Ni kusudi la Mungu usiaibike au aibu isifanye makao kwako.
Wakati mwingine mambo yanapokuwa magumu unatamani kukaa mahali au katika hali ya kujiona kuwa uko salama japo unaweza usiwe sawa..
Watu wengi hawatamani kujificha tu au kuji hifadhi tu bali wanatamani mahali hapo watakapo jisitiri basi usalama wa kutosha uwepo.
Mahali pa kujisitiri ambapo usalama sio wa kudumu hilo nalo jangwa mahali hapo ulipo bado mabaya yatakupata na kamwe hautajiona au maana ya kujificha au kujisitiri hapo.
Yakupasa ujue maficho ya aina yoyote bado unaweza usiwe salama hata kama utachukua muda wa watu kujua wapi umejificha na namna ya kukufikia lakini tambua ipo siku watakufikia tu,
Mathalani, Osama alijificha mahali ambapo aliamini kuwa yuko salama dhidi ya wa marekani lakini pindi marekani walipotambua pale alipo waliweza kujipanga na kumvamia hatimaye na kuondoa usalama wake au kinga yake na kupelekea kifo chake.
Hivyo ulinzi hauhitaji kujiona uko salama tu, bali uhakikishe huo salama.
Ni Mungu pekee mwenye uwezo wa kukuficha dhidi ya hatari mbaya nawe ukawa salama katika ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili.
Maficho yote yaliyobebwa na watu huwa usalama wake unakuwa sio wa kudumu maana watatokea watu wengine wenye uwezo zaidi yao watayaharibu hivyo maisha yako.
Lakini Yesu alipofichwa na Mungu/Mbingu katika ujio wake wa kuwa kumboa wanadamu alikabaliwa na kifo dhidi ya herode lakini mbingu ilipomficha alikuwa salama na hatimaye akalitimiza lile kusudi alilolijia japo katika vita kali lakini aliibuka mshindi.
Usalama unaozaliwa na Mungu ni mkamilifu kuliko kitu kingine sio watu au ushirikina unao uwezo wa kukupa usalama kudumu.
Ni Mungu kujua wewe unapokuwa wake inakuwa ni sawa na mazazi mwenye akili ambaye hataki kuiona aibu ya mwanaye impate.
Unahitaji wewe kuwa na Mungu ili maficho yake yawe juu yako katika vita dhidi ya huduma yako, uchumi au mahusiano yako yeye atakufanya uwe mshindi na usalama uzidio katika maisha yako.
Unaweza kujikuta umeingia katika mazingira ukaona vita ni kubwa na usione wapi pa kutokea na ukajikuta unamlaumu Mungu kwanini ameruhusu aibu ikupate bila shaka ni muhimu utambue mazingira yapo kukuvunja nguvu dhidi ya Mungu unayemwamini……………..
Daudi hata alipoingizwa katika mazingira magumu ya kupambana na Goliath bado alisimama katika kumwamini Mungu na Mungu akamuonekania,
Hauhitaji watu zaidi ya kumwihitaji MUNGU!
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson ……………………………………………………………………………………0764 018535