Usipende kutumia nguvu nyingi katika kupata kitu ambacho yeye Mungu anajua unahitaji hicho kitu.
Ø SAHAU, ATAKUKUMBUSHA ( omba, utapewa )
Mathayo 7:7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
Wakati mwingi tunapoenda mbele za Mungu tunapenda atuelewe vile tunavyojielewa ili aweze kutupa haja/ yale matakwa tunayotaka sio mbaya lakini sio ukamilifu wa kupata haja yako.
Unahitaji kujua kuwa Mungu ni Mungu wa kanuni na anafanya mambo katika mawanda ya utaratibu wake sawa na uradhi wa mapenzi yake.
Mungu ahitaji umwelekeze sana ili ajue kweli unahaja na hilo jambo bali anahitaji moyo wako ujimimine kwa bwana ukieleza sifa zake katika maisha yako.
Mikakati tunayojiwekea katika mambo mbalimbali katika maisha yetu ili kufanikisha/kukamilisha malengo yetu ndivyo wakati mwingine yanakuwa kongwa au kikwazo kikubwa cha kumuona Mungu, mathalani mtu anahitaji kazi hivyo anaandaa mikakati yake ya kumshawishi bosi ili apate hiyo ajira/kazi wakati mwingine hata kutoa rushwa/kuonga ili mradi tu afanikishe lengo lake kupata kazi.
Ahuhitaji jitihada zako nyingi ili kumuonyesha Mungu kuwa wewe ni mwihitaji bali hali ya moyo wako inaongea vizuri mbele za Mungu naye anajua kuwa wewe kweli ni mwihitaji au sio mwihitaji au tamaa zako.
Karibu katika somo!
SAHAU, ATAKUKUMBUSHA…………………………………………………….
Unapoomba jambo usipende kulitafiti kwa akili zako na kulikamia bali amini limeshafanyika fanya shughuli zingine, “ tukiomba yeye atasikia “
1 yohana 5:14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia
Unapoomba jambo alafu ukalitazama kama lilivyo wakati mwingine kukata tamaa, mathalani unapomuombea mtu mwenye tatizo la tumbo alafu ghafla tumbo likazidi hatimaye mtu akapoteza fahamu hali hiyo inapotokea na kama hauna mwingiliano (network) nzuri katika ulimwengu wa roho unaweza kutafuta njia na kusepa! ( imani yako kwa Mungu inapotea ).
Naam kuliamini jambo litakalotokea sio lazima ulikazie sana macho bali ni hali moyo wako kukubaliana na kile ulichokisema.
Yesu alisema “ mti uliokosa matunda akaulaani usitoe matunda tena”
Mathayo 21:19 Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara.
Yesu akuukazia sana ule mti ili kuhakikisha unakauka palepale bali aliposema akaondoka kesho alipopita akushangaa kuona mti umekauka baada ya wanafunzi kumwambia ila wanafunzi walishangaa sana.
Wakati mwingine unapoenda kwa Mungu katika uhitaji wako lazima akili yako iwe kwa Mungu na wala sio kwa watu unaona kuwa wanaweza kutatua shida yako ndo mana kuna neno linasema SAHAU.
Maana Mungu anajua haja yako hata kabla ujafungua kinywa chako kumuomba tayari ameshakupa ni wewe kujua namna gani ya kukichukua na ni wakati gani?
“ mkiomba amini yameshakuwa nayo yatakuwa yako”
Yohana 14:13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
Ukisha mletea Mungu au kumuomba kisha ukaamini katika kile ulichomuomba pasipo shaka yoyote hiyo hali inamfanya Mungu ashughulikie hilo jambo lako kwakuwa kwake hicho ni kigezo kikubwa kuwa una mwamini na unamtegemea na hauna mbadala wowote ila ni yeye tu.
Mungu anapotaka kufanya jambo ahitaji akili yako imwelewe sana bali anataka kuishangaza akili yako ili uzidi kumwamini.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni