Kuna wakati unaweza kumlaumu Mungu kama sio majira ya dunia kwakuwa umekosa wa kumlaumu!
Mathalani katika majira ya mvua yanapofika kutokana na maeneo unayoyaishi maji yanakuwa ni kikwazo kwako hivyo japo unaipenda mvua lakini ukifikiri mazingira yako na mateso unayoyapata unakuwa katika wakati mgumu hivyo wakati watu wanaomba mvua inyeshe wewe unafikiri adhabu utakayoipata baada ya mvua kunyesha,
Lakini kwa mtu yule ambaye anaishi mahali ambapo mvua inyeshe kwa namna yoyote yeye anakuwa katika mikono salama kama sio sehemu salama maana kwake huyo pindi watu wanapo omba mvua inyeshe yeye atakuwa anamshukuru Mungu kwakuwa anajua joto litapungua!
Asante……………………………………karibu sana!
Naam mambo mazuri yanakupata yasikupumbaze na wala mambo mabaya yanapokupata yasikufanye kuwa mnyonge.
Usione watu wengi wanacheka basi nawe ukajiunga nao ukafikiri wanapenda kucheka na pindi unapowaona watu wanalia usifikiri wana huzuni ukawapa pole wakati mwingine kile kinachoonekana kinaweza kisiwe uhalisia uliopo.
Uwa mtu mwenye akili afurahi tu kuwa ana nyumba nzuri bali ni pale atapoona misingi ya hiyo nyumba nzuri itamfanya awe salama na endelevu kwakua hiyo misingi inafanya hiyo nyumba idumu katika mazingira yoyote.
Naam kuna kipindi katika maisha ya mwanadamu unaweza pitia maisha yatakayo fanya moyo wako kuwa chini napengine ata kujuta kwanini umezaliwa duniani, kwa kifupi hali hiyo inapelekea radha ya kuishi hapa dunia inapotea kabisa, pasipo kujua katika siku kuna mchana na usiku na bora zaidi ni kujua namna ya kuishi mchana ni tofauti kabisa na kuishi usiku na kikubwa ni kujua huko katika bustani gani na ni bustani yenye ubichi au yenye ukame?
Mathalani maisha yanayo fanana na nyasi nayapenda sana maana pindi upepo mkali unapovuma zinalala na baada ya kitambo kidogo baada ya upepo kukata hizo nyasi zinarudi kama awali na maisha yake yanaendelea mpaka kikomo chake.
Pia napenda sana maisha ya mlinzi hasa wa usiku anapokuwa lindoni akivumilia baridi kali nap engine hata mbu wakimuuma lakini uku akiacha familia nyumbani kwake wakiwa wameshakula na kupumzika japokuwa yeye anakabiliana na usiku akijua asubuhi itakuja na hili baridi au mbu wakali atawasahau.
Mbali na hiyo mifano pia napenda maisha ya mkulima pindi anapoamua kupanda mbegu zake hata kama hana akiba ya kutosha na anaweza kupitia kipindi kigumu akiwa anasubiri mavuno yake; anajua njaa haitadumu katika maisha ya familia yake bali anajua muda si mrefu kitakuwepo chakula cha kutosha katika maisha yake.
Yesu alisema “ roho yangu naiweka mikononi mwako”
Akiamini na kujua kwamba katika mikononi mwa Mungu uhai wake utafichwa naam maisha yataendelea na ushindi utapatikana.
Hayo maneno aliyasema ikiwa analikamilisha kusudi lake la kuja duniani katika kuleta ukombozi wa wanadamu.
Na ni kweli maisha yameratibishwa katika ramani ya Mungu lakini bado ni uchaguzi wako kuyaweka hayo maisha mikononi mwa Mungu au sehemu nyingine ambayo wewe binafsi utaona inafaa kwako.
Ni kweli unauchaguzi wa wapi uyaweke maisha yako lakini hauna uchaguzi kuyakataa matokeo ya uchaguzi ulioufanya ni kama vile mwanafunzi asiposoma akifeli atashangaa labda awe “ hamnazo “
Usifurahi kwa sababu unakula hama unapata unachokitaka pasipo kujali maisha yako yamebebwa na mikono ya nani? Hii ni hatari sana.
Kwani wako watu walifurahi kuwa na vitu baadae wakalia pale vitu vilipoondoka hama kuanza kuwatesa!
Ni vizuri maisha yako uyaweke katika mikono salama ( Mungu ) ni sawa na kupanda mti katika chemichemi isiyokauka jua liwake liwakavyo bado utaendelea kuyafurahia maisha yako na Mungu siku zote.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………….…………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni