Kitu ambacho MAJAMBAZI, MAFISADI, MAJANGIRI NA HATA
WANASIASA…… hawawezi sahau kusema “KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA” hasa wanapokuwa
wamepewa nafasi kuongea katika hali ngumu iliyo wakuta watu fulani au jamii kwa
ujumla wake.
Naam unaweza kuwa binadamu wa kwanza pindi utakapoinuka na
kusema Mungu anamakosa au anakosea! Kwasababu katika hali ya kawaida watu wengi
wanamuogopa Mungu kuliko kumuheshimu.
Na utakuwa binadamu wa kawaida kama sio mwenye busara
utakaposema MUNGU HAKOSEI! Japo hili neno sio wakati wote linakuwa na maana
sana kwa mtu anayelisikia au kulitamka kutokana na mateso au maumivu yaliyo
ndani ya moyo wa mtu husika.
Japo wakati mwingine mazingira na uhalisia wa mambo
yanayoonekana na kile anachokisema Mungu ina onekana kuwa haiwezekani tena hata
kama yeye anasema! Kwa kuwa dhoruba inapokua kali na moyo uweza kupoteza
matumaini yake.
Ahadi ya kuingia nchi
ya kanani!
Yoshua 1:6 Uwe hodari na moyo wa ushujaa,
maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya
kwamba nitawapa.
Imani uweza kufifia pindi unapowaona watu kama majitu!
Hesabu 13:33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili,
wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
Pindi unapotambua/ kusikia ahadi ya Mungu juu ya maisha yako,
usifikiri tu kwasababu amesema basi itakuwa tu hata kama niki lala au
kuisubiria tu itakuwa au itakuja tu sio kitu chepesi kama utakavyo fikiria.
Uwa ahadi ya Mungu inapoachiliwa ndivyo vita vinainuka
kuizima hiyo ahadi isi dhihirike katika mwili au isitimie.
Hata yesu alipotaka kuzaliwa na hata alipozaliwa vita dhidi
yake ikaibuka………..hata malaika akamtokea yusufu na kumwambia aondoke!
Luka 2:9 Malaika wa Bwana akawatokea
ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.
10 Malaika akawaambia, Msiogope; kwa
kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;
11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi,
ndiye Kristo Bwana.
Kwa hivyo ni muhimu kutambua kuwa kitu kipya kinapotaka
kuzaliwa hapa anga linatambua na hata kuweka kizuizi dhidi ya hicho kitu.
Mathayo 2:13 Na hao walipokwisha kwenda zao,
tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka,
umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa
maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.
Hali ya kutambua kuwa Mungu hana kawaida ya kukosea, hali
hiyo lazima idumu katika maisha yako mpaka ahadi hiyo itimie, uwa Mungu
anaposema anakuwa ameshamaliza ahitaji nyongeza tena zaidi ya kuona imetimia.
Ni muhimu kutambua ni kweli Mungu hakosei ( maana ajawai
kukosea ) ila wewe unaweza ukakosea ukasababisha ukose ahadi ambayo Mungu
aliiandaa kwa ajili yako.
Ahadi ya Mungu hipo na inapotoka uwa imetoka inategemea
mazingira yake ili kutendeka zaidi ya asili ya neno lenyewe lisiloshindwa,
lenyewe liko zaidi ya mazingira yote na linajitosheleza alihitaji usaidizi
wowote, maana neno la Mungu ndio asili ya vyote hata vile unavyo viogopa
vinaweza kumezwa hama kusimamishwa na neno.
Na ni muhimu akili yako ijue kwamba kabla ya wewe ujazaliwa
naam hata dunia kabla haijaumbwa mpaka leo Mungu ajawai kukosea japo wakati
mwingine kutokana na akili zetu zilizo na mipaka unaweza kuhisi hama kuwaza
kwamba Mungu anakosea kutokana na muono wako lakini sio sahihi, kwakuwa hiyo ni
akili yetu sio akili yake.
Na ukumbukwe hakuna mtu/kitu kinachoweza kumrekebisha Mungu
maana vyote vilifanywa naye zaidi sana Mungu kuachilia siri yake katika akili
zetu mathalani ukuaji wa vitu: mimea, wanyama na viumbe vingine lakini sio
kuviboresha zaidi ya kujifunza kwanini iko hivyo/ inakuwa hivi.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………….0764
018535