Katika maisha ya kila mwanadamu tangu kuzaliwa na kukua kwake, ana vitu vyake vya pekee ambavyo havina mfanano na mtu mwingine, hata kama ni mapacha kila mtu atakuwa na umaalum wake, pamoja ni mapacha wewe ukashindwa kuwa tofautisha lakini wao wenyewe wakijiangalia wanaona utofauti wao.
Katika dunia tunayoishi kuna madhira mengi au majanga mengi, japo yapo majanga yanayosababishwa na wanadamu wenyewe hasa katika kuendelea na shughuli zao za kila siku na yako majanga mengine yanasababishwa na asili ya dunia, ( nje ya utashi wa mwanadamu )!
Moja la janga linalochipukia kwa kasi kubwa katika ulimwengu wa sasa ni watu KUTOJIKUBALI vile walivyo na KUJIAMINI au KUJITHAMINI.
Si ajabu kwa sasa kukuta wanawake wanatamani kuwa wanaume na pia wako wanaume wanatamani kuwa wanawake!
Hivyo inaonyesha kwa jinsi gani watu wanakataa kukaa au kuishi kwenye asili yao, mbali na hilo pia kwa sasa hasa mabinti na baadhi ya wanawake wameingia kwenye gharama kubwa ili kutengeneza muonekano wao mathalani kutengeneza kifua (maziwa), makalio kuwa makubwa na wengine kubadili rangi ya ngozi zao inawezekana kwa kujishauri wenyewe tu kutokana na elimu waliyoipata kutoka vyanzo mbalimbali hama kushawishiwa na kampuni au rafiki wa karibu.
Pia kwa upande wa wanaume wako baadhi ya wanaume hivi sasa wanasuka, wanavaa hereni na hata kubadilisha rangi za ngozi zao wengine wakiwa na lengo la kuongeza mvuto au ushawishi! nje ya hapo sijui wanatafuta nini?.
Japo ni muhimu kutambua pindi utakapoishi pasipo kujitengeneza, na kujiongeza hama kujirekebesha kusiko kuwa na tija, basi hapo utafurahia maisha yako na kuwa na uhakika maana unapoishi kama wewe, na ukaongea kama wewe na sio kama mtu mwingine ni wazi hauwezi kujisahau wala kujichoka pia uweza kujiepusha na uharibifu.
Kuna watu wanaogopa kuingia hatua nyingine katika maisha yao kwasababu ya kuona yeye bado hatoshi hivyo ujiweka katika daraja la chini na kuona astahili kuwa mahali fulani au hatua fulani!
Katika upande wa mahusiano ya uchumba hadi ndoa!
Kwa ujumla swala hili la mahusiano ni swala tata katika maisha ya wanadamu wengi kwa kiasi kikubwa limekuwa kama jipu lililoshindikana kutumbuliwa, hususa kwa upande wa vijana wa kiume na hata wakike katika kipindi hiki uhalisia wao upotea kabisa, kipindi mahusiano ya kikolea unaweza hisi mtu uliyenaye kashuka kutoka mbinguni na unaweza fikiri alikuwa karibu na Mungu kana kwamba Mungu anapoanza kusalimia basi anaanza na yeye kisha nakuendelea wengine maana sio kwa upole huo.
Katika kuondoa uhalisia katika swala la mahusiano wako watu wanaenda mbali zaidi wanahazima nguo, gari hata chumba ili ampate mtu fulani au afanikishe lengo lake na pia wako watu kula ugali au mihogo wanahisi kama wanakula sumu wanasema havipandi,
Kuna watu wana jitahidi katika kutengeneza muonekano wao vizuri ni jambo muhimu sana lakini shida inakuwa pale anapotaka kukuaminisha maisha ambayo yeye mwenyewe hayupo hapo, unaweza fikiri huyu mtu anakaa maeneo fulani kwa watu wenye uwezo wao lakini kumbe kwake uhalisi anachumba kimoja na mkeka tu na maeneo yote anamtembeza mpenzi wake ni kwa marafiki zake tu, japo umaridadi unaficha umaskini lakini tuwe wa kweli itatusaidia zaidi.
Mbaya zaidi katika mitandao ya kijamii jinsi inavyotudanya mtu anaedit picha ( anatengeneza picha ) akiwa katika mazingira mbalimbali na anasema ndio maisha yake, unaweza kukuta leo yuko ndani ya ndege na kesho yuko nje na wakati mwingine utakuta yuko mbugani anacheza na simba mbali na hayo unaweza kukuta yuko katika boti mara ameshuka anaogelea na pengine jioni ukakuta anasalimiana na rais wa marekani kumbe ni uongo mtupu.
Unapokuwa wewe na kuishi maisha yako itakusaidia sana na itasaidia kwa kufanikisha kupata kilicho sahihi au kilicho chako ila ukiishi maisha ya mwingine kitakuja kitu cha mwingine ambacho hautadumu nacho na baadae kitazidisha maumivu tu na kujiona Mungu amekuweka katika fungu baya.
Usitake kufanana na yule au hawa kuwa wewe hasa katika eneo la uchumi kama biashara yako ni kuuza karanga usitake tujue kuwa wewe unauza magari au ndege utaingia kwenye mtego ambao baadae utakugharimu sana.
Uongo unaua mahusiano mengi sana katika ulimwengu wa sasa!
Ni vizuri kwanza wewe usiwe muongo ili upate mtu asiye muongo hama iwe rahisi kwako kumgundua mtu muongo, ila usitafute mkweli wakati wewe ni muongo utamuharibu mtoto wa watu.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni