Ijumaa, 31 Desemba 2021

DUH! KUMBE THAMANI YA JANA HAIPOTEI KWA SABABU YA LEO.

 


Ni jambo jema na zuri kuwepo kwa mabadiliko hasa chanya katika mambo mbalimbali yanayoendelea katika ulimwengu huu, kwasababu hayo mabadiliko ndiyo yanapelekea mafanikio/ maendeleo mengi katika dunia tuliyonayo ya kianza katika jamii husika na hatimaye kuenea ulimwenguni mathalani maendeleo ya sayansi na teknolojia yalivyo pelekea urahisi wa mawasiliano na hata kurahisisha kwa usafirishaji wa watu pamoja na bidhaa kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine na faida nyingine nyingi ambazo unapoziona unaona maajabu ya akili ya Mungu kwa mwanadamu.

Kwa Afrika kwa asilimia kubwa tunashukuru Mungu  kwa sababu tulivyokuwa jana sio tulivyo leo hasa kwa upande wa mavazi , mavazi ya enzi hizo sio tunayovaa sasa japo tunayafurahia na kumshukuru Mungu kwa hilo ingawa yameboreshwa hata kupitiliza maana siku hata siku mitindo inakuja ya hatari zaidi na hata material ( malighafi ) ya tofauti tofauti kulingana na wazo ( idea ) ya mtengenezaji ( designer ) wakati mwingine nguo za kulalia zinakuwa za kutokea hapo na wanyoshea mikono mafundi “ designer “  wetu! Hakika kweli wakati tunaenda nao vizuri

Ni kweli jana na leo zote ni siku ila zinatofautiana kwa majira yake kama sio kwa tarehe.

Natambua tunamtambua umuhimu wa mkunga baada ya kumsaidia mjamzito kujifungua salama.

Na mwanafunzi wanatambua umuhimu wa mwalimu baada ya kufaulu maana sio rahisi kwa mwanafunzi aliyefeli akamtafuta mwalimu na kumwambia asante kwa kunifundisha!

Japo ni vizuri kumkumbuka mwalimu hata kama ujafanikiwa kufanya vizuri maana kuna maarifa fulani umeyapata kutoka kwake.

Ni muhimu sana kutokusahau jana kwasababu imekuja leo, kwasababu sio vitu vyote ulivyojifunza jana kuwa leo havitatumika tena.

Kwani hata chakula kilichobaki jana kinaweza faa leo ( baadhi ya familia ) ni muhimu tu ukiandae vizuri kitumike leo tena na kwa asilimia kubwa chakula kilicho lala uitwa kiporo na wengine ukifurahia sana.

Ni muhimu utambue mambo yako ya jana ambayo upaswi kwenda nayo leo na vilevile yako ya leo haupaswi kuyakataa kwa kuwa yanaweza yasikifae ila yaka mfaa mwingine na mengine yanaweza yasiwafae wote ya kaja na kupita.

Naam hata utandawazi unaokuja leo tusisahau asili yetu ya jana! Kwa kuwa kupitia utandawazi unaweza kuona mambo mbalimbali hivyo usione kila kitu kinachoonyeshwa na kupitia mtandao basi kinafaa kuwa sehemu ya maisha yako.

Wako watu wanakosoa jamii yao kwakuona kutembea katika asili yake ni kupotoka au kutoheshimu hadhi yake lah! Katika mabaya unayo yaona yako mema usiyoyaona au uliyoyasahau.

Tambua ni hao watakao kukumbatia na kukusitiri na hata kukuzika pindi utakapo pumzishwa katika nyumba yako ya milele na sio wale unaowafuata utamaduni wao!

Haijalishi kama unawajua kiasi gani japo uko mbali ( utandawazi ) jua lako litabaki kuwa lako tu na hapo awatajali kuwa wewe ni shabiki wa utamaduni wao au la!

Sio kila kitu kinacholetwa mezani kwako ukachukua na ukala lazima uangalie kwa umakini je! Hicho chakula akitaathiri afya yangu ulimbukeni usikutese.

Ni vizuri unapofanya jambo lazima liwe jema machoni pa jamii yako hasa likiwa lililo chanya kwako.

