Ijumaa, 14 Aprili 2023

KUNA MTU ANAHITAJI UWEPO WAKO!

 



Hakuna kitu kizuri kuwepo au kwenda mahali ambapo unajua unahitajika haijalishi kama kuna kitu unatoa au hautoi bali wewe kujua kuwa “ WEWE NI HITAJI” sehemu hiyo hapo unakuwa na fahari isiyoweza kuelezeka.

Moja ya sababu inayoweza mfanya mtu kuto kwenda kwenye shughuli mbalimbali ni pale asipoona ulazima wake wa kuwepo pale, japo wakati mwingine unaweza kujidanganya kuwa wewe sio wa lazima mahala pale kutokana na mawazo yako au kundi la watu wachache inawezekana sio kweli.

Na moja ya kitu kinachoweza kisizingatiwe wakati unajiandaa kwenda mahali ambapo huna ulazima wa kuwepo hapo ni kisaikolojia na hata mavazi, kwakuwa unajua hata nikiingia gharama kiasi gani katika kujiandaa au kujitengeneza sitaweza badili mtazamo wao mbaya juu yangu.

Na hakuna sehemu inayotia uvivu kwenda kama mahali ambapo unajua hauhitajiki ila umekaribishwa bila shaka hata ukifika mahali hapo ukikaa dakika kumi (10) unaweza hisi kama umekaa masaa kumi na mbili (12) maana kwa muda huo unakuwa umeshaboreka vya kutosha, kila kitu kinachoendelea wewe unaona ni kero ni bora mle tu shughuli iishe.

Ni wazi kutambua kutohitajika katika mahali fulani basi sio kwamba dunia yote haikuhitaji:

-          Mtazamo mbaya usiharibu furaha ya kudumu katika moyo wako.

Ni kweli mwanga unaweza usihitajike sana mchana lakini usiku utahitajika tena hakuta kuwa na mbadala wake.

Naam chakula kinaweza kisihitajiki kwa muda wote hasa wakati umeshiba lakini wakati njaa imeanza kusumbua mwili wako utaanza kukitafuta chakula mahala popote kilipo.

Pia unapokuwa hunakiu ya maji pindi utakapo yaona maji unaweza kuyapiga mateke lakini pindi mwili wako utakapozalisha kiu ni wazi utatafuta maji wapi yalipo ili kukidhi mahitaji ya mwili wako.

Ningependa kuongelea “ Maji” kama kitu muhimu kwa maisha ya mwanadamu na viumbe hai vyote ulimwenguni,

Ni kweli bahari inaweza isihitaji maji lakini sio kweli ardhi yote iko salama haitaji maji bali kuna ardhi iko na ukame mpaka inapasuka kwa kukosa maji na mara nyingine ardhi inapokosa maji inasababisha ukame kutokea na kusababisha njaa katika jamii husika.

Pindi unapoenda mahali ambapo unahitajika, ukiwepo wanaweza kukuita mfalme hata kama hauna watu unaowaongoza, kwakuwa wewe ni utatuzi wa changamoto zao haijalishi kule ulikotoka wanakuitaje? Wakati mwingine kule ulikotoka wanaweza kukuita wewe ni kiraka…………….!

Unahitaji kujua ili mradi umezaliwa na upo mpaka sasa basi ujue wewe hitaji la mahali fulani ni wewe kujivumbua tu, unaweza ukawa utatuzi wa leo au kesho.

Wewe ni zaidi ya mwanga usipohitajika mchana usihofu usiku waja ambao uhitaji wako utakuwa kama lulu kwa kuwa wanakuhitaji ili waweze kuyaona yale wanayotaka.

Yakupasa kujua uwepo wako ni wa faida katika dunia muhimu wewe usijione hasara maana utashindwa kuitumia hile hazina iliyo ndani yako.

Ni kweli unaweza kosa la kufanya ukajikuta unalia tu, ila usiruhusu machozi yakawa maisha yako bali kuna mahali ufike ujitambue na ujue haki yako na ujue wewe upo ili mtu mmoja atoke pale alipo haijalishi wewe uko wapi na pengine hata wewe unamsubiri mtu aje akutoe hapo hapana wewe msubiri Mungu tu ili akutoe nawe uende ukamtoe mtu mwingine. ( unafanyika Baraka kwa mwingine ili Mungu azidi kuwa Baraka kwako)!

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………….………….0764 018535

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni