Kijana mmoja aliyekuwa anacheza mpira na alikuwa ana ndoto kubwa kutoka kuwa mchezaji wa kitongoji mpaka kuwa wa kimataifa, lakini katika ndoto hiyo alipitia changamoto nyingi kuanzia kwa mwalimu wake na hata wenzake walikuwa wanamvunja moyo mpaka yeye binafsi kuanza kuona kuwa ndoto yake inashindwa kutimia , lakini siku moja majira ya jioni alikuwa anarudi nyumbani baada ya kutoka katika mazoezi ya mpira, akiwa amechoka sana pamoja na kutingwa na mawazo mengi yaliyokosa mwanga na huku moyo wake ulikuwa una dunda kama gari lililokosa mwelekeo na kuanza kuelekea kwenye maporomoko makali………akiwa katika hali hiyo ya giza ghafla akatokea mzee mmoja aliyekuwa akiishi jirani naye na kumwambia neno hili “ kijana uwe imara utashinda “ hilo neno liliingia mifupani, kwenye damu na nyama na hatimaye kufuta giza lililokuwa likitawala kichwa chake! Ni kama kipofu kuona mwanga kwa mara ya kwanza.
Hivyo yule kijana akaanza kutembea katika neno la yule mzee kuliko maneno ya watu wengine waalimu na wachezaji wenzake waliokuwa wakimvunja moyo na hatimaye katika bidii yake siku moja alitimiza ndoto yake na kwenda kucheza katika mataifa mengine sawa na ndoto yake.
- kuna vitu viwili katika maisha ya mtu kuna NDOTO na TAMAA YA MTU BINAFSI, mara nyingi tamaa inaweza isitimie.
Karibu!
Ni muhimu ujue uimara unajengwa ndani ya mtu husika katika kuyakabili mambo yaliyo kinyume naye au yanayo mzunguka.
Unahitaji uimara wa ndani ili kushinda mazingira yote.
- usikubaliane na mazingira vile yanavyosema maana Mungu yuko nje ya mazingira.
2 Wafalme 7:1 Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria.
2 Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.
Ni matamanio ya wengi kuwa katika mazingira yaliyo kuwa shwari maana hapo hisia na vionjo vya mwili hutulia, Lakini sio wakati wote unaweza kuwa na mazingira uyapendayo kuna wakati bahari inachafuka lakini utahitaji kuvuka.
Ndomana hata katika vyombo vya habari pindi bahari inapochafuka huwa wanashauri safari za majini zisitishwe kwa muda mpaka pale hali ya hewa itakapo kuwa shwari.
Kuna wakati mambo yanachafuka/ yanakuwa visivyo au nje ya matarajio yako ama mpangilio kuharibika ili kitu KIPYA KIZALIWE maana kuna vitu vingine haviwezi kudhihirika katika mazingira ya kawaida.
Kuna baadhi ya machafuko/ kutoelewana na mtu wako wa karibu kunatokea sio kwamba mmechokana la hasha! Bali kuna kitu kinazaliwa hapo kitakacho kupeleka wewe katika kuyafurahia maisha yako zaidi lakini pindi usipoelewa unaweza kujikuta katika wimbi la chuki na kisasi kisichokuwa cha lazima.
Kuna mambo mengine ili yatokee kwanza yanakutenganisha na yale mambo uliyo yazoea au unayo yapenda.
² Lutu na Abramu
Mwanzo 13:5 Na Lutu aliyesafiri pamoja na Abramu, yeye naye alikuwa na makundi ya ng'ombe na kondoo, na hema.
6 Na ile nchi haikuwatosha, ili wakae pamoja; maana mali zao zilikuwa nyingi, hata wasiweze kukaa pamoja.
7 Kukawako ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abramu, na wachunga wanyama wa Lutu; na siku zile Wakanaani na Waperizi walikuwa wakikaa katika nchi.
8 Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati ya mimi na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu ndugu.
9 Je! Nchi hii yote haiko mbele yako? Basi ujitenge nami, nakusihi; ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kuume; ukienda upande wa kuume, nitakwenda upande wa kushoto.
10 Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya Bwana, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari.
11 Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao.
Unahitaji kuyakubali mazingira mageni pasipo manung’uniko ili maisha mapya yazaliwe.
Natambua mahali panapokuwa katika machafuko unakuwa kama uko gizani pasipo matumaini ya mwanga unaweza usijue lini utaona mwanga.
² hakuna jaribu lisilo na mlango
1 wakorintho 10:13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
Unahitaji ujasiri tu ili uweze kuruhusu nguvu ya kupindua giza kuwa nuru lasivyo unaweza kujikuta maisha yako yote umeatamia giza.
Yohana 1:5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………………………………0764 018535