Jumanne, 1 Septemba 2015

KUMTEGEMEA MUNGU



KUMTEGEMEA MUNGU


 Mathayo 15:8

“ watu hawa uniabudu kwa kinywa tu lakini mioyo yao iko mbali nami”

Hakuna jambao ambalo Mungu analitafuta/mtu anayemtafuta kama mtu ambaye anamtegemea yeye!!

Mshangao Mungu katika dunia ya sasa!

Ni sawa baba aliye na mtoto ambaye rika la mtoto bado linatakiwa liwe chini ya uangalizi wake lakini yeye anataka ajitegemee mwenyewe pasipo kujua au kuwa na upeo wa kujua kuwa maisha ni nini? Bila shaka hilo litakuwa swali kubwa ndani ya moyo wa baba kwa kutaka kujua kinagaubaga kwa nini mwanangu anafikiria aanze kujitegemea wakati bado rika lake linaitaji kuwa chini ya uangalizi wangu.

Nikubaliane kuwa yako mambo mengine yanatokea katika maisha yetu ambayo sio mpango wa Mungu kabisa lakini tumekuwa tukijifariji tu……..lakini ukweli tumekuwa tukitegemea kitu ambacho akipo au hatukijui vizuri hama ambacho hatuna uhakika sana na mwisho tumekuwa katika mazingira tofauti na ndoto zetu.

Kumtegemea Mungu sio jambo lelemama ukiwa hapa duniani kwani dunia inahitaji uitegemee yenyewe ili ikupe kile inachofikiri kukupa……..nguvu ya dunia imekuwa ikiwavuta wengi  na kusahau kwamba imetupasa kumtegemea Mungu kwa asilimia zote hivi sasa wako watu wanawategemea wachungaji wao, marafiki na mtu ambaye anaamini kuwa atanisaidia lakini uwezi ukalinganisha mtu anayemtegemea Mungu na mwingine asiye mtegemea bali anategemea vitu vingine.

Nyimbo nyingi zime imbwa na kupendwa na watu wengi  katika ujumbe wa kuonyesha faida ya kumtegemea Mungu lakini ukweli baada ya kuimba na kucheza na hatimae kutoka jasho tukaacha hapohapo kwa kujua kuwa kumtegemea Mungu ni nyimbo na wala sio maisha ( nyimbo kugusa hisia zako sio kumtegemea Mungu).

Ukweli katika dunia ya sasa wako watu ambao kwa muonekano na  wingi wa maneno yao unaweza kuona au kuamasika na hata kushawishika kuwa watu hawa wana mtegemea Mungu lakini ukweli muonekano wa mtu na namna mtu anavyojieleza sio dalili au ishara nzuri ya kuonyesha kuwa huyu anamtegemea  Mungu na huyu amtegemei Mungu.

Ujumbe huu hauko katika kuwapima watu na kutambua nani anamtegemea Mungu na nani amtegemei Mungu, bali ni kuonyesha maisha ya sasa yalivyoenda mbali na kumtegemea Mungu hivyo na kukuhatarisha kuwa makini sana katika dunia ya leo hivyo kutambua kwa uhalisi au kwa uhakika namna ya kumtegemea Mungu.

Ukweli kumtegemea Mungu kupo na kunawezekana na kunatenda kazi ni wewe kuamua sasa na anza kumtegemea Mungu kwani hapo ndipo kunazaliwa mkristo ambaye kwa uhakika Mungu ndiye anayemtaka na anamtafuta ili amfanyie ibada ambayo anajua kwa uhakika itampendeza yeye na kuimarisha mausiano yao.

Niseme tu hakuna maisha ya ushindi kwa uhakika mbali na kumtegemea Mungu na kwa namna hiyo ukristo unakuwa wa maana na tishio kubwa katika upande wa giza kwa wewe kuishi maisha ya kumtegemea Mungu.

Lazima ujue uwezi kuondoka katika maisha ya utumwa kwa kuombewa tu au kutabiriwa tu japo mambo yote sio mabaya lakini jibu la uhakika ni kuishi maisha ya kumtegemea Mungu kuliko na udhibitisho wake na sio mtu mwingine.

Kumtegemea Mungu ni kuishi na Mungu kwa namna anavyokukuelekeza au maisha yasiyo na uhai wa akili ya kibinadamu,maisha yaliyo jaa kiu ya kutembea na hatua za Mungu. Haya ni maisha ambayo hayafuati watu waliishije bali mimi ninatakiwa niishije!

Yoshua 1:1-9

Kumtegemea Mungu tunaona yoshua wakati anaachiwa kijiti na Musa…… kipindi cha Musa alipewa fimbo na wingu lilikuwalikimuongoza katika safari yake na Israeli lakini yoshua alipewa neno la Mungu liwe dira yake katika utendaji wake na katika muongozo wake. Yoshua alikuwa na mwendo mwingine na Mungu katika kuyafikia malengo ya Mungu aliyaweka katika maisha yake….!

Uwezi ukamtegemea katika hali ya kubahatisha lazima pawepo na muongozo wa uhakika ukikuongoza kutoka hatua moja na kwenda hatua nyingine inabidi iwe ni ya uhakika na muongozo ulio salama usio sitasita………………..!

Kama kweli unataka kuondokana na changamoto zinazokukabili basi tafuta kwa bidii namna sahihi ya kumtegemea Mungu! Maana hapo ndipo palipo na tulizo lako na furaha ya kudumu.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………0764 018535

Maoni 2 :

  1. ipi ni namna sahihi ya kumjua Mungu?

    JibuFuta
  2. ili mjue Mungu katika njia sahihi!

    lazima uwe na maisha na Neno la Mungu pia Roho mtakatifu akufunulie katika utendaji wake.

    JibuFuta