Jumanne, 20 Septemba 2016

ULIYE KARIBU NAE!



ULIYE KARIBU NAE


Ni kawaida tu, ili kitu kiwe karibu na wewe, kuna uwezakano wa kuwa ni kitu kinachokuzunguka au wakati mwingine kinaweza kuwa ni kitu unachokiona kila siku pindi unapotembea au kukaa na hata unapofanya shughuli zako.

Ni kweli kabisa kuna mtu aliye karibu na wewe kwa maana anahusika na moyo wako na mwingine ujamusisha katika moyo wako ndomana jambo moja linaweza kuwa kuta wote lakini mwitikio wako utakuwa tofauti kwakua  utategemea nafasi yao  kwako.

Kwakua unaishi katika dunia ambayo ina vitu vingi mathalani miti, mabonde, milima, mito na maziwa yenye kupendezesha muonekano wa dunia na wenye tija katika maisha ya mwanadamu kwakua mwanadamu utumia maji na miti katika shughuli mbalimbali ili maisha yaende.

Japo binadamu tumezungukwa na vitu vingi vilivyopo dunia na vyeme mchango mzuri katika maisha yetu, lakini athari/matokeo yake haiwezi kuonekana mathalani katika kubadilisha tabia za mwanadamu kama alikuwa na asila basi awe na upendo na kinyume chake ni sawa!

Kwa kiasi kikubwa binadamu amezungukwa na wanadamu wenzake kwakua maisha yake yako mbali na wanyama pori wanapoishi japo wako watu wachache wanaishi misituni na kuzungukwa kwa kiasi kikubwa na miti, wanyama na milima na mabonde,

Japokuwa viko vitu ambavyo mwanadamu amezungukwa navyo lakini kitu pekee kinachoweza kuinua moyo, furaha, kusonga mbele, kuamasika, kupenda au kuchukia japokuwa viko vitu vingi  lakini kikubwa ni BINADAM mwenzake.

Kwa kiasi kikubwa utakuwa karibu na binadamu wenzako hata kama utakuwa unapenda mifugo kwa kiasi gani? Hama ulikuwa unapenda kilimo kwa kiasi gani naam hata gari au nyumba kwa vitu hivyo haviwezi kuongea na wewe katika lugha ambayo itakuwa rahisi kuielewa kwa haraka kama binadamu mwenzako akiongea.

Hivyo binadamu kwa kiasi kikubwa atakuwa karibu yako! Hivyo anaweza kufanyika changamko au huzuni katika moyo na wakati mingine anaweza kusababisha maswali katika ufahamu wako na kuanza kukufikirisha muda wote unapomuona na hata usipomuona.

Kama kuna watu/ mtu unatakiwa kuwa makini nae ni mtu uliyempa nafasi katika moyo wako( sio lazima awe mpenzi) na kumpa mambo yako nimeona uadui mwingi ukianzaia hapo kwa mtu uliye mwamini sana na hata kumuheshimu na baadae ukakuta ameweka wazi staha yako( siri) katika hali hii wako watu wamepata vilema vya maisha kama vile stroke, BP( blood pressure), vidonda vya tumbo na hata mtu kuwa na kichaa.

Katika michezo yoyote ogopa kucheza na mtu ambaye anakufahamu kwani uwa atumii muda mwingi anakuwa amesha upata ushindi mapema (ushindi asubui) na wakati mwingine ataukiwa una mazoezi ya kupambana na tembo au simba kama ujarekebisha mahali penye udhaifu huyo mtu wakati wote mpinzani wako atatafuta nafasi akuangushe kwa kugusa mahali penye udhaifu wako.

Mbali na Mungu………..mtu anayekufahamu ni JANGA kwako pindi mnapotofautiana unaweza kujikuta katika mazingira magumu sana ambapo ukuwai kuwaza kama utafika hapo mathalani mtu unaye fanya nae biashara kwa shirika( partnership) baada ya kujuana sana unaweza kukuta fedha zako zilizo kwenye benki hazipo na hatimae biashara ikafa na malengo yote yakawa mwisho.

Tukienda kwa upande wa usalama mtu yeyote anayesumbua kichwa sana katika uharifu lazima atakuwa mzoefu wa mahali hapo au mjuzi mzuri wa hayo mambo ndomana uweza kusumbua katika kupata utatuzi wa haraka.

Mtu anaye kufahamu unaweza kuwa ulipiga hatua kumi lakini ukajikuta unarudi hatua moja, ambayo kwa kiasi kikubwa itahitaji ukusanye nguvu tena katika kuanza hatua nyingine.

Kwa hakika aliye karibu nawe anaweza kuwa Baraka kwako au kuwa huzuni katika maisha yako!
Pamoja na yote bado neema ya MUNGU ipo kubwa sana katika kukupa mwendo pamoja na yeye kwakua huyo akiwa karibu yako na zaidi sana akiwa ndani yako basi UTAKUWA SALAMA!

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson………………………………………………………………..0764 018535

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

Jumanne, 6 Septemba 2016

HAUHITAJI KUMLAUMU!



HAUHITAJI KUMLAUMU


unaweza kuwa binadamu wa ajabu sana hasa katika Dunia ya sasa, pindi utakapo dhulumiwa au kukosewa hama kusababishiwa kukosa jambo fulani ambalo unaweza ukahisi kama ungelifanikiwa pale basi ungelikuwa mbali au usingelikuwa pale ulipo sasa hama wengine kusalitiwa na kujikuta kuishi maisha ya lawama.

Kulaumu kwa kiasi kikubwa yamekuwa ni maisha ya watu wengi kwa ujumla wao waliofanikiwa hata wasiofanikiwa, katika ulimwengu wa sasa ni watu wachache sana utakao kutana nao ambao wasiweze kumlaumu mtu na mbaya zaidi wako watu wameenda mbali zaidi wanawaza kumlaumu hata MUNGU.

Wako watu wanamlaumu Mungu wakisema ni bora nisingelizaliwa kuliko kupata aibu hii kutoka kwa mtu huyu au kwa watu hawa kwani kule ningekuwa salama ninge kuwa na wewe(Mungu) na mimi tu maisha yangeenda sawa kwakua najua kamwe nisinge kuumiza kwa maana yote ungenitendea ni mema tu hivyo moyo wangu unge furahi siku zote kuliko kuwepo katika dunia hii iliyo jaa machafuko ya kila namna yasiyochafua moyo tu bali hata ngozi kudhoofika/kukunjamana.

Kikawaida neno hili kulaumu limekuwa kama haki ya mtu aliyekosewa hama kuonewa na pindi ukianza kumlaumu mtu aliye kuumiza watu hawawezi kukuona kuwa umekuwa MJINGA bali zaidi sana watakuonea huruma na kukupa moyo wakisema leo imepita ujui kesho Mungu amekuandalia fungu gani katika maisha yako hivyo uwe na moyo wa subira.

Pasipo kuficha uwa naona kuna mateso makali na maumivu makali sana pindi mtu anapoingia katika maisha ya lawama, kwani kiu ya maji inaweza kutoweka ghafla, njaa ikakimbia pasipo kujua imeelekea wapi? maana unaweza kuitafuta pasipo kujua hivi kwanini imetoweka mbona sijaiambia iende, pasipo kujua hayo ni matokeo ya lawama kuota mizizi katika moyo wako.

Na hakika naweza kusema kuwa hakuna kitu cha maana sana kama kuishi pasipo kuweka misingi ya lawama, kwani yanafanya maisha yako kuwa rafiki wa furaha,amani na upendo hivyo yanapelekea kuwa ni rahisi kutimiza lengo katika maisha kwakua bidii na ufanisi kutokana na utulivu wa akili katika utendaji upelekea urahisi wa kutimiza lengo lako katika njia iliyo salama.

Najua swali kubwa ni kwanini nisimlaumu wakati yeye amechangia kuharibu maisha yangu?
Ni swali nzuri na kwa mtu mzima yeyote lazima ajiulize swali kama hili? Lakini nami naweza kukuuliza hivi ukisha mlaumu nini unafaidika katika maisha yako kitakacho kupa hatua bora katika maisha yako ya rohoni au ya mwilini.

Unaweza kusema nitaishi maisha ya kumlaumu ili niirizishe nafsi yangu je! ni kweli ndio njia sahihi ya kuirizisha nafsi yako?

Nikubaliane jambo lolote ambalo aliupendezi moyo wako basi ni wazi litaumiza moyo wako na hatimae kukupa sababu ya kumchukia au ya kumlaumu kwa kitendo alichokufanyia.

Yesu alipokuwa anapigwa mijeledi na kuteswa mpaka kufa nafikiri huyu alikuwa na sababu ya kuwalaumu watu tangu alipo mkamata hata wakamjeruhi mwili kwa mijeledi iliyo lalua mwili wake na kufanya kuwa kitu kisicho thaminika, kumbuka yesu alikuja kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu lakini hao hao wanadamu walimjeruhi na kuhakikisha mpaka anakufa,
Lakini katika yote …………. Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.( Luka 23:34).

Ni kweli kuiga kitu kinachofanywa na watu wengine ni jambo baya lakini sio kila kitu cha kuigwa ni sawa kwako hata kama stori zenu zinafanana kwa kiasi gani kila mtu kuna mahali alipotokea anachimbuko lake na anauelewa wake hivyo anautatuzi wake.

Niseme kuwa hakuna kitu kizuri kama uhuru wa ndani kwani uhuru ndio matunda mazuri yanayoonekana nje yanayooshesha kushamiri na kunawiri kwa nje! Niseme uhuru wa ndani unatuzwa na mtu husika kwani kama furaha anaipata mtu binafsi na maumivu anayapata binafsi hivyo sio kila watu wanavyo fanya ndio usahihi wa kufanya zaidi ya kutenda katika kuhakikisha uhuru wa ndani unakuwa ni maisha yako.

IPENDE HATIMA YAKO KWA KUUTUNZA MOYO WAKO NA UTUNZE MOYO KWA KUMPENDA MUNGU WAKO BINAFSI!
Imeandaliwa na:

Cothey Nelson………………………………………………………..0764 018535

Jumanne, 9 Agosti 2016

SUBIRA ISIYO NA KIKOMO!



SUBIRA ISIYO NA KIKOMO!


 Ni vizuri kuwa na moyo wa subira lakini sio kila kitu cha kusibiria mathalani uwezi ukajenga moyo wa subira kuwa labda kuna wakati maji ya bahari yatakuwa hayana chumvi!
 
Uwa sio ajabu kuona mtu anakwambia hapa nimekaa muda wote kuna kitu nasubiri! Au mwingine akasema nasubiri aseme tu mimi nimalize! Na mwingine atasema na subiri ajikwae tu mimi nichukue mzigo! Na mwingine akasema nasubiri ajipendekeze tu ni mpe yake! Na mwingine atasema nasubiri ajikoroge tu alafu ni mnyweshe! Hatari.

Japo tunajua kuwa SUBIRA kama hali ya kungojelea kitu, ila inakuwa na maana sana kama hicho kitu kinachongojelewa kina sifa ya kungojelewa/ kungojewa………usiwe ukawa unaenda mbugani kutaka kumuona simba akila manyasi kwa hiyo ukapoteza muda, fedha ili kwenda kuona tu ipi siku nitamuona akila majani au ukawa unasubiria kwa hamu kubwa kuona bundamilia mwenye mistari siku mistari hiyo itakapofutika kwahiyo ukawa unakesha na kumuomba Mungu ukitarajia kuwa hipo siku utaona mistari ya pundamilia ikifutika kwa hiyo ukajikita katika kusubiri ukatazamia yasiyo tazamika.

Ni kweli sikatai kuwa kweli subira ya vuta heri lakini ni jambo muhimu kujua kitu unachokisubiria kweli kina sifa ya kusubiriwa au kinasifa ya kupotezewa ni muhimu utambue sio kila kitu ambacho watu wanasubiri basi nawe unabidi usubiri mathalani mtu, ndugu yake akiwa amesafiri inawezekana yuko nchi nyingine hivyo anaenda kituo cha basi au cha ndege kwa ajili ya kumpokea ndugu yake basi nawe ukaenda kituoni kwenda kumpokea kitu kisichokuwepo kwa hiyo ukakaa pale kituoni watu wana wapokea ndugu zao lakini wewe upo tu mpaka mwisho unafika bado upo tu.

