Ijumaa, 21 Oktoba 2022

NDANI YA UWEPO WAKE!

 



Kila kitu  kinakuwa ni rahisi kukipata endapo ukijua kinapatikana wapi na namna ya kukipata! Endapo utakosea wapi pa kuvipata ni ngumu kuvipata, mathalani mtu mwenye akili akihitaji kumuona mamba awezi kwenda baharini na kutegemea kumuona mamba maana mamba apatikani baharini.

Pia unaweza kuta hiyo bidhaa inapatikana maeneo yanafanana lakini unaweza kukuta wote wanaweza kuuza bidhaa moja lakini inaweza kutofautiana katika ubora na hata baadhi ya bidhaa ikajulikana ni original na fake, hivyo dhana ya kupatikana pekee yake sio jibu kamili bali ubora wa hiyo bidha inaweza kuchochea katika kukamilisha maana ya upatikanaji wake maana inakuwa na tija katika matumizi yake hata kwa upande wa afya.

Karibu katika somo;

Ndani ya uwepo wa Mungu uwa kuna vitu vinazaliwa hapo:

Ø  Ushindi unatokana na uwepo wake

Ø  Nguvu inayotokana katika uwepo wake

Ø  Amani inayotokana na uwepo wake.

Ø  Ujasiri unatokana na uwepo wake

Naam yako machipuo yanatokana ndani ya uwepo wa Mungu, japo yako machipuo yanayotokana nje ya uwepo wa Mungu kufanana au hata kupelekea kutojua utofauti wake.

Ni kweli kuna uwezekano wa kuzaliwa kwa ujasiri ulio nje ya uwepo wa Mungu lakini ukweli ujasiri wowote ulio nje ya uwepo wake sio wa kudumu na ndani yake furaha ya kweli inakuwa haipo.

Unaweza kukuta mtu anajenga nyumba ya kifahari sana hama kupata kazi ambayo wewe binafsi ukiisikia unaweza kutetemeka na hata kushindwa kuamini lakini pindi hivyo vitu vikizaliwa nje ya uwepo wa Mungu bila shaka ukamilifu wa furaha ya kweli hautakuwepo.

Kwa asilimia kubwa watu wengi wanapenda kuwa na vitu vitakavyowapa furaha hata pasipo kujali hivyo vitu nitavipata nikiwa ndani ya uwepo wa Mungu au nje ya uwepo wake bali yeye furaha yake ni kuvipata tu.

Vitu vingine utakavyo vipata nje ya uwepo wa Mungu muda mwingi vinaweza visiambatane na njia iliyo sawa/sahihi hivyo ujasiri na kujiamini sio uhakika sana.

Kuwa na vitu vyenye viwango vya juu ( standard ) kwa mtu aliye ndani ya Mungu ni haki yako na wala sio vinyonge na vizuri ujue kuwa Mungu ni kama baba mwenye busara hata akiwa anamiliki/utajiri kiasi gani hata kuwa na fahari nyingi nyumba na magari ya kutosha hawezi  kumpa mtoto wake ambaye akili yake haijakomaa kumiliki nyumba akampa akae peke yake hata kama anampenda kiasi gani; kwakuwa anajua hapo sio kumsaidia bali kumwangamiza.

Ni kweli ndani ya uwepo wake viko vitu vyenye viwango: mathalani mfalme Daudi alikuwa analalia kitanda kilicho na dhahabu tupu; ila kikubwa lazima ujue akupi ufanya tambo katika jamii yako bali watu wamuone Mungu kupitia maisha yako.

Uwepo wake unatoa vyake endapo utaamua kutulia na kusubiri utoe matunda yake yatakayo dumu siku zote.

Naam kama kweli wewe ni mkristo na unatambua nafasi ya Mungu basi hakikisha unakuwa ndani ya uwepo wake ili naye akupe hazina yake.

“ uso wangu utaenda pamoja nawe nami nitakupa raha “

kutoka 33:14 Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.

Ni kusudi la Mungu endapo utakubali kuishi katika maongozi yake atakupa raha yake, yeye awezi kuviachilia vitu anajua vitaleta uharibifu katika maisha yako.

Tunajua thamani katika dunia ya leo inapimwa kile unachokimiliki, hivyo kiwango cha mali unazo miliki ndivyo thamani utakayopata kutokana watu walioibeba dunia hivyo itakavyokuwa humiliki mali yoyote basi usitegemee heshima yoyote.

Ni kweli kila mtu anatakiwa aheshimike lakini uwezi kulazimisha watu wakuheshimu na pia usilazimishe kuwa na mali ili upate heshima inayozaliwa na mali na heshima ya mali haina nguvu sana kama kumuheshimu mtu katika UTU, kwakuwa mali zinaweza kuja na kupotea.

