Jumatano, 31 Desemba 2014

KUNATOFAUTI KUBWA KATI YA MIEMKO YA MWILI NA NDOA





KUNA TOFAUTI KUBWA KATI YA  MSUKUMO WA NDOA 
 ( MIEMKO YA MWILI) NA NDOA YENYEWE!!!




Ni kweli jambo lolote ambalo unaliingia ni wazi kabisa lazima uone haja ya jambo hilo na endapo hutaona haja ya jambo hilo ni wazi hautaitendea haki hali yako na nafsi yako binafsi. Ni kweli ndoa ni jambo la heri sana lakini ni pale tu utatambua kwa usahihi uku ukisaidiwa na Mungu mwenyewe katika kukuwezesha kuyafikia yale uliyo yakusudia.

Katika dunia ya sasa ndoa nyingi zimekuwa ni safari au mapitio tu lakini sio maisha ya wawili hao ya milele, tumekuwa tukishuhudia harusi kubwa lakini mwisho tukiona upweke ukiendelea kuthibitika au watu wakiama kutoka kwa mtu mmoja na kwenda kuanzisha ndoa na mtu mwingine, watu wengi wamekuwa wakiishi katika ndoa kwa misingi mfumo wanaojua wao mathalani mfumo dume, mila na desturi.

Vijana wengi wanaona kuwa sio rahisi kuishi pasipo kuwa na mwenzi ili kuweza kupunguza makali ya mwili au kwenda sawa na miemko ya mwili inafika kipindi ambacho watu hawaaminiani wala kukubaliana kuwa kunauwezo wa kuvimudu vishindo vya mwili katika mabadiliko yao. Wako watu katika kupunguza miemko yako katika mwili katika kwenda kwa dada poa( changudoa) na wengine kutokana na kuogopa maradhi mbalimbali wamekuwa wakishaurina kuwa basi waoe ili waweze kumudu miemko yao katika miili yao.

Niseme wazi miemko katika mwili ni muhimu sana japo sio kigezo cha wewe kuingia katika ndao ningependa kusema kuwa miemko katika mwili wako ni ishara tu mwili wako kujiweka sawa kutokana na hatua uliyonayo kwani kuna hatua ya watoto kuna kuota meno na mengine mengi lakini kuna hatua ujana katika kuimalika na homoni kujipanga katika hali stahiki ni kitu kizuri sana hivyo napenda sana kusema miemko ni maandali yaliyo katika mwili na sio kigezo cha maandalizi ya ndoa, maandalizi ya ndoa yana husisha maandalizi ya AKILI na UCHUMI na sio mabadiliko ya mwili.

Tumeona ndoa nyingi za watoto wakiingia katika ndoa pasipo kujua wapo katika ndoa bali msukumo wao mkubwa unategemea sana msukumo wa mwili katika kuingia katika ndoa, niseme wazi ndoa ni zaidi ya adhabu ya kihama endapo hauta ielewa au hautua kubali kuelewa inaweza kuwa ni zaidi ya majanga lakini ukiingia katika hali stahiki inakuwa nizaidi ya asali au chochote.

Lakini watu wengi wamekuwa wakiingia katika ndoa kutokana na ushauri na rafiki wanaowazunguka katika kuwaambia kuwa mmeshakua mnafaa kuishi na mwanamke na wanaweza kukuaminisha kuwa utaweza tu tena wengine wanaweza kukusifia kwa upeo ulionao.

Nipende kusema kuwa mabadiliko ya mwili ukuanza wewe na wala Mungu akuweka mabadiliko ili uingie katika ndoa.

Lazima ujue miemko ni ishara ya kukua lakini sio swala la kusukma kuingia katika ndoa kwani inaweza kuwa ni jambo zaidi ya hatari kwakua KUJUA KUSIMAMA SIO KUJUA KUKIMBIA.
Ni wazi swala zima la ndoa lina muhitaji Mungu kupita kawaida unavyofikiria na hasa katika dunia ya sasa ilijaa mlundikano wa maisha yasiyo kuwa halisi na wenye ustawi uliokusudiwa.

Miemko ni radha katika ndoa ambayo inaweza kukupa raha kuona uhitaji wa mwezako katika ndoa katika wakati sahihi lakini sio swala la kukuumiza kichwa likaondoa usingizi likaondoa kiu yako na Mungu au bidii katika elimu yako, ni pende kusema kuwa jambo sahihi uja kwa wakati sahihi unahaja ya kukulupuka.


Japo sio kauli nzuri sana kwako lakini kwangu ni nzuri sana inayonipa nguvu NDOA ONA KAMA KIFO.............kama kipo kipo kitakuja tu, kwani kuna mtu anaweza kukikimbilia kifo na kukifurahia ila kama kipo kipo tu.


BARIKIWA RAFIKI!!!!!!!!



 Imeandaliwa na;
      

                          Cothey Nelson....................................................................0764 018535

Ijumaa, 26 Desemba 2014

UNASIKIA




UNASIKIA NINI?




Unapoona mtu anafanya jambo lolote au kuongea jua kama alijaanza ndani yake basi amesikia na kulikubali na kulifanya kuwa sehemu ya maisha yake au kama sivyo basi kusikia kumechochea kitu katika kufanikisha swala Fulani. Lakini leo siitaki kuzungumzia kusikia tu bali na zungumzia unasikia nini kwakua kile unachokisikia kina mchango mkubwa katika maisha yako............kwakua kwa sehemu kubwa mwanadamu ubadilika kutokana na kile anachokisikia na hata kukiona.

Ni ukweli wako watu wanafurahia maisha yao leo kutokana na kusikia jambo Fulani na akalifanya kuwa katika maisha yake  na vilevile wako watu ambao wanalia sana kutokana na kile alichokisikia sasa amekuwa na maumivu katika maisha yake, ni kweli kusikia sio kitu kibaya bali swala unasikia nini! Na kwa nini umeamua kusikia.


Sitazungumzia faida na hasara za kusikia bali nitazungumzia namna kusikia kunaweza kukutengeneza kama vile ilivyokutengeneza leo vile ulivyo, ukweli kuna mambo mengi yanafanyika kutokana na kusikia maneno kutoka kwa mtu mathalani mtu anakuwa mke au mume wa mtu kutokana na maneno ya mwenzi wake au mtu anaingia katika biashara haramu kutokana na kusikia kama vile ukahaba, madawa ya kulevya na mengine.

Ni jambo la kawaida usitegemee kuwa watofauti na jinsi vile unavyosikia kwakua kile unachokisikia ndicho kina kutengeneza wewe na kuwa na nafasi ambayo uko nay oleo, wako watu ambao ni wakubwa sana katika kiuchumi kutokana na kile walichokisikia kuwa katika maisha yao hivyo jua mafanikio yako yame bebwa na nini ukisikiacho..........nikupe mfano mmoja kuna ndugu na mfahamu alikuwa anapenda kufuatilia maradhi mbalimbali katika mtandaoni ikatokea akavutiwa sana kuuelewa ugonjwa wa kisukari hivyo mwisho akajikuta ule ugonjwa unaanza kushamiri katika mwili wake...........! narudia tena sio swala la kusikia tu bali nini unasikia kinaweza kukufanya chochote sawa na zima ya kile ulichokisikia.


Bila shaka umeona watu wakiwalaumu rafiki zao na wengine wakiwalaumu wenzi wao japo sijajua wewe unaye soma ujumbe huu unamlaumu nani au kumshukuru nani kwa kua lazima pawepo na mawili kati ya kulaumu au kukshukuru kwa maana nyingine ikikosekana moja basi kunalingine litafuata haiwezi ukawa tofauti na hapo! Kwa kusema hivi si chochei swala zima la kulalamika au kuchukia bali mimi na zungumzi namna nguvu ya kusikia ilivyobadilisha maisha yako.


PENDA KUSIKIA NENO LA MUNGU WAKATI WOTE

Kwani hilo neno limebeba ustawi wa Mungu katika maisha yako

Imeandaliwa na;
              
                       Cothey  Nelson..........................................................0764 018535

Jumamosi, 20 Desemba 2014

SIKU YANGU



SIKU YANGU;



Ilikwa ni siku ambayo sitaweza kuisahau na wala sihitamani kuikumba kwanamna ilivyotokea. Ilikuwa siku ambayo ilianza kwa furaha sana lakini mwisho ulikuwa tofauti na nilivyoitegemea hakika ilikuwa ni siku ya ajabu na kushangaza sana kwani ilianza kwa kusababisha furaha halafu mwisho ikiwa ni mateso............... nilikuwa na mdogo wangu tukielekea vijijini kwetu ambako tulikumbuka sana na tuna amini sana hata wao walitukumbuka sana pasipo shaka........kwani  wazazi wetu walipiga simu na kuwataarifu ndugu zetu waliopo kijijini Mbeya  walijawa na shauku sana na tarajio kutuona.

Nasi tuliamka mapema sana mimi na mdogo wangu vick tuliamka asubui sana na wazazi wetu walitusindikiza mpaka ubungo na kututakia safari njema na umakini tuwapo safarini na kipindi hicho na kumbuka mimi na mdogo wangu tulikaa pamoja tayari kuelekea kijiji kwetu, na kumbuka safari ilianza asubui mnamo saa 12 asubuhi na kipindi hicho abiria wote walikuwa wamekaaa katika siti zao wakiwa watulivu sana kila mtu akiwa na mawazo tofauti katika kule alikuwa anaelekea wapo walikuwa wanaenda katika shughuli za kibiashara, kidini na kuwatembelea wapendwa wao kama sisi tulibeba hilo kusudi la kuwa salimu ndugu kwani mimi nilitoka mjini Mbeya ni kiwa mdogo sana yapata miaka 3 na sasa narejea ni kiwa na umri wa miaka 25.

Tulipofika Morogoro maeneo ya mbuga ya mikumi gari letu lilipata shida na kushindwa kuendelea na safari yake, hivyo abiria baada ya kusubiri kwa muda wakaanza kushuka taratibu katika kupata hewa nje.........ila mimi na mdogo wangu tuliofia kushuka chini kwani tulikuwa tunakumbuka yale maneno ambayo tulioambiwa na wazazi wetu tuwe makini sana pamoja na kuwa angalifu sana................ITAENDELEA!!!

Imeandaliwa na;

                      Cothey Nelson...............................................................0764 018535

Jumamosi, 13 Desemba 2014

UMASIKINI WA MACHO



UMASIKINI WA MACHO;





Siku zote macho yanaweza kukutia nguvu au kukufanya dhaifu, hali hii inatokea mtu binafsi anapoona mwenyewe hali ya kutoweza au kuogopa na hata kama watu wanaweza kuona tofauti na vile mtu anavyoona. Kwasababu kile anachokiona mtu ndicho kinachokuwa na nguvu katika kutawala katika maisha yake.


Ukiweza kuyaponya macho yako kuona tofauti na hali ilivyo au namna unavyotakiwa kuona basi hapo ndipo kunakushinda au kushindwa, watu wote walioweza kufanya mabadiliko katika dunia na jamii walikuwa na uwezo wa kuondoa umasikini wa macho kwa sababu aliyaelekeza macho yake kuona upande ulio mpelekea njia zaidi kuelekea upande wa kushindwa.

Kuna uwezekano wa kuondoa umasikini wa fikra au akili sio rahisi kuondoa umasikini wa macho kwani umasikini mwingine uondolewa na elimu mpya inayokukubaliana na akili yako lakini huu umasikini wa macho huu unakuwa katika nafsi yako na pengine unaweza kuwa na mali nyingi lakini bado ukawa na umasikini uliokushikilia katika macho yako.

Ninge penda ujue kwamba huu ni umasikini uliotanda giza katika macho yako na hata kama ukitaka kuchukua hatua kutokana na akili yako ilivyoelewa inakuwa shida kutokana na ukamilifu wa moyo katika kukubali hali inakuwa bado ni ngumu sana.

Wakati mwingine umasikini huu wa macho unaondoa hali ya bidii ndani yako na kuwa na shauku katika kufikia ngazi bora kuliko ulipo japo wakati mwingine unaweza kutamani lakini katika kufanya maamuzi yaliyo ubeba moyo inakuwa ni ngumu.na niseme wazi tu kuwa hali hii hakuoni mtu wala hakujui mtu bali ni wewe pekee unayejihukumu na kuona ni mzigo katika maisha yako na wala uwezi kuona fahari ya wewe kumwambia  mtu mwingine kwakua  hata huyo utafikiri kama atakuelewa na kukupa pumziko ndani ya moyo wako. Utabaki nalo moyoni mwako litakua kama mzigo ambao ujui kama ni mwepesi au ni mzito bali utaubeba.

Hali hii inabebwa na hali halisi katika upeo wa macho yako yaliyo kidhi hali yako inayotakiwa katika kukufanya kuwa uwe chini, ni wazi hakuna mtu anaipenda sana hali hii ila kunakuwa na shida kuwa kama hali hii ni tatizo au ndio maisha tunayotakiwa tuishi hivyo siku zote.
Ilikuondoa umasikini wa macho lazima utambue WAZO LA MUNGU KWAKO.

Na sio wazo lako binafsi au wazo la watu wengine wanaokuzunguka.Usihishi maadamu watu wanakaa duniani ndivyo wanavyoishi, bali jitahidi kujua na kutafuta wazo la Mungu katika maisha yako ili ikutambulishe wewe ni nani? Watu wengi utafuta kwa bidii kuwa na hali nzuri ya kielimu, kufedha na mengine mengi lakini tambua kitu kimoja jinsi utavyojitmbua katika kutambulishwa na Mungu hivyo ndivyo mazingira yatavyoambatana na wewe na sio namna nyingine japo sipo mbali na kutia bidii katika kila jambo jema unalolifanya.

Katika wazo la Mungu juu yako hapo ndipo kunakusafishwa kutoka katika umasiki wa macho na kuwa utajiri wa macho uliojaa utoshelevu wa kiMungu utakaoona wewe katika wakati sahihi na uliosimikwa na Mungu mwenyewe.


Imeandaliwa na;
           

                      Cothey Nelson............................................................................0764018535

Jumatatu, 8 Desemba 2014

KESHO SIHITAKI


KESHO INA NILILIA



Biblia inasema....lakini mtu huyu ndiye nitakaye mwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka atetemikaye asikiapo neno langu. Isaya 66:2b

Kulia ni jambo la kawaida katika dunia japo kuna kulia kwa kupenda na kulia kutopenda katika haya yote inabaki neon lile hili KULIA. Tena kubaliana kwa pamoja kuwa katika sehemu kubwa katika maisha ya mwanadamu uwa hawapendi kulia na katika kulia kunakuwa na sababu ya mtu kumfanya jambo hili.

Ni wazi kama jana haitakulilia sio jambo la kujivunia sana kwani kesho inaweza kulilia haya mambo uwa kwa sehemu kubwa na utaratibu au mfumo uliokuwako unakutengeneza au unaweza kuetengeneza au kuulekebisha.

Ni jambo lisilopingika mambo ambayo yanayosababisha kesho yako inaweza kutawaliwa na kilio sio kicheko japo inawezekana kuwa ulikuwa haupendi lakini uhalisia wake utajitokeza na kuchanua matawi yake;

I.umbali wa wewe na Mungu

Ninapozungumzia umbali wako na Mungu si zungumzi umbali unao onekana lakini nazungumzia umbali usionekana bali unauhalisia mkubwa na unadhihirika kwake ni mkubwa sana.

Ni bora uwe mbali na wazazi, walezi, marafiki,ndugu au jama wakiroho japo siku hizi mtu yuko radhi kuwa mbali na Mungu lakini awe karibu na marafiki,ndugu au mpenzi.

Uwezi ukawa mbali na mtu halafu ukategemea yale yake ya husike katika maisha yako hivyo unavyokuwa mbali na Mungu tegemea vya Mungu kupita mbali na maisha yako japo unaweza kuvipenda lakini utaratibu wake utasimama kama ulivyopangwa kwakila jambo la Mungu limebeba kusudi lake hivyo linafanya vile lilivyotumwa.

Kuwa na Mungu ni mbali na kusema mimi na mwamini Mungu na yupo kwakua naishi kwa nguvu zake bali kuwa karibu na Mungu ni zaidi ya chochote na vilevile sio swala la kuhisi tu bali ni udhihirisho ulio wa kutisha uliojaa mema mengi yanayo kuhusu wewe.

Mluhusu Mungu aitawale siku yako ili akutengenezee kesho yako iliyojaa matumaini isiyokoma na iliyokamilifu sana na iliyobeba ukamilifu usio pungua.

Na mluhusu vipi!-Nguvu ya sauti yake katika maisha yako;
Je katika maisha yako kipi kina nguvu kuliko kingine au cha maana sana kuliko sauti ya Mungu ndani yako, unahitajikujua kuwa kile unachokisiliza na kukikubali inatoa dira katika maisha yako inaweza kuwa dira sahihi au isiwe sahihi.

Je! Sauti ipi inatisha au ina nguvu kwako; mwenzi,mchumba,fedha,elimu au ushirika mwingine wowote!

Biblia inasema....lakini mtu huyu ndiye nitakaye mwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka atetemikaye asikiapo neno langu. Isaya 66:2b

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson.......................0764 018535