Ni  vizuri kutambua kuwa subira ni kitu kizuri ila unasubiri nini ni jambo la msingi ilikujua huu ni wakati wake wa mimi kusubiri hichi kitu au nianze shughuli nyingine nachojua mimi hakuna kitu kinacho umiza sana kama kitu unachosubiria kikawa tofauti na vile ulivyo tarajia mathalani mama mjamzito anapokuwa ana hamu ya kumpokea mtoto wake lakini yale matarajio yake yakawa sivyo hivyo akaingia katika ulimwengu wa maumivu makali baada ya kukosa furaha yake, pia katika ulimwengu wa mapenzi unaweza ukasubiri mtu wangu ipo siku tutafunga ndoa lakini ghafla amebadilika atakikusikia tena habari za ndoa hata ukaendelea kusubiria labda kuna siku ataamka vizuri lakini wapi hatimae ukashuhudia bahari na nchi kavu vikiachana.

Wako watu wanasubiri hadi wanapata magonjwa katika miili yao ( pressure,stroke etc.) na wengine hata kuwa vichaa kwa kutegemea ipo siku atabadilika au mazingira yatabadilika na bado yamekuwa magumu tu tofauti na ulivyokusudia  na wengine atakufikia hatua ya kujiua kwa kuona subira yangu haina maaana kwani ninachosubiria sicho kinachotakiwa kusubiriwa.

Kwa kweli watu wamekuwa na hali ya kusubiri kwa vitu vingi pasipo kujua na hivyo vitu kweli vinawasubiri wao , kwani unaweza ukasubiri embe mpaka lina oza bado wewe unasubiri tu kuwa ipo siku embe lile nitakula tu!

Niseme pole sana kwa wale walikuwa wakisubiri vitu vingi pasipo kutokea au vikawa tofauti na matarajio yao, huna haja ya kuchukua maamuzi yatakayo dhuru nafsi yako au kujenga kisirani maadam unaishi jua kila kitu kitakuwa sawa maadam Mungu ( muumbaji wako yuko nawe).

Mambo ya kuzingatia:

l. Jifunze kitu kutokana na hali iliyokutokea 

 ll.tembea katika njia sahihi

lll.weka imani thabiti kwa Mungu

Tambua sote ni kazi ya mikono yake! Anatupenda atakama tukiwa wachafu kiasi gani aliye ruhusu utoke duniani analo jambo jema na maisha yako. Ni kweli watu wanaweza kukukatia tama lakini kamwe si Mungu! Ifurahie siku yako. Asante!
Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………………..0764 018535

Jumanne, 19 Julai 2016

NINI TATIZO?



NINI TATIZO?


Unaweza kukuta mtu anasema leo sijisikii kusema na mtu! au  Leo sijisikii kula chochote na huku haumwi au mabadiliko ya kibiolojia! hama Leo nataka niwe pekee yangu! au Leo sijisikii kupokea simu ya mtu yeyote wala kuingia katika mitandao ya kijamii!mh! Leo sitaki utani kabisa na mtu yeyote! Yaaani leo naomba mniache tu! Kwa kweli leo siku yangu haikuwa vizuri kabisa! Na mwingine ataenda mbali kidogo atahitaji dawa ya kutuliza maumivu ya kichwa! Na mwingine atasema Jamani leo mniombee tu maana moyo wangu siuelewielewi kabisa! Swali langu kwako  ni dogo tu JE! TATIZO NINI?

Unaweza kukuta mtu anatoa sababu ya kuvunja ahadi ya kukutana”samahani leo sijisikii vizuri kabisa” hata kama ni uongo atasema tu kwa sababu kuna kitu kime mvuruga ndani ya kichwa chake…mwingine atashindwa ata kwenda kazini na kutoa dharura ambayo haijaokoka maadamu apate tu aone mahali gani nitapata AMANI iliyotoweka ndani maana jambo hili silo la kawaida kwangu! Narudia tena nasema TATIZO NINI?

Unaweza kukuta mtu amekuwa bubu ghafla inawezekana mara tu baada ya kupokea simu au ya kutoka uko aliko toka na pindi utakapoanza kumuongelesha mdomo unaweza kuwa mzito na machozi yakatoa majibu yanaelezea hisia za moyo tafsiri ambayo ni ngumu kuielewa maana ni zaidi ya siri! Nauliza tena TATIZO NINI?

Unaweza kukuta mtu amefika chumbani kwake kajitupa ndani hanamaelezo kabisa ule ucheshi wake umepotea kabisa, lile tabasamu alipo tena na anaweza kujitaidi kukupa karatasi ikielezea yale aliyojibiwa na akapelekea kuamuru mwili wake kutoa maji yapitayo machoni! Nauliza kwa mara ya mwisho TATIZO NI NINI?

Ni kweli hali hii inaweza kukuta katika mambo mbalimbali ikapelekea kuwa na sura ambayo wewe mwenyewe kama ungajiangalia kwenye kioo ungejichukia sana….. inaweza kuwa ni tatizo la kifamilia au binafsi au jamaa ambao moyo wako ulimpa nafasi katika maisha yako kuwa ni rafiki yako hivyo lolote baya lililo mpata yeye wewe linakugusa kwa asilimia zote.

Karibu tuzungumze?

HIVI MNAPO AMUA KUVUNJA MAUSIANO YA KIMAPENZI NANI ALAUMIWE AU NANI NI CHANZO?
Je! Ni ninyi wenyewe? Shetani? Mungu? Ni nani wa kulaumiwa au hakuna wa kulaumiwa basi kama hakuna wa kulaumiwa sio vibaya mnaweza kupendana katika mwendelezo! Possible answer!
Wakati mwingine imekuwa ngumu kujua nani ni tatizo kwakua kila mtu atavutia kwake na kusema yule ni chanzo kwakua aliniambia mimi hivi! Na mwingine atasema yeye ndio chanzo kwakua yeye alinijibu hivi! Basi tukaamua hivi……..na maisha yanaendelea ni kweli hata kama msinge amua hivyo bado maisha yange endelea maadam uhai ungalipo.

 pindi mnapoingia katika ulimwengu huu mnakuwa mnaishi dunia nyingine inaitwa dunia ya wapendano na hapo mnaunganisha hisia zenu kwa ukali usio na maelezo ya kueleweka ila wenyewe mnaelewa sana kuliko maelezo.

Unaweza kuona mtu ana kuwa na huyu baadae anasema huyu anifai au moyo wangu ahujaridhika kabisa na baada ya kupumzika kwa kitambo kidogo anarudia tena na bado anasema bado moyo wangu haujapata tulizo lake! Hapa TATIZO NI NANI?  Unaweza kusema bado sio tatizo langu ila linaweza kuwa ni hisia zangu au la mtu mwingine.

Haya ni maisha ambayo hakuna mwanadamu anapenda kuishi maisha ya namna hii leo yuko na huyu na kesho yuko na yule na hata kufikia mtu mpaka anaoa au kuolewa mapaka anaanza kuwafananisha mtu aliye naye na mtu aliyewai kumjua mwanzoni.

Sikatai tatizo linaweza kuwa kwa mtu mwingine au kwako lakini lazima uchukue muda wa kutafakari sana kile unachokita katika akili yako ni kweli kipo na je! Hicho kinatengenezwa nawe au kinatengezwa na wengine na wewe unakitumia tu.

Ni muhimu kujiuliza kuwa kile kinachosemwa ni kweli kipo na kina uhusiano wa kweli na hayo mahusiano au kuna utofauti mkubwa na unajua kila hali inategemea na mtu husika.

Ninachoamini mimi kuwa UKIJUA KWELI UTAKUWA SALAMA NA UTASABABISHA USALAMA KWA WENGINE! 

Ni kweli hauwezi kuwaambia watu kitu ambacho wewe ukijui vizuri, kumlaumu mtu sio jambo jema ni bora ujitambue wewe binafsi kuweza kumudu mwili wako na ukiweka ustawi wa kudumu katika maisha yako na sio STAREHE ISIYO NA TIJA.

Katika hili uhitaji kuona Mungu akupendi au watu wanataka kukuchezea tu akili yako bali ni vizuri utambue USALAMA WAKO UNATEGEMEA UBORA WA AKILI YAKO!

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson………………………………………………………0764 018535

TUNZA THAMANI YAKO!