Usipende kufanana na maisha ya wengi kuwa thamani yao ubebwa na vitu wanavyoviona anafahari nyingi bali muheshimu na kumthamini vile alivyo lakini sio kutokana na mali zake.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………………..…….0764 018535

Alhamisi, 6 Oktoba 2022

KUJUA KUNA GHARAMA

 



 Akiona hazina kwenye shamba………..akaenda kuuza alivyonavyo ili anunue shamba!

Mathayo 13:44 Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.

Pindi unapofanya kitu ambacho  kinajulikana kwa watu wengi watu hawawezi kukushangaa sana mathalani unapopeba gunia la mahindi kwa ajili ya kwenda kupanda shambani watu awatashangaa bali watakuona mtu mwenye akili lakini pindi ikatokea unaenda supermarket na jembe lililoshikama na udongo bila shaka ukinusulika kusimamishwa na askari basi unaweza kusababisha mtafaruku kwa wateja waliopo hapo.

Naam shida ni pale wewe utaona lulu iliyojificha na watu hawaoni kile unachokiona pindi utakapo jibidisha kufanya kitu au kuingia gharama ili uweze kupata kitu ambacho wengine awakioni tegemea kutopewa ushirikiano pia ni wewe ulio na jukumu hilo hivyo likamilishe kwa gharama yoyote maana ni wewe umeona hiyo lulu.

Maana kile unachokiona wewe ambacho wengine awakioni au kuona kuwa ni kitu cha maana sahau kutiwa moyo ( maana hawaoni thamani ambayo wewe unaiona )

Unahitaji kujua zaidi kuhusu hiyo lulu/hazina unayoitafuta ili uweze kuimili kishindo cha kupingwa sio na watu tu bali hata historia inaweza kukuhukumu.

Nuhu alijenga safina huku yeye akiamini sauti ya Mungu kuwa kutakuwa na gharika hivyo ili aweze kuwa salama ni kutengeneza safina , ila pindi alipoanza kujenga na hata kumaliza lakini watu awakumuelewa ila walimwelewa pale gharika ilipotokea.

Kujua kuna raha pia kuna mateso, raha ni pale utakapofanya utajisikia vizuri haijalishi kinalipa au akilipi kwa wakati huo na mateso ni pale utakapo pata upinzani kwa watu unaowaamini na kuwa tegemea kuwa upande wako wakawa kinyume nawe kwa vile unapofanya na kukosa mwitikio mfano.mwimbaji unapoimba imba hovyo hovyo kila mahala wataona ni kero.

Kutokujua kuna ondoa gharama hama kujigharimu kwani unaweza kushika dhahabu na ukaiona jiwe unaweza kulitupa na ukawa na amani tu pasipo kujua kile ulichokitupa kina thamani gani?

Pindi inapotokea kuwa wewe tu ndio unajua kwanini unafanya hivi na kitakuweka wapi kesho! Usipo kaza katika kufanya unaweza kujikuta unajitenga na baraka zako, ukaenda katika mwelekeo tofauti na uliokusudiwa pindi utakaposhtuka unaweza kuona umechelewa/unamwendo mrefu hadi kurudi kule katika njia yako.

Unapojua kitu cha kufanya ambacho wengine awakioni usitake kutumia nguvu sana ili waelewe kama wewe unavyoelewa, ukifanya hivyo utapoteza muda na nguvu zako, kwani mchungwa unapoanza kuota unaweza usielewe au ukaufananisha na miti mingine lakini utauelewa au utaanza kupata uhakika pale utakapoona machungwa yakianza kuchomoza hapo maswali yote yatakuwa yanajijibu yenyewe tena kwa ufasaha zaidi.

Unahitaji kutia bidii katika kile unachokijua NO MATTER WHAT! Kama mkulima anapolima kwa bidii uku ukijua mara baada ya kulima kuna mavuno atakayoyapata ambayo yata mnufaisha yeye na jamii yake uona hivyo tu na hali hiyo umfanya awe na bidii na hata akichoka anajitia nguvu kwakuwa anajua kuna jamii inamtegemea na ndo mana maneno yoyote yakumvunja moyo hayatapata nafasi ndani yake bali yeye uishi kwa kile anachokiamini kwani anajua kama akiishi katika maneno hayo ya watu anaweza akajikuta ana kufa njaa.

Uzuri na umaana wa wewe kujua unakuja pale utapojua hiyo gharama  na kuipenda kuibeba au kuikubali na kuikabili maana hapo ndipo itakapotimia dhana ya kuwa huyu anajua anachokifanya , ni kama mwanafunzi mwenye ndoto kubwa mbele yake ni lazima atajibadisha kusoma sana pasipo kuchoka huku akijua bidii yake sio bure.

Ni kawaida tu mjenzi anapotaka kujenga lazima aka echini na kujua kwanza gharama yake kasha ndipo hapo atatoa maamuzi ya kujenga au kusubiri.

Luka 14:28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?

              29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,

              30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.

Unapojua usiogope gharama maana gharama zipo ili kuthibitisha kujua kwako.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………….0764 018535