Ijumaa, 29 Desemba 2023

UKISASA UNA GHARAMA



Wanasema kizuri kina gharama au kina gharamikiwa!

Inasemekana ukisasa ni mzuri na sikatai ila unagharama yake.

Kwenda na wakati ni jambo jema sana kwakuwa lina mazuri yake mengi lakini vilevile usipouelewa vizuri unaweza kufanyika kuwa teso kwako hata ukawa mtumwa wake badala wewe kufaidika nao.

Mabadiliko katika mambo mengi uwa ni jambo la heri, kwa maana kwa kiasi kikubwa mabadiliko mengi uchochea maendeleo kwa jamii au taifa kwa ujumla wake.

Tatizo linakuja katika jamii tuliyo nayo, ni jamii kubwa imekuwa ikiteseka sana na ukisasa tulionao kuliko kufaidika nao watu upenda kujaribu kila kitu hatimaye kupelekea matatizo mengi; katika upande wa afya, watu wamekuwa wakitengeneza miili yao au kutumia vitu hata kwa namna ambayo haiongezi tija kwao zaidi ya matokeo yake kudhoofisha afya zao mathalani watu wengine uona fahari kuvuta sigara muda wote lakini mwisho wake uweza kusababisha kansa ya mapafu na magonjwa mengine mengi.

Naam watu wengine wametumia ukisasa katika kuharibu jamii badala ya kuwa saidia: mathalani sasa tunaongezeko la mashoga, watu kujiunga na makundi mabaya ( kigaidi, ujangiri n,k), watu kutekwa hasa watoto na wanawake.

Ukisasa umetoa njia rahisi ya kuwafikia watu hao na kufanikisha matendo yasiyofaa kufanyika katika jamii zao.

Na watu wengi kuingia uingia katika ulimbukeni katika mitandao na kukuta wanatumia muda mwingi katika mitandao kuliko shughuli zao au watu wawapendao/wanaowategemea familia na watu wengine.

Viko vitu vingi vipya vinavyotambulishwa katika ulimwengu wa sasa kila siku baadhi yao vikiwa na lengo la kuwa na msaada katika jamii husika ziko dawa zimekuwa zikisemekana zina nguvu ya kuongeza nguvu ya kiume na kwasasa soko lake limekuwa kubwa pia yako madawa mengine yanasemekana yanaweza kupunguza unene/matumbo, miguu na hata maziwa kuwa makubwa na hivyo jamii imejiingiza katika maisha hayo wakiamini ukisasa unalipa,

Na hali hiyo kupelekea kuharibiwa zaidi kuliko kusaidika! Wakati mwingine mtu anagundua kuwa alikosea akiwa katika madhara makubwa, na wakati mwingine inakuwa ni ngumu kutoka hapo.

Na kutokana na ulimbukeni wa wengi imepelekea watu wengi kuamini hata taarifa zisizo kuwa sahihi au za kweli na baadhi ya watu wamepoteza maisha yao kwa kuamini taarifa zisizo sahihi na kuacha pengo katika jamii au familia husika.

Ukweli ukisasa ni kitu kizuri hata kupelekea mambo yote kupatikana  kwa urahisi hasa yale yaliyo ya kweli na kusaidia jamii husika, wako watu wamejifunza mambo mbalimbali mitandaoni na kuwa na matokeo chanya mathalani mkimbiaji mmoja toka aliweza kujifunza namna ya kurusha mkuki kwa kasi kupitia mtandao na hatimaye hata kupelekea kuiletea medali ya dhahabu nchi yake kutokana na ushindi alioupata kutokana na mashindano hayo.

Na wengine imepelekea kujifunza mambo mbalimbali na kufaidika na maarifa wanayoyapata kutokana na mitandao mathalani wako watu wamejifunza namna nzuri ya upishi kupitia mitandao na wengine kupata masomo yao kupitia mitandao na mengine mengi.

Ni kweli kabisa maadamu unaishi katika jamii ya kileo uwezi kujitenga na usasa ambao dunia inaenda nao maana kuna baadhi ya watu wanajiingizia fedha nyingi kupitia mitandao kwa halali kabisa,

Ukisasa ( teknolojia) katika dunia ya sasa uwezi kuukwepa ili uyafikie mambo mengi kwa haraka unahitaji kuwa na maarifa sahihi ya hicho kitu ili kikusaidie kuongeza maarifa kwa yale unayoyajua na hata usiyoyajua ili ikusaidie kufanya jambo lilelile katika ubora zaidi wenye tija kwako na jamii kwa ujumla.

Ukisasa umepelekea familia kusambalatika, ndugu kutoelewana kutokana kupenyeza taarifa zisizo sahihi katika fahamu za watu mathalani itikadi kali na imani potofu hata kusababisha kila mtu aamue vile anavyoona sawa pasipo kujilizisha kwa umakini yeye anaamini na kukiishi kile anachoambiwa.

Mahusiano mengi yamekuwa ya kidumu kwa muda wa kitambo na mengine yamekuwa yakivunjika hata kabla ya ndoa na mengine yamevunja baada ya ndoa kutoka na mmoja au wote kutaka kuenenda kama ukisasa  unavyotaka ufanye mathalani kutaka kufanya mapenzi kinyume na maumbilena mengine mengi.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson………………………………………………………..0764 018535

 

Ijumaa, 8 Desemba 2023

NI LAZIMA UPITE ILI PAWEPO NA NJIA;



Uwa njia inatengenezwa na mtu au watu na wala haijitengenezi yenyewe! Ni lazima awepo mtu na aamue pawepo njia ndipo njia utokea,

Na katika utendaji wa Mungu tunaona kuwa ni tabia ya Mungu kufanya njia pasipo na njia! Kwakuwa uweza wake hauna kikomo/hauzuiliki.

Kutoka 14:10 Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia Bwana.

13 Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.

-          Ni maneno ya musa akiwaambia Israel yakionyesha kuamini neno la Mungu na uweza wake!

Kama binadamu unayeishi katika dunia hii kuna majira unafika unaweza kuona kukumbana na mazingira ambayo sio rafiki/kandamizi unaweza kuona nyuma maadui na mbele bahari ya shamu hapo ni lazima patokee njia ili uweze kupita la sivyo unaweza kuangamia,

Ni kweli watu upenda kupita njia ambayo ipo tayari inatumika pasipo kujua hiyo njia mpaka imekuwa njia kuna mtu ili mgharimu kuifanya ili wengine wafaidike kwa kuitumia, waswahili wanasema “mwanzo ni mgumu”,

Unapopita katika njia ambayo wengine imewagharimu hata ikawepo basi hapo jua nawe unadeni katika kutengeneza njia ili wengine wapite.

Usiogope kuandaa njia kwa ajili ya wengine ili wapite lakini tambua kama na wenzako wangeamua kuogopa wewe leo usingeijua njia unayoipita leo.

Na tambua kupita katika hali ngeni (experirnce) mpya iliyo katika changamoto kwakuwa uwezi kujua hasa matokeo yake yatakuaje! Na hata kama ni jambo ambalo wengine wamepitia na wako salama lakini swali litakuwa kwako ni kweli matokeo aliyoyapata mwingine nawe utayapata au itakuwa tofauti na ikiwa tofauti utakuwa katika hali gani? Mathalani unaweza kuwa muathirika wa ukimwi na ni kweli unaweza kuwa na shuhuda za watu waliopona  ukimwi lakini ikija upande wako ni kweli utapona au utakufa? ( maana tunajua sisi tuna amini lakini muamuzi ni Mungu ).

Ni kweli unapopita mahali akili yako inapo kosa mwanga au matumaini basi machozi hapo yanakuwa ni fungu lako.

Niseme tu inaweza ukalia baada ya kujitambua kuwa umekosa au kupoteza matumaini kwani hata yesu mwenyewe alilia hata akatokwa na machozi ya damu lakini lile chozi alikumfanya ashindwe kukamilisha kusudi lake alilopewa na Mungu hapa duniani.

Tatizo sio kulia bali nikuendelea kulia katika hali ya kukosa muelekeo matumaini tena,

Ni muhimu kuwa na fikra pana na usione katika dunia ni wewe pekee ndio mambo yanakusonga kana kwamba jicho la Mungu liko mashariki nawe uko magharibi kwahiyo Mungu haoni kile kinachoendelea katika maisha yako.

Usilie kwa sababu ya kutoa uchungu moyoni kwani baada ya kulia na kama hali haijabadilika basi hapo kilio kitaendelea pasipo kukoma lakini itakuwa tofauti tu mara tumaini jipya litakapo chipuka ndani yako.

Mruhusu Roho mtakatifu alete mwanga au tumaini katika akili yako iliyo na giza maana ni yeye tu awezaye kuifanya njia nawe ukaiona kisha ukachukua maamuzi ya kupita, na lazima uione kutokea ndani yako! Maana ni yeye anayekuonesha njia ambayo wengine hawawezi kuiona mpaka pale umepita ndipo wengine waione njia wapite kwasababu wewe umepita.

Kuna raha sana baada ya wewe kupita na wengine wakaona njia nao wakaanza kupita unakuwa kama mtu aliyejigharimu kujenga nyumba nzuri japo aliteseka lakini furaha yake inakuwa pale atakapoona watu wengine wanakaa humo na kupafurahia yeye uwa furaha yake inazidi hasa akikumbuka namna alivyokosa usingizi na kujinyima ili akamilishe jambo hilo japo anaweza jua kuwa ile gharama aliyoingia kuna mtu anafurahia.

Ni kama yesu furaha yake uwa inaongezeka japo ili mgharimu kufa na kufufuka, ila anapoona kuna watu wanaokolewa yaani wanaifuata njia ambayo yeye aliitengeneza.

Ni sawa na mama mjamzito uwa furaha yake inakuwa nyingi pindi anapo mpakata mtoto wake katika mikono yake japo inawezekana alipita katika hatua ngumu tangu ujauzito hadi kujifungua!

 

ISHI ILI WENGINE WAISHI!

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

 

Imeandaliwa na:

 

Cothey  Nelson………………………………………………………0764 018535