Ijumaa, 31 Januari 2020

HII PINGU NI KWA AJILI YAKE!




Pindi unaposikia neno “ PINGU” akili yako inaweza kukupa tafsiri/picha ya kifungo kinachotokana na kosa fulani ambalo mtu amelitenda inawezekana kwa kujua hama kutokujua au kwa kukusudia hama kutokukusudia au kwa kusizingiwa hama ni kosa kwa uhalisia alilolifanya mtuhumiwa.

Na ni jambo linalojulikana kuwa maisha ndani ya kifungo ni maisha yasiyo na uhuru bali utumwa na mateso uwa ndio fungu lake.

Japo sio kila vifungo vinafanyika kwa watu ni bahati mbaya bali yapo baadhi ya makosa ambayo mtu anayafanya kwa kujua kabisa kuwa baada ya tukio hili ambalo na kwenda kulifanya kifungo ni haki yangu mathalani unaweza kukuta mtu/watu wanasema “ kwa kosa/jambo hili nililofanyiwa wachanifanye haya japo najua kifungo na mateso ndicho kitakachofuata “

Ukiangalia kwa mapana zaidi wakati mwingine ukweli kifungo akimtesi mfungwa tu bali hata wale wanaouhusiana karibu naye wanateseka, kwani mbali na kukosa uwepo wake kwa karibu pia inawezekana hata jamii yake kukosa huduma ulizokuwa unawapatia, hivyo jamii yake ikiyakumbuka yote hayo majonzi na huzuni itatawala mioyo yao na hatimaye maji adimu yakaanza kutiririka machoni ( machozi ).

Pia unaweza kuingia kifungoni pasipo kujua kwanini yamekukuta hayo na kukuingiza hapo lakini mwisho wa jambo inaweza kuwa funzo kwako au kwa mtu mwingine na wakati mwingine hilo jambo linaweza kuwa faida kwa mtu mmoja au familia, jamii na hata taifa kwa ujumla wake.

Mwanzo 45:5………… Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu.

Haya ni maneno ya yusufu baada ya kutoka gerezani na kuwa na nafasi ya juu katika ufalme wa farao, yeye alikuwa na uwezo mzuri kutambua sababu ya kifungo chake!

Na ni ukweli kuwa uvumilivu unaweza kuzaliwa ndani yako pindi unapojua najigharimu hivi kwa sababu ya hiki au kile hama kwasababu ya mtu au watu pia wanaweza wasiwe na uhusiano nawe wa damu au WAKAWA NAO! Mathalani mzazi anapohatarisha maisha yake hata kujiingiza kwenye shughuli zitakazo athiri afya yake napengine hata utu wake ili kuhakikisha yule anayemtegemea anapata mahitaji yake inawezekana mtoto/ndugu au mtu baki tu.

Yohana 10:15……….. kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.

 Naam wako wazazi wanalala njaa ili kuhakikisha mtoto anaenda shule na kupata mahitaji yake muhimu.

Wakati mwingine ili kitu kimoja kizaliwe lazima kimoja kife, mathalani ili upate kuvuna mahindi ni lazima mbegu za mahindi uzifukie zioze chini alafu mmea uchipuke na hatimaye upate mavuno yake mbali na hilo pia hata mdudu kinyonga pindi anapozaa anapoteza uhai wake ili kiumbe kingine aina yake kiweze kutokea.

Ni muhimu usitushwe na hali ngumu unayoipitia au hali inayokuzunguka bali tishiwa/ogopa na matokeo yajayo baada ya hali ngumu iliyokuwa inakukabili au inayokukabili.

Wafilipi 3:14………. nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.

Wafilipi 3:13…………Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;

Kwa asilimia kubwa inaaminika kwamba “ Hakuna ukombozi bila kujigharimu “ ndomana hata ukombozi wa nchi nyingi za afrika ulipatika baada ya mtu mmoja kujigharimu ( kuhatarisha maisha yake ) mathalani Tanganyika-hayati.Mwl. J.K.Nyerere, Afrika ya kusini-hayati. Nelson Mandela na wengine wengi.

1 Yohana 3:16…….. Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.

Na kuna msemo unasema “ ili upate lazima utoe “

Furahia sana pindi itakapo kubidi kuvikwa pingu kwa ajili ya usalama wa mtu mwingine.

Pingu  yako ya LEO ndio fahari yako ya KESHO!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………0764 018535

Ijumaa, 17 Januari 2020

BAADA YA DHIHAKA KUNA HESHIMA!




1 petro 1: 11……..Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.

Uwa tunaifurahi leo kwasababu tumeipita jana na tunaitumaini kesho kwakuwa tunaishi leo,
Mathayo 17: ( 24-27 )…… 24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

                                         25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
                                         26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
                                          27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

Tuna tambua katika machafuko hapo uimara wa mtu uonekana, na ni katika msingi ulioshikiliwa na neno lazima uwe salama katika dhoruba yoyote.

Moja ya kitu kinachopiganiwa sana na watu ni kuwa na heshima “ kuheshimika” maana itazidi kumjengea nafasi katika jamii aliyekuwepo.

Japo ni mtego mkubwa kwakuwa watu wengi wako tayari kupata heshima lakini awako tayari kudhihakiwa pasipo kujua wakati mwingine dhihaka uweza kukupeleka kwenye heshima. Ndomana wengine uweza kusema baada ya taabu/dhiki faraja!

Inakuwa sawa na mtu anataka kuvuna pasipo kujigharimu katika kupanda!

