KUMTEGEMEA MUNGU
Mathayo 15:8
“ watu hawa uniabudu kwa kinywa tu lakini
mioyo yao iko mbali nami”
Hakuna jambao ambalo Mungu
analitafuta/mtu anayemtafuta kama mtu ambaye anamtegemea yeye!!
Mshangao Mungu katika dunia
ya sasa!
Ni sawa baba aliye na mtoto ambaye
rika la mtoto bado linatakiwa liwe chini ya uangalizi wake lakini yeye anataka
ajitegemee mwenyewe pasipo kujua au kuwa na upeo wa kujua kuwa maisha ni nini?
Bila shaka hilo litakuwa swali kubwa ndani ya moyo wa baba kwa kutaka kujua
kinagaubaga kwa nini mwanangu anafikiria aanze kujitegemea wakati bado rika
lake linaitaji kuwa chini ya uangalizi wangu.
Nikubaliane kuwa yako mambo
mengine yanatokea katika maisha yetu ambayo sio mpango wa Mungu kabisa lakini
tumekuwa tukijifariji tu……..lakini ukweli tumekuwa tukitegemea kitu ambacho
akipo au hatukijui vizuri hama ambacho hatuna uhakika sana na mwisho tumekuwa
katika mazingira tofauti na ndoto zetu.
Kumtegemea Mungu sio jambo
lelemama ukiwa hapa duniani kwani dunia inahitaji uitegemee yenyewe ili ikupe
kile inachofikiri kukupa……..nguvu ya dunia imekuwa ikiwavuta wengi na kusahau kwamba imetupasa kumtegemea Mungu
kwa asilimia zote hivi sasa wako watu wanawategemea wachungaji wao, marafiki na
mtu ambaye anaamini kuwa atanisaidia lakini uwezi ukalinganisha mtu
anayemtegemea Mungu na mwingine asiye mtegemea bali anategemea vitu vingine.
Nyimbo nyingi zime imbwa na
kupendwa na watu wengi katika ujumbe wa
kuonyesha faida ya kumtegemea Mungu lakini ukweli baada ya kuimba na kucheza na
hatimae kutoka jasho tukaacha hapohapo kwa kujua kuwa kumtegemea Mungu ni
nyimbo na wala sio maisha ( nyimbo kugusa hisia zako sio kumtegemea Mungu).
Ukweli katika dunia ya sasa
wako watu ambao kwa muonekano na wingi
wa maneno yao unaweza kuona au kuamasika na hata kushawishika kuwa watu hawa
wana mtegemea Mungu lakini ukweli muonekano wa mtu na namna mtu anavyojieleza
sio dalili au ishara nzuri ya kuonyesha kuwa huyu anamtegemea Mungu na huyu amtegemei Mungu.
Ujumbe huu hauko katika
kuwapima watu na kutambua nani anamtegemea Mungu na nani amtegemei Mungu, bali
ni kuonyesha maisha ya sasa yalivyoenda mbali na kumtegemea Mungu hivyo na kukuhatarisha
kuwa makini sana katika dunia ya leo hivyo kutambua kwa uhalisi au kwa uhakika
namna ya kumtegemea Mungu.
Ukweli kumtegemea Mungu kupo
na kunawezekana na kunatenda kazi ni wewe kuamua sasa na anza kumtegemea Mungu
kwani hapo ndipo kunazaliwa mkristo ambaye kwa uhakika Mungu ndiye anayemtaka
na anamtafuta ili amfanyie ibada ambayo anajua kwa uhakika itampendeza yeye na
kuimarisha mausiano yao.
Niseme tu hakuna maisha ya
ushindi kwa uhakika mbali na kumtegemea Mungu na kwa namna hiyo ukristo unakuwa
wa maana na tishio kubwa katika upande wa giza kwa wewe kuishi maisha ya
kumtegemea Mungu.
Lazima ujue uwezi kuondoka
katika maisha ya utumwa kwa kuombewa tu au kutabiriwa tu japo mambo yote sio
mabaya lakini jibu la uhakika ni kuishi maisha ya kumtegemea Mungu kuliko na
udhibitisho wake na sio mtu mwingine.
►Kumtegemea Mungu ni kuishi na Mungu kwa
namna anavyokukuelekeza au maisha yasiyo na uhai wa akili ya kibinadamu,maisha
yaliyo jaa kiu ya kutembea na hatua za Mungu. Haya
ni maisha ambayo hayafuati watu waliishije bali mimi ninatakiwa niishije!
Yoshua 1:1-9
Kumtegemea Mungu tunaona
yoshua wakati anaachiwa kijiti na Musa…… kipindi cha Musa alipewa fimbo na
wingu lilikuwalikimuongoza katika safari yake na Israeli lakini yoshua alipewa
neno la Mungu liwe dira yake katika utendaji wake na katika muongozo wake.
Yoshua alikuwa na mwendo mwingine na Mungu katika kuyafikia malengo ya Mungu
aliyaweka katika maisha yake….!
Uwezi ukamtegemea katika
hali ya kubahatisha lazima pawepo na muongozo wa uhakika ukikuongoza kutoka
hatua moja na kwenda hatua nyingine inabidi iwe ni ya uhakika na muongozo ulio
salama usio sitasita………………..!
Kama kweli unataka kuondokana
na changamoto zinazokukabili basi tafuta kwa bidii namna sahihi ya kumtegemea
Mungu! Maana hapo ndipo palipo na tulizo lako na furaha ya kudumu.
Imeandaliwa
na:
Cothey Nelson……………………………………………0764
018535
ipi ni namna sahihi ya kumjua Mungu?
JibuFutaili mjue Mungu katika njia sahihi!
JibuFutalazima uwe na maisha na Neno la Mungu pia Roho mtakatifu akufunulie katika utendaji wake.