Ijumaa, 29 Oktoba 2021

NI KWELI MLIMA NI MREFU LAKINI UNAPANDIKA!

 



Kama tunavyojua milima kama miinuko iliyojitokeza katika ardhi iliyo chipuko kwa asili ( tangu dunia kuumbwa) na mingine iliyojitokeza kutokana na tabia nchi mathalani volcano na sababu nyingine! Tunaishi na kuifurahia.

Moja ya kitu kinachoweza kufanya uendelee kupanda mlima/kuendelea na safari yako ni uwezo wa jicho lako katika kuona kilele cha mlima!

“ maana pale utakapo paona ndipo utakapo pamiliki”

Kile unachokiona ndicho utakachokimiliki nje ya kuona uwezi kumiliki ( uwezi kumiliki gizani ).

Nguvu inazaliwa au kupungua kutokana na nguvu ya kuona inayozaliwa ndani yako.

“ ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo”

NI KWELI MLIMA NI MREFU LAKINI UNAPANDIKA!

Karibu!

Mwendo wako katika kupanda mlima uamliwa na ukubwa ( upana au urefu ) wa mlima hivyo masaa, siku au mwezi utakao tumia katika kufika kilele cha mlima na sio kwamba au pandiki huo mlima .

Mathalani mlima mrefu katika afrika ni KILIMANJARO na hapo haimaanishi kuwa hakuna mlima afrika zaidi Kilimanjaro la asha! Ipo milima mingi tu na iliyo na muonekano  mzuri na wa kuvutia vilevile pia inapandika vizuri tu ila moja ya utofauti ya utofauti ya mlima huu ni mingine ni siku au muda utakazo tumia ili kufika kileleni.

Ukweli wakati mwingi jicho linapoona mlima vile ulivyo mkubwa unaweza kukuta miguu ikakosa nguvu na kupelekea hata moyo kughairi.

Ni muhimu ujifunze kuona jambo kwa jicho la tatu, uone tu maadam pana nafasi ya kuweka hatua kuelekea juu basi hapo uanze kuona fursa ya kwenda juu na hatimaye kufika kileleni.

Pindi akili yako inapoanza kuona kama kuna kufika basi ustahimilivu na kuvumilia mitelezi, kujikwaa na hata kuchomwa miiba na mengine mengi na hatimaye unafika.

Kuna siri kubwa sana ya ushindi inayozaliwa katika kuona kwa kuwa bila ya kuona hakuna ushindi.

“ kikubwa uwezi kwenda pasipo kuona”

Mathalani unapoona huyu mtu si mwema kwako hakuna jambo jema litakalopata kibali/kukubaliki katika moyo wako hata akicheka utaona anakusanifu.

Mungu anakuwa sawa na imani yako ukiona anaweza utaweza!, utaona uweza wake, maana ukiona kuwa ni baba yako naye atakuwa baba yako ( imani- jicho lililojichifa ). Jambo ukishaliona kuwa ni gumu ni vigumu tu yeye kukupa akili yake. ( kuyafunua macho )! Labda upate neema tu.

Macho yako yanaweza kuzuia utendaji wa kimbingu au kuruhusu utendaji wa kimbingu.

Ishara ya kukubali na kuamini Mungu ni mkubwa na hakuna linalo mshinda ni pale tu akili yako na macho yako hayataweza kuona huu mlima mkubwa na haupandiki,

“ nitayainua macho yangu ni tazame mlimani msaada wangu utatoka wapi?”

Tambua dunia na vyote vimetoka kwake yeye ndiye anajua alifanya nini milima ikatokea na mbingu ikawa juu na nchi ikawa chini na bahari/maji yakawa ni mipaka yake.

“ aliyekitengeneza anaweza kukibomoa”

Kama vyote asili yake ni yeye basi mshike yeye na wala si maneno ya watu!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………..………………….0764 018535

Ijumaa, 15 Oktoba 2021

MIWANI YANGU INANIPOTEZA

 



Miwani kama kifaa kinachowekwa machoni ili kutoa usaidizi wa macho ili kuweza kuona vizuri, na inawezekana ukavaa miwani kwa kupenda au kutopenda na kwa asilimia kubwa wanaovaa miwani uwa wanakuwa na matatizo ya nguvu katika kuona,

Japo matatizo ya macho yamegawanyika katika sehemu kuu mbili:

i.                    Kushindwa kuona mbali

ii.                  Kushindwa kuona karibu

Pamoja na matatizo hayo lakini chanzo chake kinaweza kutofautiana mtu na mtu, wako waliopata na matatizo ya macho kwa kurithi, vyakula, mtindo wa maisha na wako waliokuwa wanavaa miwani kama kutafuta muonekano mzuri pasipo kujua hiyo miwani ni tiba kwa mgonjwa wa macho waka kuta wanakumbwa na matatizo ya macho.

Pia wako watu wanamatatizo ya macho wamefikia hatua ya kuvaa ya miwani lakini awavai ( kutopendelea ) au uvaa kwa tukio maalum au majira fulani tu.

Vilevile wako watu wasio na matatizo ya macho lakini upendelea kuvaa miwani inawezekana katika kutengeneza muonekano wa kuvutia zaidi.

Karibu!

Ningependelea kuangalia miwani katika uwanda wa uhuru wa kuvaa au kutovaa,

Ni kweli unaweza vaa miwani pengine pasipo kujua hiyo miwani ni tiba ya macho, lakini wewe ukaamua kuvaa ili mradi uimarisha umaridadi pasipo kujua kwa kuendelea kuvaa miwani kutapelekea kuathirika kwa macho yako.

Sio vizuri kuona rafiki yako anavaa miwani basi ukaona na wewe uingie mkondo huu wa kuvaa miwani pasipo kujua kwanini rafiki yako anavaa miwani.

Kuna vingine vya leo vinaathari kubwa kesho.

Unapoishi katika jamii unapata kujua/kuona mienendo mbalimbali inayoendelea katika jamii,sio uone mtu anavaa nguo za gharama, anakaa katika makazi mazuri hama anaendesha magari ya kifahari, ukasema maisha ndio haya pasipo kujua gharama katika kupata na kutunza.

Na pengine unaweza usijue uharibifu gani unakula nafsi yake chinichini,

Sio kila unachokiona unataka kukichukua ( kuvaa miwani ) kumbe unaweza kukiacha na bado ukawa salama sana.

Ni kweli unaweza uvae ukisasa lakini angalia yasije yakakupata ya kisasa! Au ukapoteza maana katika wengi maana kila nafsi itapata maumivu yake.

Ni vizuri kutembea katika njia ambayo inakupa mwanga kuliko kung’ang’ania njia ukijua unamfurahisha mtu uku unajua unaangamia wewe binafsi.

Using’ang’ania miwani ambayo ina umiza macho yako hata kama maumivu sio makali hata kama watu watakusifia sana au kukuona umekuwa wa kisasa ni bora uache au rudi kwa daktari akuibadilishie akupe itakayo kufaa.

Usipende kufuata kila upepo unapoenda/ usipende upepo maadam unakupuliza maana kuna upepo mwingine unaongeza joto na sio ubaridi.

Kumbuka tunaishi mara moja hapa duniani ipende nafsi yako ishi katika ustawi wako na itunze nafsi yako.

Ni vizuri na ni muhimu kumuheshimu mtu aliye kuzidi umri,elimu, hekima n.k lakini sio kila neno anenalo mtu huyu ukalichukua ( ukalivaa ) lipe nafasi kujua je! Hilo neno au ushauri nafsi yako itakuwa salama.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………….……………0764 018535

Ijumaa, 1 Oktoba 2021

MAUMIVU ( RAHA ) YA PATANO:


Katika dunia tuliyonayo kuna mambo yanafanyika ambayo unaweza kukosa majibu kwa nini yanafanyika hivi au yanakuwa hivi au mtu huyu anafanya hivi! Wakati mwingine unaweza kujipa majibu mwenyewe na pengine ukasema hayanihusu.

Kuna mambo ambayo mtu ujikuta unaguswa kufanya binafsi hata bila kushurutishwa na mtu na pengine kuamua kumshauri mtu unayemuona anafanya visivyofaa kumwambia aache au afanye kwa namna nyingine ambayo itampa matunda kama sio kumsaidia.

Mathalani unaweza kukuta mtu anasumbuliwa na figo na limefikia kiwango cha kutofanya kazi likahitaji mbadala na watu hata ndugu wakagoma kutoa figo zao ili kukuokoa maisha ya mtu walisema wanampenda na hawata mwacha kamwe katika shida yoyote lakini ghafla kwa namna isiyofikiriwa akatokea mtu mmoja ambaye inawezekana mnamfahamu au msiomfahamu akawa yuko radhi kutoa figo yake na hatimaye akaitoa figo yake! Mkabaki na butwaa……..!

Pasipo kujua inawezekana aliwahi kuweka patano na mgonjwa wakati wa uzima wake “ sitaweza kukubali kuona unapotea wakati uwezo wa kukusaidia ninao “ !alisema aliyetoa figo, na hapo alikuwa anatekeleza alichokisema kwa matendo tu.

Unaweza kukuta mtu anatenga muda wake na kwenda majalalani na kukaa na mtu mnayemuona chizi na pengine hata kula naye pasipo kujali mazingira yaliyo mzunguka au watu watanielewaje bali ujali hile raha ya nafsi yake anayoisikia pindi akifanya hicho kitendo-kuheshimu patano!.

Pia unaweza kukuta mmoja ambaye sio ndugu hiyo familia lakini yeye binafsi amejitolea kumpeleka hospitali mgonjwa wa hiyo familia kwa kutumia usafiri wake ( gari ) kumpeleka na kumrudisha nyumbani pasipo kuchangiwa hata hela ya mafuta bali siku zote ufanya hivyo uku moyo wake umejawa na furaha pasipo kuchoka, unaweza usijue kwanini anafanya hivyo unaweza kuta alishaingia mapatano kuwa “usafiri wangu utatumika kwa faida yako na hasa wakati unashida” na hapo anasimamia kile alichokisema.

Nakubaliana kabisa kuliweka patano sio kazi bali kulisimamia patano hiyo ni habari nyingine.

Mathalani kuna mapato yanawekwa nchi na nchi kutotengeneza mabomu “nuclear” ili kutoiweka dunia katika hari ya hatari lakini bado wanakwenda kinyume na hayo makubaliano, wanabaki kulaumiana wenyewe kwa wenyewe.

Pia katika hali utekelezaji kuna uwezekano kuwa unayaheshimu maagano yenu hama kuna kuna siri iliyojificha iko ndani yake.

Kuna aina mbalimbali ya mapatano lakini mimi ningependa kuongelea makundi haya ya mapatano:

i.                    Mapatano kati ya nafsi na nafsi

ii.                  Mapatano kati ya nafsi na Mungu.

Mapatano ya nafsi naam hayo mapatano nimeyaongelea kidogo hapo juu lakini pia ningependelea kuongelea mapatano kati ya nafsi na Mungu haya ni mapatano ya ajabu sana maana unaweza kukuta unafanya mambo ambayo wewe mwenyewe uyaelewi, watu awaelewi ( unaowaamini na usio waamini ) ila cha ajabu moyo wako unajawa na furaha na amani ya kutosha.

Mathalani unaweza kuwa na patano na Mungu kufuta viatu vya mtumishi pindi anapoingia kanisani kuongoza ibada aijalishi amepiga kiwi au ajapiga/ vina vumbi au havina vumbi wapo watu watainuka kinyume nawe pengine atamchungaji mwenyewe akawahaelewi na watu wakainuka na kukuvunja moyo hiyo hali isikuweke chini!

Unapoishi katika patano lako na Mungu hapo kunawiri katika utu wa ndani kuna kuwa dhahiri, nguvu ya ndani inaongezeka na macho yako yanatiwa nuru ya kiungu.

Nipatano la ajabu sana maana kuna wakati mwingine litakupeleka kujitoa mwanga mathalani hilo patano linaweza kukuweka kuwa karibu na mashoga na kuwa na mzigo nao, jamii na hata familia yako inaweza kuwa kinyume nawe hata isikuelewe unapotoa muda wako kuongea na mashoga maana watu uamini  ” ukitembea na mwizi nawe utakuwa mwizi ”  inabidi uwe na nguvu ya kusimamia patano lasivyo unaweza kulivunja patano lako na Mungu.

Wakati mwingine unapolitumikia patano lako na Mungu kubali kuvunja heshima ya cheo  na nafasi yako katika jamii unayoishi.

Katika patano na Mungu tunaliona kwa Samson alivyoenda kinyume na utaratibu wa jamii yake ya kuoa nje ya kabila lake, lile patano lilikuwa na nguvu ndani yake naye aliamua kuliishi patano kwa gharama yoyote.

Waamuzi 14:1 Samsoni akatelemkia Timna, akaona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti.

 2 Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemwona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi mnipatie, nimwoe.

 3 Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu zote, hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana ananipendeza sana.

 4 Lakini baba yake na mama yake hawakujua ya kuwa jambo hili ni la Bwana; maana alitaka kisa juu ya Wafilisti. Basi wakati ule Wafilisti walikuwa wakiwatawala Israeli.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………….……………….0764 018535