UPOFU
WA AKILI
Tunakubaliana sote kwa
pamoja kuwa tofauti kubwa ya mwanadamu na mwanadamu na tofauti ya tofauti ya
mwanadamu na wanyama sio Akili tu bali matumizi ya AKILI, hivyo hapa kuna vitu
viwili kuwa na akili na matumizi ya akili na pia katika matumizi ya akili kuna
matumizi sahihi na matumizi yasiyosahihi….matumizi ya akili yanazalisha majina
kama haya mjanja,mjinga,mzembe,mvivu,goigoi,mwelevu na hata kuitwa
usiyejitambua.
Naamini katika maneno
makali ambayo binadamu apendwi kuambiwa ni neno kuwa HUNA AKILI hii ni lugha
yenye ukali yanayoathiri mfumo mzima wa maisha ya mtu katika mwenendo wake
mzima.japo wako watu wanakataa kuambiwa kuwa wanamatumizi mabaya ya akili zao
au kwa lugha rahisi anaitwa mjinga ambalo ni neno lilojaa mauzi kebei na kwa
hakika alivutii katika masikioni mwa mtu.
Ninapozungumzia upofu wa akili sina maana kuwa akili
iliyokosa mwelekeo au akili iliyokosa njia sahihi yanamna kutatua majukumu
yanayo mzunguka,…………..bali hali ya kujua
uaribifu wa maisha yako na kwenda katika njia hiyo pasipo kujali kitakachotokea,
mtu wa namna hii ataashauriwe na mtu wa namna gani? Bali ushikilia kile
alichokiamua/alichokiamini mathalani kuwa katika maamuzi ya kuchukua kuingia
katika UJAMBAZI,UCHAWI na hata UKAHABA, mtu wa namna hii sio kitu rahisi kumtoa
mtu katika maazimio yake hayo labda mpaka aone madhara yake na anaweza kuona
anahitaji msaada na asiupate huo msaada kwani jamii inawakata au inawanyanyapaa
na hata kuwatenga kuishi na watu hawa katika hali ya kujiami.
Sikatai wako watu wanajiingiza
katika mfumo huo usio rasmi wakiwa na mawazo tofauti wako watu watasema mimi
nitafanya kwa muda tu alafu nitaacha na pindi atakapoacha anaamini atakuwa
anaweza kujishughulisha katika shughuli nyingine ambayo itampatia kipato katika
kuendesha maisha yake….lakini katika mawazo hayo ni wachache sana wanao uwezo
kuyatimiza hayo mawzo…zaidi sana wanachokiongea sio kile wanachokifanya
inawezekana katika ushawishi binafsi au ushawishi wa wenzao.
Naamini kama akili yako
ikiwa njema haiwezekani tu ukaingia katika mfumo huo ambao utahatarisha maisha yako
na niseme wazi maamuzi ya jinsi hii aichagui MSOMI au ASIYESOMA au MASIKINI au TAJIRI wote akili zao zinaweza
patwa na upofu wakafanya mambo ambayo yakaongeza giza katika maisha yao badala
ya kuongeza nuru….ni wazi kuwa kazi hii hauwezi fanya milele ila sio rahisi
kutimiza lile lengo ambalo umelipanga kuwa nitatimiza.
Watu wanaofanya
shughuli hizi wengi wanasema wafanya hili sio kwa kupenda bali kunashinikizo
ambalo linamsukumo katika kuyafikia maamuzi hayo inawezakuwa maisha, msuko wa
mwili wake na hata katika mtazamo wake
au ushawishi watu……….tunaamini kunashughuli nzito kamaukiingia sio rahisi sana
kutoka huko mathalani mtumiaji madawa ya kulevya na msambazaji wa madawa ya
kulevya anaweza asitoke kutokana na manufaa anayo yapata au kutokana na
kuathirika katika mwili wake.
Japo ziko taasisi
zilizoazishwa katika kuwasaidia jamii kuondoka na tatizo hili lakini tatizo
limekuwa likupungua tu lakini ukweli tatizo limeendelea kuwepo wakati wote na
jamii imekuwa ikizidi kuathirika na janga hili pasipo kujua nini cha kufanya.
Ushauri wangu kwa watu wa jinsi hii……kwanza nitoe
shukrani zangu kwa kila taasisi ambazo kiukweli zimejitolea kuhakikisha jamii
inaondokana na janga hili na kuwa jamii isiyo na watu wenye akili zilizotiwa
giza ambazo kwa muonekano zimekosa njia sahihi, zimekosa mwelekeo na hata
kukosa kuthamini kesho yao………lakini kubwa katika yote Mungu anaweza kuyafanya
yale ambayo kwa uhalisi yalikuwa ni magumu sana kama mzazi au mlezi na hata
ndugu mwamini yesu katika maisha yako awe dira katika maisha yako yote na yeye
ataleta nuru kwa wale waliofikia hatima mbaya ambayo jamii haiwaelewi tena……na
kwa mtu aliyeathirika katika utendaji niseme sana wewe ni mtu wa maana sana
kwani katika biblia yesu aliwapenda waliokataliwa na jamii husika mathalani wenye ukoma, makahaba na hata
watoza ushuru Mungu ni zaidi ya baba anayejua kulea,kujali na kukupa kile kitu
ambacho hakuna mtu anaweza kukupa mkabidhi yesu maisha yako na kuamua kwenda
kanisani kwa waliokoka na kufundisha neno sahihi la Mungu!
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson………………………….0764 018535