ANAIJUA
KESHO YANGU
Hakuna kitu kizuri kama
kuwa na KESHO yenye uhakika, yenye matumaini mema yenye furaha ya kudumu, yenye
maisha mengine yenye daraja linguine lilibeba jambo jema katika maisha yako.
Hakuna mtu mzuri ambaye
unaweza kukaa nawe katika furaha na kujiamini kama mtu anaye ijari kesho
yako……..na katika dunia ya sasa watu wengi wana amini kuwa kesho inatengenezwa
na leo na hasa wako watu wengine wana amini pia kuwa kesho inakutegemea wewe!
Ni jambo la kawaida kwa
mtu anapoona kesho yake itakuwa ni nzuri au imebeba jambo jema kwa mtu mathalani mfanyakazi uweza kujibidisha
sana pindi anapo ahidiwa kitu kizuri ambacho kitaboresha maisha yake…mfano bosi
akamwambia mfanyakazi wake akisema kama ukiendelea na moyo huu kufanya bidii
katika kazi nitakupa nyumba,gari au mshahara uliobora zaidi.
Na wengine uweza
kushusha bidii zao katika kazi pindi anapotambua kesho yake haina mabadiliko
chanya au manufaa katika maisha yake, uwa katika kipindi hiki mtu uweza kuacha
kazi anayoifanya………..hauwezi kuendele mbele tu wakati ukijua mwisho wa njia
yako kuna shimo litakalo hitimisha maisha yako.
Hakuna jambo la maana
sana kama kutambua yuko mtu anayeitambua, kuijali na kuithamini kesho yako ni
jambo linalo kukupa kushinda hata kabla ujapigana!
Lazima utambue kuwa
yuko Mungu anayeipenda kesho yako na kutaka kuwa ya maana zaidi
unavyofikiria……….japo wakati mwingine tunaona sisi kuijali kesho yetu kuliko
yeye ambaye anairuhusu kesho ije kwa ajili yako.
Ni seme wazi kuwa kesho
yako hauwezi kuielewa na kuibeba na hata kuistahimili pasipo Mungu kuweka wazi
kwako…….mkulima japo anaamini baada ya kulima katika kufuata kanuni za kilimo
chenye tija lakini bado anaweza asiifurahie kesho yake kwani matatizo mengi
yanaweza kujitokeza mfano mafuriko na kuondoa mazao shambani na kupeleka mtoni,
wakati mwingine unapozalisha vizuri unaweza ukakosa soko la kuuza, hata mkono
wa serikali ukashindwa kukutoa pale ulipo kwa kununua yale mazao na hatimae
ukabaki na yohayo mazao na hatimae kuoza na kupata hasara baada ya kupata
faida,
Hivyo kuanza vizuri sio
kuonyesha kutakuwa na ishara nzuri ya kuendelea katika ustawi wake bali vyote
vinamtegemea Mungu!
Hivyo ni seme kesho
yako uiweke mikononi mwa Mungu haijarishi nini kitatokea baki hapo kwa kua
katika yeye hakuna maumivu bali kuimarisha, hakuna kuachwa bali kuna
kukumbatiwa, hakuna kutengwa bali sikuzote kuna kukumbukwa ndo mana Mungu anasema mama anaweza kumsahau mtoto
anyonyae lakini yeye hawezi kumsahau mtu wake na kamwe hawezi kukusaliti
kwa kuwa ndani yake hakuna kisasi.
Wako watu wanaiweka
kesho yao katika mali,wenzi na hata ndugu wa wapendao hivyo kuyaweka maisha yao
rehani kwakua hao wote wana kesho yao na inaweza kuwa kuwa ni tofauti na kesho
yako………..naomba ni kuhakikishie kuwa hakuna mtu anaweza kuitunza kesho yako
kwakua kila mtu anahitaka kesho yenye manufaa yaliyo bora na yenye mantiki na
katika hali hiyo unaweza kuwa na mtu ambaye mnashindana katika kuitafuta kesho
iliyo bora, sio kesho ya maana sana pindi unaweza mkatembea na msichana
mwenzako wote mkawa na kiu inayo fanana katika hayo pakawa shida kutoelewana
baada ya kusaidiana mkawa mnakandamizana!
Lazima
ujue kesho yako nzuri ni fahari ya Mungu!!
Imeandaliwa
na:
Cothey Nelson…………………………………………..0764
018535
ANAIJUA KESHO YAKO MWACHIE
AINDAE!!!