Moja ya
maisha mazuri unapokuwa hapa duniani ni maisha ya maombi!
Matendo 10:1 Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa
kikosi kilichoitwa Kiitalia,
2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na
nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu
daima.
3 Akaona katika maono waziwazi, kama
saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!
4 Akamtazama sana, akaogopa akasema,
Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa
ukumbusho mbele za Mungu.
Ukijua siri
iliyo katika maombi hauwezi kuwa mtu wa lawama! Huu ulimwengu unakutambulisha
na kupa kuishi katika nafasi yako.
Ayubu 1:1 Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa
akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha
Mungu, na kuepukana na uovu.
2 Kisha walizaliwa kwake wana saba, na
binti watatu.
3 Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo
elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia
tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana
kuliko watu wote wa upande wa mashariki.
4 Nao wanawe huenda na kufanya karamu
katika nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakatuma na kuwaita maumbu
yao watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao.
5 Basi ilikuwa, hapo hizo siku za
karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka
asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote
ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi,
na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote.
-
Kuwa
na mali nyingi hakuondoi nafasi ya wewe kuomba, maana kuomba ndio ustawi wa
yale/ shughuli unayoifanya.
Maombi sio
ghasia au makele! Bali ni tendo linaloonekana katika mwili bali linatafsiri na
nguvu katika ulimwengu wa roho,
Yohana 17:1 Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea
mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako
naye akutukuze wewe;
2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya
wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.
3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue
wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
4 Mimi nimekutukuza duniani, hali
nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.
5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja
nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.
6 Jina lako nimewadhihirishia watu
wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako
wamelishika.
7 Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa
yatoka kwako.
8 Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa
wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya
kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
9 Mimi nawaombea hao; siuombei
ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;
Kama vile
uchoki kumuazia mema kwa mtu unaye mpenda ndivyo hivyo upaswi kuchoka kuomba
kwa kuwa unampenda,
Yakobo 5:16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa
ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake
mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
17 Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua
isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
Mtu unayempenda
unamshirikisha magumu na mazuri unayaopata katika mwenendo wenu wote, maana
unajua atakusikiliza na kukupa mwanga katika yale unayoyaendea.
Isaya 1:18 Haya, njoni, tusemezane,
asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama
theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Wafilipi 4:6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila
neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na
Mungu.
Upaswi
kuanza kuwa serious na kuomba pale unapokutana na mambo kisha ukakosa jibu huo
sio msingi mzuri kuwa endelevu katika maisha yako,
-
Hali
hiyo itapelekea kuto kujua yule unaye muomba na hali hiyo upelekea kuomba
vibaya,
Yakobo 4:3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
Kama hakuna
kitu kinaenda pasipo mazungumzo basi hakuna kitu kinaenda pasipo maombi, na
ndio kitu kimojawapo kinachoweza kufanya kuufurahia wokovu wako,
Yohana 16:24 Hata sasa
hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
Nyumba ya
watu wasiozungumza anguko lake ni kubwa, ndivyo ilivyo wokovu bila maombi
huwezi kushamiri,
Hauhitaji
kusimamiwa ili uombe unahitaji kujua umuhimu/faida za maombi ili uombe:
Unahitaji
kujua umebeba nini ili maombi yawe mazuri, ukibeba hazina njema utaomba vyema
ila ukibeba hazina mbaya utaomba vibaya,
Maombi yana
nguvu pindi utakapojua nini unafanya! Shetani haogopi maneno yako anaogopa
maarifa yako unayo yatumia sio yaliyo kichwani pasipo faida yoyote.
Matendo 19:13 Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo,
wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu,
wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.
14 Walikuwako wana saba wa mtu mmoja
Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo.
15 Yule pepo mchafu akawajibu,
akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani?
16 Na yule mtu aliyepagawa na pepo
mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika
nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.
Ndani ya maombi kunazaliwa:
a) Kunazaliwa njia kutoka pale ulipo:
-
Na
hali hii inakupa amani na utulivu hata kama ujatoka katika mazingira hayo,
-
Mungu
ujifunua katika ulimwengu wa maombi na kukupa mwangaza wako,
Zaburi 16:11 Utanijulisha njia ya uzima;
Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya
milele.
Zaburi 18:30 Mungu, njia yake ni kamilifu,
Ahadi ya Bwana imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia.
b) Kunazaliwa hali ya kuweza au
kushinda,
-
Kuna
kuimarishwa au kutiwa nguvu unapokuwepo katika maombi pale unapoona moyo wako
umezidiwa au kuelemewa.