Unapokuwa kijijini ishi kama mwanakijiji na unapokuwa mjini basi ishi kimjini basi hapo utakuwa bora kwa jamii yote zaidi sana mpende Mungu.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………………………..0764 018535

Ijumaa, 10 Desemba 2021

MUNGU ANATAKA KUJIONA YEYE!



Ni kawaida tu, kibinadamu kila mtu yeyote pindi anapojingalia kwenye kioo, upenda kujiona yeye na wala sio mtu anayefanana na yeye na wala sio yeye!

Katika mambo ambayo yanayomfurahisha Mungu kama sio kumpendeza ni pindi anapomuona mwanadam anapenda ajione yeye katika kila kitu kinachohusu maisha yake afya, uchumi na mambo yote ya kijamii.

Pindi anapojiona yeye katika maisha ya mwanadamu basi hapo udhihirisha kuwa huyo ni mali yake hata bila kusema kwa mtu husika kuwa yeye ni mali ya Mungu.

Lengo kubwa la Mungu kukufanya ni kutaka utambue na kumpa heshima kama Mungu na wala sio kitu kingine.

Ndomana anapoona utendaji wako mkubwa wa akili katika mambo yanayo kukabili upenda kukuacha ili utukufu wake usichanganyike na uwezo wa kibinadamu.

Namna nyepesi ya kumruhusu Mungu atawale/ahusike na shida hama jambo lako ni kutokuwa na nia ya kuwa komoa watu bali kuhakikisha Mungu anaonekana na kuwa unakuwa kwa faida yake.

Mtihani mkubwa unakuja pale namna gani Mungu anataka aonekane katika kile unacho/kinachokukabili inawezekana kazi pengine wewe ungependa kuendelea hapo ili wale wanaokuchukia wakuone, hivyo ukawa unafunga na kuomba katika hali hiyo lakini Mungu pengine anataka uondoke hapo ili utukufu wake uonekana huko unakokwenda! AU kuna mabaya yatakuja kwenye ofisi hiyo ambayo yanaweza kuweka maisha yako rehani.

Mathalani,Daudi alikuwa anaomba ili mwanae apone na aliacha hata kula ili amshawishi Mungu afanye kitu kwa ajili ya kunusuru uhai wa mwanae lakini Mungu akutaka kuonekana kwa namna hiyo ambayo sawa na matakwa yake.

Watu wengi wanakata tama kwa kutojua namna gani Mungu anataka aonekane katika yale yanayo kukabili, mathalani wengine walitegemea afanye leo lakini Mungu alipendezwa kufanya kesho kutwa hivyo akili ya Mungu na mtu zikatofautiana, naye akashindwa kukubaliana na tofauti hiyo.

Pindi unapotambua namna gani Mungu anataka ajionyeshe kwa watu kutokana  na yale yanayo kukabili ushindi unakuwa ni haki yako mathalani wanaisraeli walipokuwa wakipigana vita Mungu aliwapa ushindi kwa namna mbalimbali sawa na namna yake au alivyokuwa anataka wakati mwingine waliimba na ushindi ukapatikana na mara nyingine Musa kwa kunyoosha mkono Israel walishinda n.k

Ukitaka kushindana na Mungu au kuchelewa katika hatua yako basi tafuta namna yako tofauti na mpango wake au alivyokusudia.

Moja ya kitu ambacho Mungu anataka akione yeye kwako pindi unavuka salama au kushinda vita ni watu wamuone yeye katika huo ushindi na sio wewe kutaka wakuone wewe! Mungu anaweza kubatili huo ushindi au usijirudie tena katika hatua inyofuata.

Unahitaji kujua Mungu anataka kujiona yeye katika maisha yako na sio mtu mwingine ili aweze kuwa Mungu kwako kwelikweli na kuchukua shida yako pamoja na kuwa furaha yako katika siku zote za maisha yako.

Unahitaji kujua Mungu anataka aonekane katika jambo lolote linalo kukabili hivyo kumruhusu aonekane kama anavyotaka ni kumshawishi atende .

Muhimu katika yote, ni vizuri utambue pindi Mungu atakavyojionyesha bila shaka nawe UTAONEKANA TU! Usiwe na haraka.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………….0764 018535

Ijumaa, 26 Novemba 2021

MUNGU ANAJUA

 



Pindi unasikia neno hili “ Mungu Anajua” uwa huna mashaka hata kidogo na moyo wako unasema ni KWELI, maana hakuna kificho mbele za Mungu....maana yeye anajua hata utawaza nini baada hilo la sasa unalowaza!

Kujua ni uhuru na ushindi wa kufanya mambo mengi na kuto kujua utumwa usio wa hiari unaokupeleka mahali pengine usipotaka kwenda!

Naam!

Ni kweli umeshiba leo lakini Mungu anajua pia utahitaji kula kesho.

Ni kweli una nguvu leo maana ni kijana lakini Mungu anajua kesho yako maana nguvu zako zitaisha maana utakuwa ni mzee.

Karibu!

Moja ya kitu kinachosababisha watu kukata tamaa hama kukosa matumaini ni kutojua kuwa Mungu anajua na anaelewa vizuri sana.

Katika dunia tuliyonayo wako watu baada ya kuachwa na wapenzi wao wanafikiri kujiua ndio dawa ya kuficha aibu yao, pia wako watu walioachishwa kazi au madili yao kuharibiwa na hata kupelekea kucheleweshwa mipango yao, wengi wamekata tamaa na kuhisi wana mikosi na wanaona kama Mungu AJUI!

Ni muhimu utambue kuwa akili yako inapokosa majibu haina maana kuwa Mungu amekosa majibu, ikiwa maisha yako umeyakabidhi kwake jua kila jambo linalotokea limebeba hatima kubwa njema katika maisha yako. ( Mungu yeye anajua mwisho tangu mwanzo )!

Wakati mwingine uwa tunalia kwasababu atukutegemea yatokee yale yalitokea hasa kwa yale yanayoonekana  mabaya lakini kwa Mungu sio kitu au jambo la kushangaza kwake.

Na muhimu tutambue utofauti wa akili zetu na Mungu ndo maana yeye anaitwa Mungu na sisi wanadamu.

Pia kuna wakati mambo yanaweza kutokea katika maisha yako ukajua Mungu yuko na mambo mengine kabisa wala akufikirii wewe, hivyo unaweza kuzidi kuwa chini kwa kukosa mwelekeo uliosahihi.

Uwa Mungu anajua sio kwa kuwa una matatizo tu bali anajua hata jambo lingine likikutokea na namna gani ya kuwa salama hapo.

Ni maisha mawili haya ukiishi, kuishi katika mazingira uku ukijua Mungu anajua kinachoendelea na wewe hama ajui kitu au chochote kinachokuhusu wewe, wakati mwingine ni kweli inaweza kukupa wazo hilo kutokana na mazingira lakini ukweli haupo hivyo.

Katika maisha haya kuna uwezesho mkubwa wa Mungu wa ajabu pindi unapojua katika hali ngumu inayokuzunguka Mungu anajua utatoka vipi!

Hauhitaji maombi mengi sana ili utoke ulipo kuwa bali unahitaji akili yako ikubaliane kuwa Mungu anajua na uwe tayari kufuata njia zake ili utoke hapo ulipo.

Nikubaliane tu, uwa ni ngumu tu kujua hasa kama Mungu anajua kinachoendelea katika maisha yako!

Yesu “ mimi ndimi ufufuo na uzima “-lazaro.

Yohana 11:1 Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake.

 2 Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi.

 3 Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi.

 4 Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.

 5 Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro.

 6 Basi aliposikia ya kwamba hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo.

 7 Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena.

 8 Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena?

 9 Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.

 10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake.

 11 Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha.

 12 Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona.

 13 Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala usingizi.

 14 Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa.

 15 Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini; lakini na twendeni kwake.

 16 Basi Tomaso, aitwaye Pacha, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twendeni na sisi, ili tufe pamoja naye.

 17 Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne.

 18 Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu, kadiri ya maili mbili hivi;

 19 na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao.

 20 Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani.

 21 Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.

 22 Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa.

 23 Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka.

 24 Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.

 25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;

Usihisi mambo yanaweza kukuchanganya basi ukajua na Mungu yana mchanganya sawa na akili yako inavyo waza bali Mungu uwa anaona njia mahali panapoonekana giza.

Unapoyaendea mambo/kuyakabili mambo huku ukijua kuwa Mungu anajua na hali hii bado nitatoka salama na ushindi ni haki yangu.

Katika mazingira yeyote upaswi kujiweka chini lazima roho yako iwe na nguvu kwa kuwa MUNGU ANAJUA ULIPO NA UNAPOENDA!

Mashaka wala uwoga sio fungu lako!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson..............................................................................0764 018535

Ijumaa, 12 Novemba 2021

MSIKIE MUNGU

 



Na moja ya kitu kinacholeta furaha kwa mtu ni pale anapotambua ANASIKILIZWA hapo ndipo kiu inaweza kukatika bila maji, njaa inaweza poteza nguvu yake bila ya chakula.

Endapo utafanikiwa kujua namna ya kumsikiliza Mungu nawe ukawa mwaminifu kumsikiliza, basi hapo utauteka moyo wake! Utaupendeza moyo wake.

Japo kuna vitu vinataka kusikilizwa na wewe na vinajiona vinasababu ya kusikilizwa na wewe! Hivyo unahitaji kujidhatiti katika kuitumikia sauti ya Mungu.

Kuna vitu vingine ukivipa sikio lako unaweza usitoke salama lakini sio kutoa moyo wako katika kusikia sauti ya Mungu ni hakika utakuwa salama milele.

Ukitaka kuifikia hatma ya wanadamu basi endelea kuwapa sikio lako ila endapo ukitaka kuifikia hatma ya Mungu juu ya maisha yako basi mpe sikio lako lote! Uchaguzi ni wako.

Ukweli katika uwanja wa kusikiliza unavipingamizi vingi: kujisikiliza, kuisikiliza dunia na kumsikiliza Mungu.

Kumsikiliza Mungu kwa njia nyingine tunaweza sema ni kupata ustawi unaotokana na Mungu kwa namna yake unaozaliwa ndani ya sauti yake.

Kiukweli Mungu kwako ahitaji vitu vingine maana vyote ni vyake na akihitaji anavipata bali kitu anachokitaka kutoka kwa ni kuona moyo wako unamsikiliza yeye.

Kama kweli unataka kuwa kipenzi cha Mungu basi jifunze sana namna ya kumsikiliza.

“ mtu atayekayefanya mapenzi yangu” Matendo 13:22

Yohana 4:34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.

“ chakula changu ndicho hichi ni yatende nikamalize”

Unaweza ukatembea na manabii na ukaishi kwenye sauti zao lakini unaweza usiwe nabii lakini uwezi kutembea kwenye sauti ya Mungu usipate maatamio ya kiMungu.

Na muhimu utambue Mungu anaifurahia dunia kwa uwepo wako na uwepo wako unakuwa na thamani zaidi kwakuwa unaishi katika sauti ya Mungu.

Moja ya kitu kitakachoweza fanya ili watu waweze kukusikiliza ni muhimu sana ujifunze kumsikiliza Mungu ili yeye akuanganishe na watu wako.

Kuna wakati mwingine unakuwa katika hali ngumu unaweza tamani hata kusikia neno la mtu ili liweze kuchangamsha moyo wako angalau upate faraja kwa kipindi lakini hapo ujue unahitaji kuisikia sauti ya Mungu ili ikupe mwelekeo wa kutoka hapo ulipo.

Naam moja ya sauti isiyochosha kusikia wala kukinai ni kusikia sauti ya Mungu maana kila wakati usikiapo katika masikioni inakupa uwanja mwingine wa ushindi.

Nani vizuri utambue ushindi wa Mungu katika maisha yako unazaliwa ni baada ya kusikia sauti yake hapo neema ya uwezesho uachiliwa katika kufanikisha jambo husika.

Na ishara ya kumpenda Mungu uwa inaoneka au dhihirika pale utakapo amua kumsikia.

Na Mungu anataka apate uhakika wa kuwa utasikia kisha achilie Baraka zake kwako!

“ msikilize akusikilize”

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………0764 018535