
Karibu tena katika
nafasi ya pili tukiendelea kuhusu swala zima la MAUSIANO, kwakua limekuwa janga
na changamoto kubwa katika jamii tuliyonayo kwa kiasi kikubwa na kuzaa matokeo
ambayo yameleta muonekano wa pande mbili yaaani POSITIVE SIDE au NEGATIVE
SIDE,yote juu ya yote bado tunaona ni matokeo ya yanayotekea katika dunia.
Katika kuendelea na
maswali ili kupata hali uelewa wetu hivi kweli unaweza kujishawishi au
kushawishika na hata kushawishiwa katika kuingia katika mausiano……….wakati mwingine watu ufurahia au huzunika na wengine
walisema kwamba hawakuwa katika utayari wakuingia katika hayo mausiano lakini
kutokana na kushindwa kuimiri katika nguvu ya ushawishi kutoka katika upande
mwingine wamejikuta wameingia pasipo hiyari yao wenyewe!
Hivyo kutokana na dhana
hiyo wako watu wanaojilaumu wenyewe kwa kukubali kushawishika na wako watu
wanawalaumu watu ambao waliwashawishi na kufikia katika hali walio kuwa nayo,
na wakati mwingine watu wanapoanza uhusiano wao wanakuwa na furaha kubwa pasipo
mashaka yoyote na wala kutojua kama ipo siku ambayo watachukizana na kuwa kama
maadui wakubwa ambao kama hawajawai kuwepo katika dunia.
Ni kweli matokeo
yanapokuwa mabaya katika mapenzi ya wahusika basi kinachofuata hapo ni uhasama
wa kudumu na ni watu wa chache tu ambao wanaachana na bado wakaendelea kuusiana
kama marafiki katika mausiano mengine mbali na uhusiano uliokuwako hapo
awali……na wapo ambao wanadumu katika hili na wako ambao wanashindwa kuimiri
kuwa mbali na baadaye kuamua kurudiana tena!
Na amini kabisa yako
maumivu makali sana kati ya watu wawili waliopendana sana na baadae kutengana
pamoja na hayo yote hayo maumivu hayamshindi YESU alipokuwa msalabani akibeba
dhambi za dunia na kututoa mateka katika ufalme wa giza.
MAMBO YA MSINGI KATIKA KUYAJUA
KABLA KUCHUKUA MAAMUZI SAHIHI YA KIMAPENZI
I.UTAYARI
WA KIMWILI
II.UTAYARI WA KIUCHUMI
III.UTAYARI WA AKILI
IV.KIBALI KATIKA MOYO WAKO
V.KIBALI CHA MUNGU
Haya ni mambo matano
ambayo nitaenda kuyanyambua ilikuleta mwanga zaidi katika maamuzi yako na
kuleta ujasiri katika maamuzi yako! Na kuwa msaada kwako au katika rafiki zako
unaowapenda.
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson……………………………………………0764 018535