Imekuwa ni rahisi mtu kuikabili dhiki/changamoto baada ya kuona kuna neema mbele yake lakini sio kitu rahisi kuikabili dhiki/changamoto kama hataona neema itakayozaliwa baada ya hapo.

Unapoamua kuishi na Mungu hayo majira uwezi kuyakwepa kwakuwa yapo ili kuhakikisha heshima yako inadumu na sio kushuka ni sawa mjenzi wa ghorofa lazima haende chini sana ili apate uwezo wa kwenda juu sana.

Kila mtu upenda heshima lakini ni muhimu kutambua heshima inatengenezwa unaweza jua au kutojua lakini ukitembea kwenye kanuni basi matunda yake yatadhihirika tu.

Unapotambua baada ya dhiki kuna heshima haupaswi kuishi maisha ya unyonge au ya ukiwa bali ni kipindi cha kuimarisha roho+akili+mwili wako tayari kuingia katika hatua nyingine ya maisha yako iliyobeba heshima yako.
Kipindi cha dhihaka kinakuwa kigumu sana kwa mtu asiyejua namna gani ya kuishi katika kipindi hicho, unaweza kukuta mtu katika kipindi hiki amejawa na lawama, huzuni na teso lisilokoma, na hali hii inaweza pelekea kushindwa kuifikia heshima yake.

Unapaswa kujua heshima inakuja, katika kujibu maswali yaliyo jikita katika fahamu zako na hata kuondoa pumziko la roho yako na sio kuwa kikwazo kwa wenzako.

Na heshima ya kudumu haiji tu kwasababu imetokea tu bali kwasababu unastahili, hivyo ni lazima ustahili kwanza ili heshima iweze kuja kwakuwa kila jambo linatokea katika mazingira yake na kama si mazingira yake ni vigumu kutokea.

Ni muhimu kuzingatia katika dhiki uko na nani ili heshima ije!

Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. ” zaburi 23:4

Usije ukaishi maisha ya kufuata mwili ukategemea heshima ya Mungu ikuambate/kukufunika kwa kuwa heshima yake haichanganywi .

Unapopita katika dhiki pamoja na Mungu basi hapo tegemea heshima ya Mungu kukuinua.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………….0764 018535


Ijumaa, 3 Januari 2020

AMANI YANGU INATUNZWA NA YEYE!




Yohana 14:27
“Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga”.

Moja ya bidhaa/kitu adimu katika ulimwengu wa sasa ni AMANI, maana palipo amani ndipo radha ya kitu unachokifanya unakiona,mtu uliye naye au mahali uliopo upafurahie na siku zote uona sababu au umuhimu wa kuwa hapo.

Moja ya kitu ambacho mtu angetamani awe nacho siku zote za maisha yake ni Amani ya kudumu ndani ya maisha yake, na kizuri zaidi amani ikiwepo udhihirisho wake utaonekana ila amani inapotoweka viashirio vyake utaviona na hapo unyonge na ukiwa pamoja na hali ya kutoendelea uweza kujitokeza na hata kupelekea kupoteza mwelekeo.

Tatizo sio kuwa na kitu bali ni namna utakavyo kitunza ili kiendelee kuwepo “ uki kitunza kitadumu “
Namna unavyokaa nacho kinaweza kuzidi kukita mizizi yake au kupoteza utawala wake.

Wako watu amani yao inatunzwa na kazi nzuri aliyonayo, rafiki mwenye uwezo wa kumsaidia apatapo shida, mchumba au mali alizonazo n.k , inapotokea vitu hivyo vikipotea/kuondoka uwa vinaondoka na amani yake kwakuwa vitu hivyo ndivyo vilivyo shikilia amani yake hama ndicho chanzo cha amani yake ( hivyo vinaondoka na amani yake ).

Sio rahisi kujua msingi wa amani wa kila mtu unayemuona ( hasa jamii ya waaminio/ waendao kanisani ) uwa wengi upenda kusema “ amani yangu ina Mungu” huna haja ya kubishana nao, subiri vile vitu halisi/ hasa vinavyoshikilia amani yake pindi vitakavyopata mtikisiko utoshangaa hata ratiba za kanisani zitaanza kupungua na kuanza kambi za ghafla ghafla pamoja na maombi yasio kuwa na mpangilio maalum bali yanasukumwa na hisia pamoja na msongo wa mawazo.

Kujua kuwa “ amani yako inatunzwa na Mungu “ na kuifanya “ amani yako itunzwe na Mungu “ hivi ni vitu viwili tofauti ni sawa sawa na mbingu na nchi, uwezi kuirahisisha kimawazo ukasema mbingu na nchi vinafanana ukaachana na uhalisia uliopo!

Natambua kuna vionjo vya mwili vinavyobebwa na matukio mazuri yanayomtokea mtu mathalani kuifikia/kuikamilisha ndoto yake, moyo uweza kuchangamka na kusababisha tabasamu kwenye uso.

Hatua ya kwanza ili uwe na amani iliyozaidi ya amani zote jambo muhimu lazima umpate Mungu kwanza ili akupe amani yake hiyo AMANI hainaga mbadala, uwezi kutamani amani ya mtu wakati mtu mwenyewe umtaki! Lazima umpate mtu hapo ndipo utaanza kuiona amani yake.

“ palipo na yeye amani yake ipo”.

Usikubali “ kujitekenya na kucheka mwenyewe ” huku ni kupoteza muda unapoamua kuwa na amani ya Mungu basi hakikisha unampata Mungu kwa ukamilifu wake.

Hii itafanya/kuzidisha mng’ao wako kuzidi wala usififie maana uko katika amani inayonawirisha.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………………0764 018535