“ ikiwezekana kikombe hiki kiniepuka “
Luka 22:39 Akatoka akaenda mpaka mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa
desturi yake; wanafunzi wake nao wakafuatana naye.
40 Alipofika mahali pale aliwaambia,
Ombeni kwamba msiingie majaribuni.
41 Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi
cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba,
42 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi
yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.
43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea
akamtia nguvu.
44 Naye kwa vile alivyokuwa katika
dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka
nchini.
c) Hayumbishwi/ kutoyumbishwa
-
Mtu
anayeomba anajua kwanini anafanya hiki na kwa nini afanyi kile, kwa sababu
katika maombi kunazaliwa maongozi,
d) Hauwezi kuchoka/ kutochoka
-
Katika
maombi kuna kuimarishwa katika utu wa nje na utu wa ndani ila hautukuwa katika
hali hii ya uzuri kama tu utaomba vibaya,
Unapokuwa mwana maombi kwa Mungu
inakuwa:
i.
Ni
kitu anachohitaji kusikia
-
Mzazi
mwenye mapenzi na familia yake upenda kusikia sauti za watoto wake anapokuwa
nyumbani, na sio sauti za majirani.
“ njooni tusemezane “
Isaya 1:18 Haya, njoni, tusemezane,
asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama
theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
ii.
Ni
kitu anachotegemea
Yohana 10:27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao
wanifuata.
-
Ashtuki
kusikia sauti yako.
-
Unapoishi
katika himaya yake na haumuombi yeye unampa maswali mzazi kuwa yeye ndio baba
yako au kuna mtu mwingine anakuhudumia: mathalani unasoma secondary wewe umuombi
kitu chochote kwa mzazi, sio nguo za shule, vifaa vya shule au kumkumbusha ada!
Maombi kwa
lugha nyepesi ni mazungumzo/ mawasiliano kati ya wewe na unaye muomba,
-
Hauwezi
kuwa salama nje ya maombi, kwa kuwa kupitia maombi Mungu atajua hitaji lako na
kukupatia,
Hakuna
maombi yenye majibu halisi nje ya kupendwa!
-
Kuna
majibu ya haraka na sahihi zaidi pindi utakapo muomba Mungu anayetambua
unampenda,
Maombi
yasiyobebwa na upendo yanakuwa ni maombi ya msimu namatukio pamoja na mazoea,
Mahali pekee
unatakiwa kuwa na furaha na shauku ni mahali pa maombi maana ni mahali ambapo
unakwenda kuzungumza na unayempenda na sio adui,
-
Kuna
maandalizi ya kuzungumza na adui pia kuna maandalizi ya kuzungumza na upendaye!
-
Mawasiliano
na unayempenda ( maombi ) uongeza pendo: kila mtu anajisikia kwanini leo
sijaongea naye na Mungu anasema leo sijamsikia mwanangu/rafiki.
Ili maombi yawe na matokeo:
i.
Ni
lazima ukiishi kile unachokiomba
-
Usiombe
kitu ambacho ukielewi wala hauna namna ya kukifanya kuishi kupitia hilo ombi,
-
Ni
lazima ukiri wako uhusishe moyo wako, usiongee kitu ambacho umeona wengine
wanaongea tu, pasipo kujua kwa nini huyu anaongea hivi,
Mathayo 6:7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya
kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
ii.
Lazima
ukiamini kile unachokiomba
-
Lazima
imani yako iwe katika kile unachokiomba, na ujue maombi ni tendo la kuamisha
kitu toka katika ulimwengu war oho na kuingiza katika ulimwengu wa mwili,
-
Unahitaji
nguvu na maarifa ili kuyafanya hayo na kuamini,
Marko 11:24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali,
aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu
amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale
wamtafutao.
iii.
Maongozi
ya Roho mtakatifu
-
Huu
ndio msingi wa maombi, bila Roho mtakatifu maombi bado hayajaanza,
-
Hata
kama uliomba kwa miaka 10 ujue bado ujaanza kuomba
-
Maombi
bila ya Roho mtakatifu ni sawa na kumpigia simu mtu huku simu yako imezima,
hakuna muunganiko!
Warumi 8:26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana
hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua
kusikoweza kutamkwa.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson……………………………………………………………0764 018535