Ijumaa, 12 Agosti 2022

NI KWELI NI KITU KIZURI LAKINI SIO KILA KITU;

 



Mme/mke, pesa, nyumba au gari ni kitu kizuri lakini sio kila kitu kwako!

Katika maisha ya kila siku kama binadamu uwaza na kuwazua na pengine hayo mawazo yaka mpelekea kufanya bidii ili akizi uhitaji wake kama sio jambo la ndoto yake.

Maana kuwa na kitu kizuri kitamfanya awe salama katika moyo wake na kupandisha thamani yake katika jamii inayomzungumka.

Japo ni kweli ukikosa hivyo vitu uwezi kufa ingawa vinaweza kukupelekea kwenye umauti endapo vitazidi uwezo wa ufahamu wako.

Ni kweli ukivipata hivi vitu utakuwa na amani na endapo utakosa hivi vitu amani yako itatoweka?

Kwa mtu mwenye akili uwa anajiandaa sana na kuwa na msimamo imara kujenga ya msingi katika kufanya maisha yake kuwa bora.

Ni kweli unaweza kuwa na kitu kizuri lakini kisipowekwa sehemu sahihi kina kosa kazi hivyo kina kosa maana, mathalani unaweza kuwa na mke mzuri sana kimuonekano na hata uelewa mzuri wa maisha na bidii katika kufanikisha mambo katika familia yake lakini pindi ukaamua kumpa nafasi ya kuwa bibi yako badala ya kuwa mke wako hapo hautaweza kuona maana ya kuwa na huyo mke na hawezi kufungua hazina zilizositirika ndani yake.

Ni jambo lililokuwa la kawaida mtu anapoona mambo yake yakienda vizuri uweza kustarehe na kuona sasa amefika kileleni mwa maisha pasipo kujua unapokuwa na kitu sahihi unahitaji kukiweka katika mazingira sahihi na salama ili uendelee kuona huo uzuri wake.

Na pindi unapojiachia/kujisahau kuna hali inaweza kuingia kati yenu na kupoteza sukari/asali na kuwa chungu au shubiri.

Ndo maana mwanzo mwa kitu au kwa kukiangalia unaweza kuona ni kitu kizuri na tena kitakufaa sana katika maisha yako lakini usipo kuwa makini unaweza kuona ule uzuri na ufanisi unaanza kupotea na kuanza kuona /kupelekea kuwa kuona ni wa kawaida pengine kumchukia kama si kumchoka.

Napia hali ya kumchukia au kutopenda tena inakuja pale unapoanza kukitumia pindi unapoona mapungufu yake japo mwanzo ulikuwa uyaoni maana yalikuwa yamefunikwa nguvu ya penzi au alikuwa  msikivu na inapotokea kuwa tofauti inaweza kukupelekea hata kujuta.

Naam mathalani ulikuwa na ndoto ya kuwa na gari la aina fulani lakini pindi ukalipata na kuanza kulitumia mara muda si mrefu ukaanza kushindwa kulihudumia hapo sasa bila shaka utaona mzigo wa kuwa na gari la ndoto yako baada ya kuona fahari yake.

Pia unaweza kujenga nyumba ya ndoto yako na kila mtu akaitamani na pengine hata ukafanya sherehe ndogo ya ufunguzi wa nyumba lakini kumbe eneo hilo ulilolijenga sio sehemu sahihi sana na hatimaye siku si nyingi mvua ikanyesha na kuiharibu hiyo nyumba ya kifahari hapo shaka na majuto yanaweza kuwa ni maisha yako endapo akili yako itafika mwisho.

Naam unaweza kuwa na ndoto ya udhamivu( kiwango cha elimu ) na baada ukapata neema ya kuipata hiyo hatua bila shaka kuna maisha ulitegemea utaishi lakini ukisha pata hiyo shahada ya udhamivu lakini maisha yakawa hayana tofauti na mwanzo au vile ulivyotegemea utakuwa katika mazingira gani?

Bila shaka kuwa na kitu ulichokusudia kwa muda mrefu pindi unapo kipata basi hapo ujue kuna maisha mengine uishi ili uweze kukifurahia na kukitumia pasipo kuchoka.

Naam unapokitafuta kitu unakua na mikakati ya kukipata hivyo unavyokipata basi hapo ni upande mwingine katika kujua mwenendo wake au tabia ya kitu hicho iliuweze kukimudu na sio kikusumbue.

Unaposwa kila kitu unachokipata kuna mabadiliko yake hivyo usipo jiandaa na mabadiliko yake basi ujajiandaa kuwa nacho.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na :

Cothey  Nelson……………………………………………………………..0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni