Ijumaa, 16 Desemba 2022

UJACHELEWA,



Kuna wakati macho yetu na maneno ya watu yanaweza kutudanganya na kuona tumechelewa kumbe sio hivyo!

Na moja ya kitu kinachoweza kutufanya kuona tumechelewa au tunachelewa ni matarajio tuliyonayo kwa jambo husika kukawia,

Naam mathalani mnawezafanya kazi kwa miaka 10 lakini ukijilinganisha na wafanya kazi wenzako japo inawezekana mnalipwa kiasi sawa lakini unaweza kuona kuwa wamekuacha mbali sana na hali hiyo ikapelekea kujiona mnyonge kama sio mpweke nakujiona kama ndege mtoto aliyekosa kumbatio la mama yake wakati analihitaji ukabaki kujilaumu na kutafuta dhambi yako.

Wakati mwingi matarajio yetu yanakuwa ndio kifungo chetu hasa yanayo ambatana na tamaa zetu binafsi mathalani unaweza kuwa katika mahusiano ukawa na furaha nyingi na hata ukaweka matarajio kuwa Mungu akipenda kipindi kijacho nitaanzisha familia yangu, lakini unaweza kukuta mwenza wako hayuko tayari au kuna mambo hayajakuwa sawa wakati mwingine hali hii inapozidi unaweza kujikuta unavunja mahusiano matukio haya yakijirudia unaweza kujihisi kuwa unanuksi kama sio mikosi hama wewe ni fungo la kukosa.

Siku zote kila matarajio uwa yanabebwa na mfumo fulani inawezekana unajua au ujui  unaweza kuwa ni mfumo wa mbingu au duniani na wala sio matarajio yetu tu, hivyo ukishindwa kuelewa  mfumo unaotawala jambo lako  ni wazi mtapishana na matokeo au yale unayoyatarajia.

Unaweza kuona uhitaji wako unachelewa maana kila jambo lina maandalizi yake, endapo usipo jua kiwango cha maandalizi yake unaweza kutaka jambo lisilo la wakati huo na mwisho likakutesa badala la kulifurahia.

Naam inawezekana ukawa na sifa zote za kupata hilo jambo na kila mtu akakupa matumaini yote lakini ukiwa nje ya mfumo unaweza kukuta nafasi hiyo sio yako.

Jifunze kutazama mambo kwa jicho la Mungu wakati mwingine unaweza kuwa na sifa za dunia lakini ukawa hunasifa za mbingu hivyo ukakosa hiyo nafasi kutokana na mtazamo wako na wa Mungu kupishana.

Kwa asilimia kubwa watu wengi pale walipo sasa awakutegemea kuwa hapo lakini wakajikuta wako hapo na pengine yamezidi matarajio yao.

Hivyo tukubaliane kuwa sio kila matarajio uliyonayo ukafikiri kuwa ni sahihi na kutojua labda kuna makubwa zaidi unayo weza kuyafikia.

Pia mbali na hapo kikubwa sio kuwa na matarajio tu bali ni kuwa nyezo ya kukusaidia kukamilisha hayo matarajio na moja wapo ni afya njema itakayo kuwezesha kukamilisha ndoto yako maana nje ya afya njema kuna magonjwa yanawezapelekea kupoteza uhai na matarajio yako yakakoma hapo.

Kikubwa usikate tamaa wala usitoe nafasi ya kumlaumu mtu maana asili ya ubinadamu ni ubinafsi kila kitu kizuri mtu upenda  kianze naye lakini Mungu ndiye msimamizi wa kweli atakupa kile unachopaswa kupewa kwa majira yake.

Usishikilie matarajio uliyonayo tu kana kwamba bila hayo uwezi kuishi, kuna kipindi matarajio yako yanawezapishana na mawazo ya Mungu, hivyo Mungu anapoanza kulidhihirisha kusudi lake hautakiwi kupingana naye maana yeye anakujua vizuri kuliko wewe unavyojijua  na yeye ndio hitimisho la maisha yako.

Hivyo usiwe mnyonge pindi unapohisi kuwa matarajio yako yanachelewa ila elewa mfumo ulioambatana na matarajio yako wala hauna haja ya kukata tamaa

“ uhai ni bora kuliko matarajio yako”

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson………………………………………………………………….0764 018535

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni