Ijumaa, 3 Januari 2025

HATMA YAKO IMEFICHWA NDANI YA MUNGU

 



NENO “ FICHA “ limebeba usiri mwingi sana.

Limejikita katika hali ya ubinafsi zaidi!

Naam Pindi unapo tambua mahali ambapo umeficha hazina yako iko salama na hakuna mtu anaweza kuiona wala kuichukua bila shaka unakuwa na raha isiyo ya kifani ndani na nje yako.

 Mathayo 6:19 Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;

 20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;

 

*     *     *      *       *        *       *           *          *          *           *           *         *          *         *

Maadamu umezaliwa tu basi ujue hatma yako iko ndani ndomana ukapelekea wewe kuzaliwa.

Hatma wakati mwingine uitwa KUSUDI LA WEWE KUWEPO, hivyo maadamu umezaliwa unasababu ya kuzaliwa la sivyo usingezaliwa! Kama taasisi inapohitaji kuongeza mfanyakazi bila shaka kuna kuwa na wajibu pamoja na haki ya mfanya kazi aliyekuwepo na atakayeingia.

- uhitaji wa hiyo taasisi ndio unapelekea sababu ya kuajiri.

Hivyo duniani pasingekuwa na uhitaji wako, Mungu asingeruhusu wewe uzaliwe, hivyo kila mtu ili mradi amezaliwa pasipo kuangalia amezaliwaje basi liko kusudi la kuzaliwa kwake.

Kusudi/ hatma sio swala au jambo la kumuomba Mungu akupe ila kinacho hitajika hapo ni udhihirisho tu maana tayari Mungu amekiungamanisha na maisha yako.

Hivyo sio rahisi mtu kukutenganisha na hatma yako, maana ni Mungu amekiweka kwa kusudi maalum ( special mission ) na hakuna mwanadamu yeyote atayeweza kukiondoa au kukichukua.

Japo, Ni kweli unaweza kuwa na hatma kubwa lakini unaweza kushindwa kudhihirika au kufanyia kazi hivyo ukawa hasara baada ya kuwa faida.

 

 

 

² Mwenye talanta moja

Mathayo 25:24 Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;

 25 basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.

 26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;

 27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.

 28 Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.

 

² mti usiozaa uvumilia

Luka 13:7 Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?

 8 Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi;

 9 nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate.

 

Mungu anahuzunika pindi anapoiweka hatma kubwa ndani yako anapoona hauitumii na wakati mwingine hata hauitambui kama unayo hatma ndani yako.

 Hosea 4:6 Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

 

Mungu anapoweka hatma ndani yako ina maana amekupa ufunguo wa mafanikio yako.

- unaposhindwa kulitumikia kusudi lako basi unajichelewesha katika mafanikio yako.

Maana unapofanya jambo lililoshikamana na hatma yako inakuwa ni sawasawa na maji yanayotoka kwenye kisima kisicho kauka.

Vitu muhimu katika hatma yako ni kuitambua hatma yako iliyo ndani na kujua wakati sahihi wa kuitumikia hiyo hatma na kuhakikisha unaitumikia katika viwango vya hali ya juu.

 

Mng’ao wako uko pale utakapoanza kulitumikia kusudi au hatma.

- unapoipenda hatma yako ina maana maana umejipenda wewe.

Kwa lugha nyepesi tunaozungumzia hatma tunazungumzia kazi za Mungu alizoziweka ndani yakoili uweze kufanya badala yake.

Waefeso 2:10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

Yakupasa kujua haupo kuangalia dunia inavyokwenda bali unamchango katika kubadilisha dunia yako haijalishi ni dogo au kubwa.

Ni hatari sana kuishi ukitamani matokeo ya watu wanaoishi kwenye hatma zao ukafikiri Mungu amewapendelea zaidi yako.

Na wewe ukiishi katika kujitambua utapelekea wengine kuanza kukutamani na kukufanya kuwa wewe ni mfano kwao.

Ili uweze kutembea katika hatma yako katika faida ni lazima kwanza utembee katika Mungu, maana yeye ndiye anayejua kwanini amekuchagua na akaweka hiyo hatma na kwa ajili ya nini?

 

Yakupasa kujua tija yako mbele za Mungu ni pale utakapoamua kuishi kwenye hatma yako kwa msaada wa Roho mtakatifu.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………………………..0764 018535

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni