingine.

Nikubaliane kuwa wakati mwingi vitu vinavyokatwa uwa vinakuwa haviko katika maandalizi ya kukatwa au katika jambo hilo hivyo yanapotokea mtu aliyekatwa  mtu uweza kuwa katika hali mbaya na hata kufikiria maamuzi ambayo ajawai kuwaza awali, mathalani mtu aliyekopa fedha bank ili aweze kuinua vitega uchumi vyake na inapotokea akashindwa kurudisha fedha hizo banki na banki ikafika hatua ya kumfirisi mali zake hapo anaweza kuona ndoto zake zimefika mwisho.

Naam kama binadamu sisi tunaona kile kinachoonekana lakini sio kisichoonekana , niseme tu wakati mwingi unapoona vitu vyako vinakatwa ujue hapo ndipo mwisho wa sura ya kwanza ( chapter 1 ) utakiwi kuwa na mshtuko wala kuwa na jazba na hata kukata tamaa bali hayo yawe ni maandalizi ya kuingia sura ya pili ( chapter 2 ) kuna vitu vinabidi vikatwe maana havina sifa ya kuingia sura ya pili ya maisha yako.

Unapaswa kujua kila sura ina mambo yake hivyo sura ya kwanza haiwezi kufanana kabisa sura ya pili bali wewe tulia ili unapoingia sura ya pili kuna mfumo mwingine ukiuelewa huo mfumo utafurahi maisha yako.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………………..0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni