UPANDE
ULIO BEBA USALAMA WAKO
Moja ya vitu vinavyopendwa
na watu wengi ni usalama!
Kwakua katika usalama kuna
utendaji katika uhuru na nafasi ya kufanya jambo lenye ubora wake.tuna fahamu
kuwa moja ya kazi ya vyombo vya ulinzi ni kulinda mipaka ya nchi ( kuhakikisha
usalama wa nchi wakati wote)
Na hichi ndicho kitu ambacho
watu wengi ukitamani sana…..usalama wao pamoja na mali zao, kwakua wanajua
katika usalama basi mambo mengi uwa rahisi kufanyika pasipo na ugumu usiokuwa
na lazima.
►Shida
kubwa moja ya watu wengi wanapenda sana kuwa na usalama lakini namna
wanavyoenenda wanaufukuzia mbali usalama wao na vitu vyao……….sawasawa mtu
anayetumia dawa(dozi) katika hali mbaya lakini bado mtu anatumia kilevi kikali
lakini katika hali hiyo bado anaamini Mungu atamsaidia.
Niseme wazi siku inapande
mbili yaani usiku na mchana……..na hata dunia inapande mbili yaani uliosalama na
usio salama, na hakuna ambaye apendi usalama lakini ugumu uko katika kudhihirisha kuwa wewe unapenda usalama katika
maneno tu au pia katika mfumo mzima wa maisha yako.
Kibinadamu yako mambo
mengine mtu anafanya akiwa ametiwa giza akiamini anaona kumbe haoni sawasawa na
mtu kuamini anajua kumbe ajui! Ndani ya dunia kuna mtindo ukiishi ambao
utaondoa usalama wa maisha yako na kusababisha mambo mengine yazidi kukukabili.
Unahitaji kujua kwamba
binadamu wewe ni sahihi kwamba uhuru ulionao unapaswa usifanane na wanyama
katika utendaji wako na katika kutimiza hisia zako inakupasa ujue kuwa viumbe
vyote vya dunia vinapaswa vijifunze kupitia wewe na sio wewe ujifunze kwao
unaweza kukataa kabisa lakini ukweli ni kwamba mambo mengi tunayoyafanya
yanafanana na wanyama kwa asilimia kubwa mathalani kupigana hadharani na
matendo mengine yanayofanana na hayo.
Kuna maisha ya mengine mtu
anaishi unaona mwisho wake wa maisha yake umebebwa na maumivu, kukataliwa na
hata kutengwa lakini bado mtu anakuwa anakaza mwendo kuendelea, na
ukiwasikiliza wanasababu nyingi wengi wakisema maisha magumu, nilikataliwa na wengine
wanasema nimetendwa vibaya hivyo staili ya maisha haya ndio niliyoichagua hivyo
na ishi maisha haya sio kama napenda bali inanilazimu.
Niseme kwamba kwa namana yoyote
ulivyo, jua yuko mmoja tu ambaye atakupenda vile ulivyo na kutopenda aibu yako
iendelee kwakua kwa yeye ulitoka na kwake utarejea, hivyo niseme wazi katika
maisha yoyote unayoishi bado Mungu aliyenipenda mimi basi anakupenda nawe tena
upendo uleule hakika ni baba mwema.
Niseme maadamu unaishi tu
haijarishi uko katika hali gani nini kimeathiri mwili wako, akili yako na kuona
kuwa umeharibu mstakabali wa maisha yako napenda ujue kuwa bado unayo nafasi
kubwa kwa Mungu aliyekuumba anaweza akainawilisha tena ngozi yako na kuwa zaidi
ya ulivyokuwa jana! Huna haja ya kulia na kusononeka sana bali yuko Mungu
ambaye kwake yeye kila kitu kina nawilishwa na kuzidi kwa bora.
Mungu anasubiri maamuzi yako
tu katika kurejea kwake naye akufanye kuwa mtu wa maana katika viwango vyake.
Mungu awezi kukurahumu wala kukuchoka bali anajua kuwa kwa wewe unaweza kuwa
mtu mwingine kupitia yeye.
Hivyo Mungu anasubiri umpatie
maumivu yako,teso lako na dhihaka yako ili yeye achukue na kukuacha ukiwa huru
mbali na mateso…………maana salama yako ndio furaha yake.
Giza katika dunia japo ni
sehemu ambayo watu wengi upenda kufanya mambo yao kwasababu kuna maficho yao
lakini hawapendi kujua kuwa ndani ya giza kuna upofu uharibifu na mateso
yaliyobebwa na huzuni isiyokoma.
Nuru ya Mungu katika dunia hii………
hapo ni sehemu salama japo watu wengi hawapendi kwenda katika njia hiyo kwani
haina mvuto lakini niseme kwamba katika nuru kuna nguvu na uimara uliobeba
stara ya mwanadamu.
Imeandaliwa
na:
Cothey
Nelson…………………………………………0764 018535